URA – SACCOS YAPATA HATI SAFI MIAKA TISA MFULULIZO.


 


Na. Lubango Mleka, Arusha. 

KAMISHINA wa fedha na lojistiki (CP) Liberat Sabas amekipongeza Chama cha ushirika cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS LTD) kwa kuendelea kupata hati safi kwa miaka tisa (9) mfululizo kutoka kwa mkaguzi wa nje, jambo ambalo limewezesha  kuwa chama bora kitaifa kwa miaka mitano mfululizo na kuwa  chama kinachoongoza kwa mtaji mkubwa, mali na idadi kubwa ya wanachama.

Kamishna Sabas yameyasema hayo leo Novemba 28, 2025 wakati akimwakilisha mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillius Wambura kufungua mkutano wa 17 wa chama hicho unaofanyika jijini Arusha. 

 “kupata hati hizo safi kwa mfululizo, zinaakisi uwazi na uadilifu wa uendeshaji makini wa chama chetu” alisema CP Sabas.

Matokeo ya ufanisi huo kwa mwaka 2025 yametokana na uongozi bora, nidhamu ya kifedha na moyo wa umoja na  kujituma  kwa watendaji wa chama hicho.

CP Sabas aliongeza kuwa uongozi bora na nidhamu ya kifedha imewezesha chama hicho kuwa na akiba ya shilingi bilioni 139, mikopo yenye thamani ya bilioni 108 ambazo zimetolewa kwa wanachama zaidi ya 51,000 ambao wanaendelea kunufaika na chama kwa kufanya shughuli za kiuchumi.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya chama hicho ambaye ni Kamishna wa Polisi Jamii CP Faustine Shilogile alisema kuwa mkutano huo ni muendelezo wa mikutano ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa lengo la kuimarisha utendaji na ufanisi wa chama URA -Saccos.

CP Shilogile alisema kuwa utararibu wa mikutano hiyo imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kutoa mafunzo, kujadili maendeleo ya chama, pamoja na kupitisha maazimio kwa manufaa ya wanachama na Jeshi la Polisi kwa ujumla.  Kupitia mafunzo hayo, wajumbe wa mkutano huo wamekuwa wakijengewa uwezo wa kiutendaji ili kuendelea kutoa huduma kwa wanachama na kukiimarisha chama.

Kwa upande wake Mrajisi msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Dar es salaam, Bi Angella Nalimi alisema kuwa anaitambua URA – Saccos kama chama bora kwa kuzingatia taarifa ya utendaji wa vyama vya ushirika (SACCOS) iliyozinduliwa Septemba 29, 2025, Ura -saccos imekuwa ya kwanza kwa ukubwa wa mali kati ya Saccos 20 bora   Tanzania.









Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.