TRUMP KUKUTANA NA PUTIN

RAIS Donald Trump wa Marekani amedokeza kuwa atakutana na na rais wa Urusi Vladimir Putin ana kwa ana hivi karibuni ili kujadili usitishwaji wa vita vinavyoendelea nchini Ukraine.



Trump amesema mkutano wake na Putin ni matokeo ya mazungumzo yenye tija kubwa yaliyofanyika mjini Moscow kati ya mjumbe wake maalum Steve Witkoff na Rais Putin. Urusi tayari imethibitisha kuhusu mkutano huo huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky nae akitoa wito wa kukutana ana kwa ana na Putin ili kuzungumza namna ya kuvimaliza vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu.





 #USA #Trump #Russia 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.