MIILI YA WATU WANNE YAKUTWA KANDO YA BARABARA MAPINGA PWANI
Na Mwandishi Wetu, Pwani.
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani, limethibitisha kutokea kwa vifo vya wanaume 4 ambao miili yao imekutwa pembezoni mwa barabara ya Mapinga kuelekea Kibaha, ikiwa na majeraha usoni na miguuni.
Miili hiyo ambayo ilisafirishwa hadi Hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa uchunguzi zaidi na baadaye, wazazi na ndugu waliweza kuitambua miili hiyo ya vijana wanne kuwa ni wakazi wa Dar es Salaam, ambao ni Mikidadi Abbas Mikidadi (21), Hassan Juma Jumanne (21), na Fadhili Patrick Hiyola (19) amba oni deiwaka wa bodaboda Pamoja na dereva bajaji Abdalla Fadhil Nyanga (21) ambao wote walikuwa wanafanya shughuli zao Dar es Salaam.
Jeshi la Polisi limesema miili hiyo imekabidhiwa kwa familia kwa taratibu za mazishi baada ya uchunguzi wa kitabibu kukamilika huku uchunguzi wa kina kubaini mazingira na wahusika wa mauaji hayo unaendelea.
Jeshi la Polisi mkoani Pwani limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa yoyote inayoweza kusaidia kufichua ukweli wa tukio hilo na kusisitiza kuwa ushirikiano wa jamii ni muhimu ili kubaini kilichotokea na kuwachukulia hatua kwa waliosababisha vifo hivyo.



Maoni