Machapisho

RC MTANDA AKABIDHI PIKIPIKI 18 KWA VIKUNDI 2 VYA VIJANA BUCHOSA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 23 Juni, 2026 amekabidhi pikipiki 18 zenye thamani ya Tshs. Milioni 54.9 vya vikundi viwili vya vijana vya Bodaboda Lugasa na Waungwana Group Mbugani. Akiongea kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mhe. Mtanda ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye eneo la matumizi ya fedha za mapato ya ndani kwa maendeleo ya wananchi. Halmashauri ya Buchosa inafanya vizuri sana , kwanza kwenye kukusanya mapato na pili kwenye kutumia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwa kutumia mapato yao kununua vyombo kama pikipiki na kukopesha kwa vijana. Amesema Mkuu wa Mkoa. Aidha, ametoa wito kwa halmashauri hiyo kusimamia urejeshaji wa mikopo hiyo ili itumike kununua zingine na kuwezesha makundi mengine yaweze kukopeshwa. Aidha, amewataka vijana walionufailka na mkopo huo kuheshimu sheria za usalama barabarani kwa kuendesha kwa staha kwa usalama wao na wa watumia barabara wengine aidha kuzitumia pia kwa mal...

NIMERIDHIKA NA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA HALMASHAURI - RC MTANDA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kwa kufikia malengo kwenye ukusanyaji na matumizi mazuri ya fedha za makusanyo na kisha kuwataka kuendelea kukamilisha miradi ya maendeleo. Ametoa agizo hilo leo tarehe 23 juni, 2026 wakati akihutubia Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) 2024/25. "Siku za nyuma nilikuwa nawasema sana kwenye ukusanyaji wa mapato na matokeo duni kwenye matokeo ya elimu ya Msingi na Sekomdari ila kwa sasa mmenyanyuka sana kwenye maeneo yote hayo kwakweli napenda kuwapongeza sana na nawataka muendelee hivi hivi". RC Mtanda. Aidha, ametoa wito kwao kuendelea kusimamia matumizi mazuri ya dawa na kuhakikisha zinawafikia wananchi na kutorohusu kuzihifadhi hadi zinafikia mwisho wa matumizi jambo linaloisababishia hasara kwa Halmashauri. ...

EWURA CCC YATOA MWANGA KWA WANANCHI WASIOJUA PAKUPELEKA MALALAMIKO

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma Zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) limesema zaidi ya wananchi 500 wametembelea banda lake katika Wiki ya Utumishi wa Umma na kupata elimu, ushauri pamoja na fursa ya kuwasilisha malalamiko yanayohusu huduma za maji, umeme na gesi. Afisa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa EWURA CCC, Amani Mbogo, amesema baraza hilo lina jukumu la kulinda na kutetea maslahi ya watumiaji wa huduma za nishati na maji kwa kuhakikisha sauti zao zinasikika na changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi. Akizungumza katika Wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea jijini Dodoma, Mbogo amesema wananchi wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohusiana na huduma za maji na nishati, lakini hawafahamu mahali pa kupeleka malalamiko yao ili kupata msaada. “Tumepokea wananchi wengi waliokuja kupata elimu kuhusu majukumu ya EWURA CCC, kutoa maoni, ushauri na kuwasilisha malalamiko yao. Mwitikio umekuwa mkubwa na unaonyesha umuhimu wa k...

SANGA AIPONGEZA CRDB KWA KUDHAMINI BUNGE BONANZA MIAKA MITANO MFULULIZO

Picha
Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  MWENYEKITI wa Bunge Bonanza, Festo Sanga, ameipongeza CRDB Bank kwa kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa Bunge Bonanza kwa miaka mitano mfululizo, akisema mchango wa benki hiyo umekuwa nguzo muhimu katika mafanikio na ukuaji wa tukio hilo kila mwaka. Akizungumza katika Bunge Grand Bonanza lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Sanga amesema ushirikiano wa CRDB umechangia kuifanya shughuli hiyo kuwa zaidi ya tukio la michezo, kwa kuwa imekuwa jukwaa la kuimarisha afya, mshikamano na mahusiano mema miongoni mwa wabunge, watumishi wa Bunge na wadau mbalimbali. Amesema udhamini wa benki hiyo umewezesha bonanza hilo kuendelea kukua na kuvutia ushiriki mkubwa zaidi mwaka hadi mwaka, hali inayodhihirisha umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za umma na sekta binafsi katika maendeleo ya jamii. “Kwa mwaka wa tano mfululizo CRDB imeendelea kusimama nasi katika kufanikisha Bunge Bonanza. "  Tunatoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB...

TANZANIA IPO TAYARI KUPOKEA AFCON 2027

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Sillo, amesema maandalizi ya kuelekea Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 yanaendelea vizuri, huku akibainisha kuwa Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kupokea na kuandaa mashindano hayo kwa mafanikio. Sillo ametoa kauli hiyo wakati wa Bonanza la Bunge (Bunge Grand Bonanza) lililofanyika jijini Dodoma, ambapo amesema kaulimbiu ya bonanza hilo inayohusiana na AFCON 2027 ni ishara ya namna Watanzania wanavyoendelea kuhamasika na kujiandaa kwa tukio hilo kubwa la kimichezo. Amesema maandalizi yanayoendelea kufanywa na Serikali, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya michezo na huduma nyingine muhimu, yanaonyesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha Tanzania inakuwa mwenyeji bora wa mashindano hayo ya kihistoria. “AFCON 2027 ni fursa kubwa kwa Tanzania kujitangaza kimataifa kupitia sekta ya michezo. Sisi kama Bunge tutaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuhakikisha maandalizi ...

WENYEVITI WA VIJIJI WA MONDULI WAMLIPUA MBUNGE WAO ISACK JOSEPH KWA KAULI YA KUNYANG'ANYWA MIHURI

Picha
Na Hamida Ramadhan, Monduli.   Mvutano mkubwa umeibuka katika Jimbo la Monduli baada ya Mbunge wa Jimbo hilo, Mheshimiwa Isack Joseph Copriano maarufu kama Kadogoo, kutoa kauli bungeni akiunga mkono hatua ya wenyeviti wa vijiji kunyang'anywa mihuri ya Serikali, kauli ambayo imezua hasira na malalamiko kutoka kwa viongozi wa Serikali za Mitaa katika wilaya hiyo. Wenyeviti hao wanasema kauli ya Mbunge wao imewadhalilisha, imewashushia hadhi mbele ya wananchi na imeondoa imani ya wananchi kwa viongozi waliowachagua kwa kura. Sintofahamu hiyo ilianza baada ya Mbunge Copriano kuchangia bungeni kuhusu migogoro ya ardhi na matumizi ya mihuri ya Serikali, ambapo alisema wazi kuwa anaunga mkono hatua ya kunyang'anywa kwa wenyeviti wa vijiji mihuri hiyo. Akizungumza bungeni, Mbunge huyo alisema: "Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro, na mimi nimefurahi sana na wenyeviti wa vijiji watanisamehe niwapongeze sana TAMISEMI kwa kunyang'anya wenyeviti wa vijiji mihuri. Wanyang'anyeni wa...

ZIMAMOTO YAWAKARIBISHA WANANCHI KUPATA ELIMU YA UOKOAJI KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  WANANCHI wametakiwa kutumia fursa ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kutembelea banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kupata elimu ya kujikinga na majanga ya moto pamoja na mbinu za uokoaji wakati wa dharura. Akizungumza katika maadhimisho hayo yanayoendelea jijini Dodoma, Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi, alisema banda la jeshi hilo limekuwa likitoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kuokoa maisha na mali pindi majanga yanapotokea. Amesema wananchi wanaofika katika banda hilo wanapata mafunzo kuhusu hatua za kuchukua kabla, wakati na baada ya kutokea kwa majanga ya moto pamoja na maafa mengine yanayohitaji huduma za uokoaji. "Tunatumia maonesho haya kukutana moja kwa moja na wananchi na kuwapa elimu itakayowasaidia kujikinga na majanga pamoja na kuelewa namna ya kushirikiana na jeshi la zimamoto wakati wa dharura," amesema. Nzalayaimisi ameleza kuwa elimu hiyo ni sehemu ya mkakati wa jeshi hilo wa ku...

VETA YAONESHA BIDHAA ZINAZOTENGENEZWA NA WANAFUNZI WAKATI WA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetumia maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuonesha bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanafunzi wake, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kutambua mchango wa mafunzo ya ufundi stadi katika maendeleo ya kiuchumi. Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa Rasilimali Watu wa VETA, Eliaika Manyanga, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, alisema bidhaa zinazooneshwa zimetengenezwa na wanafunzi kwa kushirikiana na walimu wao kupitia mafunzo ya vitendo yanayotolewa katika vyuo vya VETA. Alisema bidhaa hizo zinajumuisha vifaa mbalimbali vya matumizi ya nyumbani na ofisini vinavyotumiwa na makundi tofauti ya jamii, huku vikionesha kiwango cha ujuzi na ubunifu unaopatikana kwa wahitimu wa taasisi hiyo. Manyanga alisema VETA inaendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu yanayolenga kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajirika, huku akibainisha kuwa udahili wa wanafunzi kwa muhula ...

