YANGA YAICHAPA AS FAR 1–0, YAENDELEA KUWIKA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 











TIMU ya Yanga ambao ni Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya AS FAR Rabat katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika uliopigwa leo, Novemba 22, 2025, katika Dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Yanga SC walipata bao pekee la mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wao Prince Dube dakika ya 58, akimalizia kwa ustadi pasi ya kutengeneza nafasi iliyotolewa na Mudathir Yahya.

Kwa ushindi huo, Yanga SC wamefanikiwa kuvuna pointi tatu muhimu wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, na hivyo kujiweka kwenye mazingira mazuri katika harakati zao za kusaka nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo barani Afrika, na kuweka hisroria ya kuwa timu ya kwanza  kupata ushindi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.