CCM YATAKA WATENDAJI, WATAALAMU KUWAJIBIKA IPASAVYO
Na Gilbert Dioniz na Allan Kitwe, Ngara CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Ngara Mkoani Kagera kimewataka Watendaji na Wataalamu waliopewa dhamana kusimamia miradi ya maendeleo kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao ili kuharakisha maendeleo ya wananchi. Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngara Vitalice Ndairagije kwenye ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya kukagua miradi ya maendeleo. Amesema kuwa kiu ya wananchi ni kuona miradi inayotekelezwa na serikali yao inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, na hili haliwezi kufanikiwa kama Watendaji na Wataalamu waliopewa dhamana hawatafanya kazi kwa weledi. ‘Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuleta mamilioni ya fedha hapa Ngara kwa ajili ya miradi ya maendeleo, fedha hizi tunataka zifanye kazi iliyokusudiwa na zisimamiwe ipasavyo’, amesema. Mwenyekiti alidokeza kuwa miradi ikisimamiwa ipasavyo itakamilika kwa wakati na thamani ya fedha zilizotumika ...