ASMA MWINYI FOUNDATION YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  MWANZILISHI na Mkurugenzi wa Taasisi ya Asma Mwinyi Foundation, ambaye pia ni Mbunge wa Welezo, Unguja, Asma Ally Hassan Mwinyi, ameungana na watoto wenye usonji (Autism), ugonjwa wa Down Syndrome na mtindio wa ubongo (Cerebral Palsy), pamoja na wazazi wao, kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kuwapa fursa ya kusikika na kujadili changamoto zinazowakabili. Katika maadhimisho hayo ya Juni 16, Asma Mwinyi Foundation kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe iliandaa ziara maalumu ya watoto hao na wazazi wao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, ambapo walipata nafasi ya kuzungumza na viongozi na kueleza changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha ya kila siku. Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Asma alisema lengo la kuwakutanisha watoto hao na wazazi wao ni kuendelea kutoa elimu kwa jamii, kuondoa unyanyapaa na kuhamasisha upatikanaji wa huduma bora za afya na matibabu kwa watoto wenye mahitaji...

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAHIMIZA VIJANA KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WAZIRI ya Viwanda na Biashara imewahimiza wananchi, hususan vijana na wajasiriamali, kutumia kikamilifu fursa zinazotolewa na taasisi zake ili kukuza biashara, kuongeza kipato na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa. Wito huo umetolewa leo Juni 17, 2026 na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Saidi Msabimana, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. Msabimana amesema wizara hiyo, ambayo ni miongoni mwa taasisi muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, imeshiriki maonesho hayo pamoja na taasisi nane zilizo chini yake kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi pamoja na kutoa elimu kuhusu biashara, viwanda na uwekezaji. Amesema jukwaa hilo limetumika kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa kuwapa taarifa za huduma zinazotolewa na kuwaelekeza namna ya kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla. “Tunatumia jukwaa hili ku...

NBS YAONA TAKWIMU NI NGUZO MUHIMU YA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema takwimu rasmi zitakuwa nyenzo muhimu katika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kuifikisha Tanzania katika uchumi wa dola trilioni moja na kuongeza kipato cha wananchi. Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa NBS, Daniel Masolwa, alisema hayo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, ambapo taasisi hiyo inashiriki kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma na majukumu yake. Masolwa amesema kaulimbiu ya mwaka huu inayosema “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu” imeipa NBS fursa ya kueleza umuhimu wa takwimu rasmi katika kupanga maendeleo, kufanya maamuzi sahihi na kufuatilia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya taifa. Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu, Sura ya 351, NBS imepewa mamlaka ya kukusanya, kuchakata na kusambaza takwimu rasmi zinazotumika katika sekta mbalimbali za maendeleo. “Takwimu rasmi ni msingi wa upangaji ...

WANANCHI WATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA WATOTO

Picha
Na. Wellu Mtaki, Dodoma.  Wazazi na walezi wamehimizwa kuwalea watoto katika maadili mema ili kuwaepusha na tabia za kuiga zisizofaa ambazo zinaweza kuwaletea madhara katika maisha yao.  Sambamba na hilo, wananchi wametakiwa kutambua na kuheshimu haki za watoto ili kuhakikisha wanakua katika mazingira salama na yenye upendo. Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Faithmary Lukindo, alipokuwa akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Eliakim Chacha Maswi, katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Kituo cha Malezi ya Watoto Kikombo jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kijiji, viongozi wa dini, wastaafu pamoja na waimbaji wa Kwaya ya Gethsemane. Akizungumza katika hafla hiyo, Lukindo alisema mtoto anapopewa haki ya kusikilizwa na kutoa maoni yake, hujengewa hali ya kujiamini na kujiona mwenye thamani ndani ya familia na jamii inayomzungu...

CCM YASHITUKA KUHUSU MIKUTANO YA KUCHOCHEA MAAANDAMANO.

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinazo taarifa zinazoashiria kuwepo kwa mikutano inayofanywa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambayo inadaiwa kuhusisha mipango ya kuhamasisha maandamano yenye uwezekano wa kuvuruga hali ya amani nchini. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa CCM anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, alisema chama hicho kimeendelea kuwataka Watanzania kuzingatia umuhimu wa utulivu na mshikamano wa kitaifa. Kihongosi ameeleza kuwa CCM inaamini maendeleo endelevu hayawezi kupatikana iwapo kutakuwa na misukosuko ya kisiasa, akisisitiza kuwa tofauti za vyama zinapaswa kuishia kwenye majadiliano ya sera. Alisema chama hicho kinatoa tahadhari kwa wananchi kutoshawishika kushiriki katika matukio yanayoweza kusababisha machafuko, akibainisha kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa. “Taarifa tulizonazo zinaonyesha k...