MOKIA OLE MREFU AWATAKIA KILA LA HERI MAKIBA SEKONDARI
Na Mwandishi wetu, Arumeru. MWENYEKITI wa chama cha wafanyabishara wa madini Mkoa wa Manyara na kurugenzi ya Habari na Mawasiliano wa chama cha wafanyabishara wa madini Taifa (CHAMMATA) Mokia Ole Mrefu, amewajengea uwezo na kuwapa moyo wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari Makiba Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, wanaotarajia kufanya mtihani wao wa kuhitimu hivi karibuni. Ole Mrefu amezungumza na wanafunzi hao kwenye maadhimisho ya miaka 30 tangu shule hiyo ianzishwe na mahafali ya 15 ya kidato cha sita kwa kuwatakia kila la heri katika mtihani wao wa kuhitimu. 'Hongereni sana vijana wetu jasiri wa kidato cha sita mnaojiandaa kuhitimu, leo nasimama kuwapa moyo na kuwakumbusha jambo moja muhimu: mmefika hapa si kwa bahati, bali kwa juhudi, nidhamu, na uvumilivu wenu," amesema Ole Mrefu . Ameeleza kwamba safari waliyoipitia imekuwa na changamoto nyingi, masomo magumu, mitihani ya majaribio, na nyakati za kuchoka, lakini bado mmesimama imara, hiyo peke yake ni ushin...