HALMASHAURI YA MONDULI YATUA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR KUJIFUNZA




Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.

TIMU ya wataalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoani Arusha ikiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Happiness Laizer imefika katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa lengo kujifunza jinsi ya ukusanyaji wa mapato.

Timu hiyo imepokelewa na mwenyeji wao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji hilo ndugu Elihuruma Mabelya ambapo katika mazungumzo yake aliwaeleza wataalamu hao kuwa ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam unachangiwa na ushirikiano wa watumishi katika kanda maalum za ukusanyaji mapato.

Amesema uanzishwaji wa kanda hizo, umewezesha kuwasogezea wananchi huduma mbalimbali katika maeneo yao hali iliyochangia kuwapunguzia umbali wa kufuata huduma zikiwemo vibali mbalimbali, leseni n.k makao makuu ya Halmashauri.










Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.