TANROADS YAENDELEA KULINDA BARABARA.
Na Ahmed Ahmed - Dodoma.
WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kulinda miundombinu ya barabara ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuwa salama kwa watumiaji wakati wote.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameyasema hayo Mei 20, 2025 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2026/2027.
"Kwa hakika haya ni mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya muda mfupi kwa upande wa miundombinu ya barabara na madaraka," alisema.
Ulega amesema barabara zinaendelea kuwa miundombinu muhimu ya usafiri nchini kutokana na kufika katika maeneo mengi ikilinganishwa na miundombinu mingine ya usafiri na usafirishaji.
Amesema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026, ukarabati wa kawaida ya barabara zenye urefu wa kilomita 16,782.58 umefanyika pamoja na marekebisho maalum ya kilomita 1,101.12.
















Maoni