WANAWAKE NKINGA HOSPITALI WAZINDUA KIKUNDI CHA KUSAIDIANA




Na Lubango Mleka, Nkinga - Igunga.

WANAWAKE watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga jana Disemba 11, 2025 wamezindua rasmi kikundi chenye lengo la kusaidiana katika changamoto mbalimbali za kimaisha.

Kikundi hicho kilichopewa jina la Nkinga Super Women Group kimezinduliwa katika Kikao cha kwanza cha Kufunga Mwaka, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ndg.Victor Ntundwe alikuwa ndiye mgeni rasmi.

"Ninawapongeza kwa kuunganisha nguvu ya pamoja katika kukabiliana na changamoto zenu, Siku zote Umoja ni nguvu, Uongozi wa hospitali unawathamini sana kwa jinsi mnavyoongoza wafanyakazi wengine kwa nidhamu, weledi na kuwa vinara wa huduma kwa mteja" amesema Mkurugenzi Ntundwe katika hotuba yake

Bi.Epifania Nyaki ni mwenyekiti wa Umoja huo amesema, kuanzishwa kwa Umoja huo ni matokeo ya mawazo katika sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani Machi, 2024 baada ya kushikwa mkono na Mkurugenzi wa Hospitali, na ndipo January 2025 kikundi hicho kikaanza rasmi.

Ameongeza, kwasasa kikundi hicho kina wanachama 30 na ametoa rai kwa Wanawake wengine kuendelea kujiunga bila kujali kiwango cha elimu, huku akisisitiza kwamba nikupitia Vikundi pekee ndipo wanaweza kukutana pamoja na kusaidiana.

Bi.Claracia Kabambo ni mmoja kati ya wana kikundi amesema, Wanawake watumishi hawapaswi kutegemea mshahara pekee bali wanapaswa kuwa na vyanzo vingine vya mapato, na kuwahimiza Wanawake wenzake kujiunga katika umoja huo.

Dr.Martha Ibrahimu ni katibu msaidizi wa kikundi hicho amesema, kikundi hicho kimefanyika baraka, kwani mwanakikundi anapopata changamoto au baraka hukutana pamoja na kushare mawazo na inasaidia kuimarika kwa Afya ya akili.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.