WAFUGAJI WA JAMII YA KIMASAI HANDENI WAMETAKIWA KUEPUKA MIGOGORO NA KUSHIRIKIANA NA POLISI

 



Na Mwandidhi Wetu, Tanga.

WAFUGAJI kutoka vijiji vya Msomela na Kwamantuku, Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga, wametakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudhibiti matukio ya uhalifu na kudumisha amani katika jamii zao.

Wito huo umetolewa leo tarehe 22 Novemba 2025 na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Tanga, ACP Wambura, alipokutana na wawakilishi hao katika kikao cha majadiliano.

ACP Wambura amewaasa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi, kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu na kuchochea amani katika maeneo yao.

Aidha, Wafugaji hao wametoa pongezi kwa juhudi za Polisi Mkoa wa Tanga, na kuahidi kuendeleza mahusiano mema na wakulima, kuepuka migogoro, na kuwa mabalozi wa amani kwa kutoa taarifa za uchochezi au vurugu mara wanapozibaini.







Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.