TAKUKURU MKOA WA MWANZA IMEFANIKIWA KUDHIBITI KIASI CHA TZS MILIONI 85.5

 


Na Mwandishi Wetu, Mwanza. 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kudhibiti kiasi cha Sh milioni 85.5 kupitia uchambuzi wa mfumo wa malipo ya fedha za kujikimu kwa walimu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Abnery Mganga, amesema kuwa katika utekelezaji wa majukumu ya kuzuia rushwa, taasisi hiyo ilifanikiwa kudhibiti kiasi hicho cha Sh milioni 85.5 na kuhakikisha kinalipwa kwa walimu waajiriwa wapya wa shule za sekondari waliokuwa na madai katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Aidha, Mganga amesema mafanikio hayo yametokana na uchambuzi wa mfumo uliofanywa na taasisi hiyo pamoja na halmashauri kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa katika kikao kazi kati ya TAKUKURU na wadau wa halmashauri. Hatua hiyo imewawezesha walimu 77 waliokuwa na madai kulipwa stahiki zao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.