RACHEL NJAU AMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAPATIA WANAWAKE LESENI

 


Na Mwandishi wetu, Mirerani 

MAKAMU Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini wanawake Tanzania (TAWOMA) Rachel Joseph Njau amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatia wanawak leseni za uchimbaji na ununuzi wa madini bila malipo.

Hivi karibuni Waziri wa Madini Anthony Mavunde aliwapatia leseni ya uchimbaji madini na leseni ya ununuzi wa madini wanawake na vijana 423 waliopo katika vikundi 21 wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.

Rachel ambaye pia ni Katibu wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Tawi la Mirerani ametoa shukrani hizo kwenye uchaguzi wa TAWOMA Tawi la Mirerani ambapo Magreth Nelson alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa TAWOMA kwa wanawake wafanyabiashara wa magonga ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite.

Ameeleza kwamba kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidia wanawake kwenye mpango huo kinaongeza idadi ya wanawake wanaonufaika na sekta ya madini.

"Tunampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumtuma Waziri Anthony Mavunde ambaye naye tunamshukuru kwa kutoa leseni hizo kwa ajili ya manufaa ya baadhi ya wanawake waliopo katika sekta ya madini,," amesema Rachel Njau.

Ameeleza kwamba Rais Dkt Samia amewajali na kuwathamini wanawake waliopo katika sekta ya madini kwa kuwapatia leseni hizo nao hawana cha kumlipa zaidi ya kusema sante sana.

Makamu Menyekiti huyo wa TAWOMA Taifa, amewasihi wanawake hao waongeza thamani madini ya Tanzanite kupendana, kushirikisha na kuondokana na maneno uzushi au masengenyo.

Hata hivyo, amewatoa hofu baadhi ya wanawake wanaodanganywa kuwa watafutiwa leseni wasihofie hilo kwani mwenye uwezo huyo hapo Mirerani ni afisa madini mkazi (RMO) George Kaseza.

"Tuachaneni na kelele zisizo na maana yoyote ile na vitisho kuwa kuna watu watafutiwa leseni ili hali wamepatiwa kihalali jamani, tuleni keki hii wote bila wasiwasi wowote" amesema Rachel.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.