SANGA AIPONGEZA CRDB KWA KUDHAMINI BUNGE BONANZA MIAKA MITANO MFULULIZO
Na Jasmine Shamwepu, Dodoma. MWENYEKITI wa Bunge Bonanza, Festo Sanga, ameipongeza CRDB Bank kwa kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa Bunge Bonanza kwa miaka mitano mfululizo, akisema mchango wa benki hiyo umekuwa nguzo muhimu katika mafanikio na ukuaji wa tukio hilo kila mwaka. Akizungumza katika Bunge Grand Bonanza lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Sanga amesema ushirikiano wa CRDB umechangia kuifanya shughuli hiyo kuwa zaidi ya tukio la michezo, kwa kuwa imekuwa jukwaa la kuimarisha afya, mshikamano na mahusiano mema miongoni mwa wabunge, watumishi wa Bunge na wadau mbalimbali. Amesema udhamini wa benki hiyo umewezesha bonanza hilo kuendelea kukua na kuvutia ushiriki mkubwa zaidi mwaka hadi mwaka, hali inayodhihirisha umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za umma na sekta binafsi katika maendeleo ya jamii. “Kwa mwaka wa tano mfululizo CRDB imeendelea kusimama nasi katika kufanikisha Bunge Bonanza. " Tunatoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB...