MUUGUZI BANDIA AKAMATWA BAADA YA KUHUDUMIA WAGONJWA ZAIDI YA 4,000 FLORIDA.





MWANAMKE mmoja amekamatwa nchini Marekani kwa tuhuma za kujifanya muuguzi aliyesajiliwa.

Uchunguzi wa polisi ulianzishwa baada ya wakuu wa hospitali kukatisha kandarasi ya Autumn Bardisa kutokana na wasiwasi kuhusu sifa zake za kikazi.

Wachunguzi waligundua kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa ametoa huduma za matibabu kwa wagonjwa 4,486 kati ya Juni 2024 na Januari 2025.

"Hii ni moja ya kesi za kutatanisha zaidi za udanganyifu wa kimatibabu ambazo tumewahi kuchunguza," Mkuu wa Kaunti ya Flagler Rick Staly alisema.

Bardisa aliajiriwa na AdventHealth Palm Coast Parkway huko Palm Coast kuanzia Julai 2023 hadi Januari 2025.

Anadaiwa kuwasilisha hati za uwongo na kutoa nambari ya leseni ya muuguzi aliye na jina moja la kwanza ambaye aliajiriwa na AdventHealth katika hospitali tofauti.

Ofisi ya Kaunti ilisema alielezea tofauti hiyo kwa kudai kwamba alikuwa ameolewa hivi majuzi na amebadilisha jina lake la ukoo. Aliombwa kutoa leseni yake ya ndoa lakini hakufanya hivyo.

Mnamo Januari, Bardisa alipewa nafasi ya kupandishwa cheo. Mfanyakazi mwenzake alimripoti kwa mamlaka walipogundua kuwa leseni yake ya msaidizi wa uuguzi ilikuwa imeisha muda wake.

Mkataba wake ulikatishwa na uchunguzi wa uhalifu wa miezi saba ulianzishwa.

Maafisa wa upelelezi walitekeleza hati ya kukamatwa kwake kwa makosa saba ya kufanya kazi ya afya bila leseni na makosa saba ya ulaghai wa kutumia taarifa za kitambulisho.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.