KALEYA MOLLEL ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA SIMANJIRO
Na Mwandishi wetu, Simanjiro DIWANI wa Kata ya Msitu wa Tembo, Kaleya Melita Mollel amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, kwa kura zote 24 za Madiwani waliohudhuria kikao. Mwakilishi wa Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro, Edosi Evaristi Ndikwiki amesema Mollel ambaye ni Diwani wa Kata ya Msitu wa Tembo, amepata kura zote 24 zilizopigwa Ndikwiki pia amesema, madiwani hao wamemchagua Diwani viti maalum wa Tarafa ya Terrat, Mwanjaa Jacob kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kura zote 24 za ndiyo. Amesema katika uchaguzi huo uliofanyika mji mdogo wa Orkesumet ulihusisha madiwani wote wanaotokana na CCM wa kata zote 18 na viti maalumu sita. Ndikwiki amewaasa madiwani hao kutoa ushirikiano kwa wataalam wa halmashauri hiyo kwani wameshaapa kutumikia nafasi zao. "Tuzingatie mahusiano mazuri na watumishi, tuwape ushirikiano na tuwe watatuzi wa migogoro tusiibue migogoro ambayo itaturudisha nyu...