Machapisho

AKAMATWA NA POLISI KWA KUTOA MIMBA YA MIEZI 6

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora JESHI la Polisi Mkoani Tabora linamshikilia mwanamke mmoja (21) mkazi wa Mtaa wa Singo, Kata ya Gongoni katika halmashauri ya manispaa Tabora kwa tuhuma za kutoa ujauzito wake unaokadiriwa kuwa na umri wa miezi 6. Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Richard Abwao amethibitisha kutokea tukio hilo Aprili 6 mwaka huu majira ya saa 12.45 za jioni katika Kata hiyo ambapo mwanamke huyo mpare, mkristo na mkulima aligundulika kufanya kitendo hicho. Amesema kuwa mtuhumiwa baada ya kumeza dawa ya kutoa ujauzito huo, uchafu aliuweka kwenye kopo na kuufunga kwenye mfuko ili akautupe kwenye shimo la takataka lililo jirani na eneo hilo. Kamanda ameongeza kuwa mbali na mtuhumiwa huyo pia wamemkamata mwanaume mmoja (25) msukuma, mkazi wa Kata ya Chemchem katika manispaa hiyo ambaye ni Mtaalaumu wa Maabara aliyempatia dawa za kutolea mimba hiyo. Ameeleza sababu ya kutoa ujauzito huo kuwa ni mwanaume aliyempa mimba hiyo kuikataa hivyo akaamua kwenda kwa Mtaalaumu binafsi wa Maabara ili ...

MRADI WA ESP KUNUFAISHA WASICHANA ZAIDI YA 60 NZEGA.

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora.  WASICHANA zaidi ya 60 wanaotoka katika familia zisizo na uwezo Wilayani Nzega Mkoani Tabora wanatarajiwa kunufaika na mradi wa uwezeshaji mtoto wa kike kupata ujuzi (Empowerment Through Skills Program in Tanzania-ESP). Mradi huo unaofadhiliwa na nchi ya Canada (Canada Fund) kwa lengo la kuwezesha watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kupata fursa za ujuzi, unatekelezwa katika Vyuo 12 viivyopo katika Mikoa zaidi ya 8 hapa nchini. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Mwanhala, Nzega ni miongoni mwa vyuo 12 vilivyoingizwa katika program ya ufadhili ili kutoa mafunzo hayo ya muda mfupi (short course) kwa watoto wa kike.   Akizungumza juzi na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho Enock Lalida, Afisa Utumishi Hekima Amri Lupembe ameeleza kuwa mradi huo ni muhimu sana kwa kuwa unawapa fursa watoto wa kike kupata ujuzi. ‘Wasichana 30 wanaotoka katika kaya zinazoishi katika mazingira magumu Wilayani hapa tayari wamesajiliwa na kuan...

RUWASA KIGOMA WAMWAGA PONGEZI KWA RAIS SAMIA

Picha
  Na Allan Kitwe, Kigoma.  WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoani Kigoma wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 79 za miradi ya maji. Pongezi hizo zimetolewa na Meneja wa Wakala huo Mkoani hapa Mhandisi Mathius Mwenda alipokuwa akiongea kwenye mahojiano maalumu na waandishi wa habari Ofisini kwake. Amesema kuwa RUWASA Kigoma ina kila sababu ya kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kufanikisha utekelezaji miradi mbalimbali ya maji katika Wilaya zote 7 za Mkoa huo hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa kero ya maji. Mhandisi Mwenda amebainisha kuwa kuanzia Machi 2021 hadi Februari 2026, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alitenga zaidi ya shilingi bilioni 79 kwa ajili ya kutekeleza miradi 113 ya maji katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo. Amedokeza kuwa kati ya kiasi hicho cha fedha, serikali ilitoa jumla ya shilingi bilioni 55.9 na wadau wakaiunga mkono kwa kutoa kiasi cha shiling...

ASKOFU MEIVUKIE AASA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora WAKRISTO na jamii kwa ujumla wameaswa kuchukua tahadhari na kumwomba Mungu ainue wapatanishi dhidi ya mataifa ya Marekani, Israel na Iran ili vita inayoendelea sasa baina yao imalizike kwa amani ili kuepusha athari kwa jamii. Wito huo umetolewa jana na Askofu Paul Meivukie wa Kanisa la TAG-Jimbo la Tabora Kati ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kitete Christian Centre (KCC) alipokuwa akitoa salamu za pasaka kwenye ibada kanisani hapo. Amesema kuwa athari za vita vinavyoendelea sasa katika mataifa hayo ni kubwa mno, na Tanzania sio kisiwa, haiwezi kujitegemea kwa kila kitu, hivyo ni muhimu sana kumwomba Mungu na kutumia vizuri chakula tulicho nacho. Huu sio wakati wa kulaumu viongozi bali kuwaombea ili Mwenyezi Mungu awaongoze na kuwapa hekima ya kutoa maamuzi sahihi ili kuepusha bei za bidhaa kupanda zaidi hali inayoweza kuleta shida kwa wananchi. ‘Sote tunafahamu vita inayoendelea baina ya Marekani, Israel na Iran, naomba tuendelee kuchukua taha...

AFISA USAFIRISHAJI SIMANJIRO KORTINI KWA WIZI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro.  Afisa usafirishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Ismail Khalifan amefikishwa mahakamani kwa kosa la jinai la wizi wa shilingi 500,000 akiwa mtumishi wa umma. Afisa usafirishaji huyo Ismail amefikishwa kwenye mahakama ya wilaya ya Simanjiro na kusomewa shitaka hilo la wizi wa shilingi 500,000 fedha ambazo ni mali ya Halmashauri hiyo. Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) Faustin Mushi amesoma shataka hilo Aprili mosi, 2026 mbele ya hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro Charles Uisso. Mushi amesema Ismail anashtakiwa kwa kosa la wizi akiwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 258 (1), 265 na 270 vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya  16 R:E 2023. Amesema Ismail anashitakiwa kwa kosa la wizi wa shilingi 500,000 alizopewa na mwajiri wake kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya magari ya halmashauri ya wilaya hiyo. Amesema katika kesi hiyo ya jinai namba 7118/2026...

