HATUA MPYA PANGANI! USAMBAZAJI WA MITUNGI YA GESI YA RUZUKU WAANZA RASMI
Na Mwandishi Wetu Pangani. WILAYA ya Pangani mkoani Tanga imepiga hatua muhimu katika kuboresha maisha ya wananchi wake kupitia utambulisho wa mradi wa uuzaji na usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku. Mradi huo unalenga kuongeza upatikanaji wa nishati safi na salama ya kupikia, hususan kwa kaya zenye kipato cha chini. Akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha mradi huo mbele ya katibu tawala wa Wilaya ya Pangani, Bi. Ester Gama, msimamizi wa mradi kutoka REA, Ndugu Abdulrazack Mkomi ameeleza kuwa lengo kuu la mradi huo ni kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, ambayo yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira pamoja na athari za kiafya kwa wananchi, hasa wanawake na watoto. Alifafanua kuwa kupitia mradi huo, mitungi ya gesi ya kilo sita itapatikana kwa bei nafuu ya shilingi 17,500 tu kutokana na ruzuku iliyotolewa, hali itakayowezesha wananchi wengi zaidi kuimudu na kuanza kutumia nishati mbadala iliyo rafiki kwa mazingira. Aidha, mfumo mz...