WADAU WA KILIMO WAOMBA SERIKALI KUONDOA KODI YA ONGEZEKO (VAT)
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
WADAU wa Kilimo wameiomba serikali kuondoka kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya asilimia 18 kwenye mifuko ya tabaka ya kuhifadhia mazao ya nafaka na mbegu ili kuwesha wakulima kuongeza kipato na usalama wa chakula.
Hayo yalielezwa Jijini Dodoma na Afisa Mradi Jukwaa la Wadau wa Kilimo wasiokuwa wa Kiserikali (ANSAF) Werner Hillary wakati akifungua warsha ya kujadili maboresho ya kisera ili kudhibiti changamoto za upotevu kwa wakulima wadogo kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas.
" Warsha hii ilitohusisha wadau mbalimbali wa Kilimo ikiwemo Serikali, wazalishaji wadogo na Asasi za Kiraia ni sehemu ya mradi unaotekelezwa kwa ushirikiani wa Helvetas Tanzania, SAT, Chuo cha Kilimo SUA na Chuo Kikuu cha Zurich.
Afisa huyo amesema lengo la wadau kuiomba Serikali kuondoa kodi ya VAT ni kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kununua na kutumia mifuko hiyo inayozuia wadudu waharibifu na upotevu wa nafaka.
"Matumizi ya mifuko ya tabaka husaidia wananchi kujikinga na njaa kwa kuhifadhi chakula kwa muda mrefu bila kuharibiwa na wadudu. Mifuko hii ni muhimu kwa afya ya binadamu na ubora wa bidhaa sokoni," alisema.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Kilimo (SUA), Dk. Ramadhani Majubwa ambaye ni mmoja wa watekelezaji wa mradi, amesema katika tafiti walizofanya walibaini muamko wa wakulima kutumia mifuko hiyo ni mdogo.
Amesema mradi huo a4unalenga kuhamasisha matumizi ya mbinu bora za uhifadhi wa mazao ndio maana wamekutanisha wadau ili kujadiliana na kupata muafaka wa pamoja juu ya mapendekezo ya maboresho ya kisera juu ya mifuko ya tabaka.
Dk. Majubwa amesema mradi huu ulifanya tafiti ambayo iliangalia mambo mawili; moja likiwa ni kuangalia athari za kuondoa VAT na pili ulipaji wa baadaye wakati mkulima ameshauza mazao yake.
"Mifuko hiyo inapunguza upotevu na uharibifu wa mazao baada ya kuvuna na kupunguza njaa kutokana na kuzuia uvamizi wa wadudu. Tafiti imedhihitisha kuwa serikali ikiondoa VAT ya 18% wakulima wengi wataweza kununua mifuko hiyo na kuhifadhi chakula kwa tija," alisisitiza.




Maoni