SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO KAZI NA VIONGOZI WA POLISI CHINI.
Na Lubango Mleka, Arusha.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene, ameongoza kikao kazi na viongozi wa Jeshi la Polisi nchini kilichofanyika jijini Arusha, Novemba 21, 2025 ikiwa ni mara yake ya kwanza kuongoza kikao hicho baada ya uteuzi wake wa kuongoza Wizara hiyo
Waziri Simbachawene ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dennis Lazaro Londo, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Maduhu Kazi.




Maoni