KAMPENI YA TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIKA YAZINDULIWA UYUI
Na Lubango Mleka, Uyui.
KAMPENI ya “Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa” awamu ya pili imezinduliwa Oktoba 14, 2025 katika ukumbi wa VETA Uyui, ikiambatana na maandamano kutoka stendi ya Isikizya.
Uzinduzi huo umeongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uyui, SSP Edward J. Ituja, huku Afisa Tarafa Shaban Said akimwakilisha Mkuu wa Wilaya, Mh. Mohamed Mtulyakwaku kama mgeni rasmi.
Washiriki walihusisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, na chuo cha VETA, viongozi wa dini, wazazi na maafisa wa polisi.
Viongozi hao waliwahimiza vijana kuepuka matumizi ya dawa za kulevya, ukatili wa kijinsia na makundi hatarishi, huku wazazi wakisisitizwa kuchukua jukumu la malezi.
Mgeni rasmi aliwataka wanafunzi kutumia mitandao kwa uangalifu na kuwa mabalozi wa nidhamu na maadili mema katika jamii.








Maoni