MWENYEKITI MAREMA AWASIHI WACHIMBAJI KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO

Picha
  Na mwandishi wetu, Mirerani.  MWENYEKITI wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Elisha Nelson Mnyawi amewaomba wadau wa madini kujitolea na kuwasaidia waathirika wa mafuriko katika Tarafa ya Moipo. Mwenyekiti huyo wa MAREMA Mnyawi ameyasema hayo mji mdogo wa Mirerani, leo jumapili Machi 29,2026 wakati akikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mwalimu Fakii Raphael Lulandana vyakula na vifaa vya thamani ya shilingi milioni 22 vilivyotolewa na kampuni ya Permanent Mining LTD kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika Tarafa ya Moipo. Ameeleza kuwa japokuwa wachimbaji madini wamekuwa wakijitoa mara kwa mara kupitia hisani kwa jamii (CSR) wasiliache hilo likapita bila kuchangia chochote. Amesema wachimbaji mbalimbali ikiwemo Franone Mining, God Mwanga, Chusa Mining, California Camp, Bilionea Saniniu Laizer, Sunda Mining wamekuwa wakisaidia jamii wasaidie pia waathirika hao waliokumbwa na mafuriko. "Kupitia hadhara hii nampongeza Mkurugenzi wetu God Charity amba...

MTI MMOJA, ENEO AMBALO SIMBA HULITUMIA KWA HONEYMOON KRETA YA NGORONGORO.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro.  UNAWEZA kustaajabu lakini ukweli upo hivyo, ukitaka kuwaona simba wakiwa katika harakati za kuongeza familia fika katika  Kasoko ya Ngorongoro eneo la mti mmoja ambalo limezungukwa na vichaka, miti na nyasi za wastani. Eneo hili ni maarufu sana kwa waongoza utalii kutokana na makundi ya simba waliopo katika hifadhi hiyo kupenda kupumzika  na hasa wanapokuwa katika msimu wao wa kujamiina ama kutafuta watoto na kuongeza familia. Simba hupenda kujamiiana mara baada ya kushiba ambapo zoezi hilo linafanyika mda wowote mchana au usiku. Tofauti na Binadamu ambapo Kazi Ngumu hufanywa na wanaume, kwa Simba ni tofauti, kazi ya kutafuta chakula ama Mawindo kwa ajili ya msosi wa familia huongozwa na simba jike ambapo mara baada ya kuhisi njaa na tamaa ya kujamiina huamua kutafuta chakula ili kwanza kushiba halafu kuingia kwenye harakati ya kuongeza familia. Wakati wa mawindo simba huchagua chakula cha kushiba na hapa ina maana simba hahangaiki s...

TANZANIA YASHINDA TUZO YA KIMATAIFA YA UFADHILI WA MIUNDOMBINU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Afrika Kusini.  SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha imeendelea kung’ara kimataifa baada ya kushinda tuzo ya “Infrastructure Finance Deal of the Year 2026” zinazotolewa na Global Banking & Markets, kufuatia mafanikio ya upatikanaji wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.78 kwa ajili kugharamia ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme (SGR) kwa kipande cha tatu na cha nne. Tuzo hiyo imepokelewa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, kwa niaba ya Wizara ya Fedha katika hafla ya utoaji Tuzo za Global Banking & Markets iliyofanyika jijini Cape Town, Afrika Kusini. Ushindi huo unatokana na mpango mahiri wa utafutaji ufadhili wa mradi huo mkubwa wa kimkakati, unaotarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi na kurahisisha usafirishaji nchini na Ukanda wa Maziwa Makuu, mkopouliopatikana kupitia ushirikiano kati ya taasisi za bima kutoka nchi za Sweden, Poland na Italy pamoja na Benki za Maendeleo za Kikanda, chini ya uratibu wa Benki ya St...

DAKTARI HATIANI KUUZA SARUJI NA MATOFALI ZAHANATI SUKURO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro.  MGANGA mfawidhi wa zahanati ya kijiji cha Sukuro kata ya Komolo wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Dk Daud Ndagala ametiwa hatiani kwa ubadhirifu wa mifuko ya saruji na matofali ya kukarabati zahanati hiyo. Mahakama ya wilaya ya Simanjiro imemtia hatiani Dk Ndagala kupitia shauri la jinai namba 4344/2026 kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi. Hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro Charles Uisso amesoma hukumu hiyo Machi 26,2026 na mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kituo maalum cha Mirerani Gervas Sarakikiya. Hakimu Uisso ameieleza mahakama hiyo kuwa Dk Ndagala ametiwa hatiani kwa kufuja Sh1 milioni za mauzo ya mifuko 57 ya saruji ya kukarabati zahanati hiyo. Amesema pia, Dk Ndagala alichepusha tofali 220 zilizoandaliwa kwa ajili ya ukarabati huo kisha akaziuza Sh605,000 kwa mtu binafsi. Amesema mshtakiwa huyo amefanya makosa hayo akitumia nafasi yake ya mganga mfawidhi wa zahanati ya ...

MAMBO YALIYOJIFICHA KUHUSU HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA UDZUNGWA

Picha
  1. Hifadhi ina njia mbalimbali za matembezi ya miguu na jumla ya Maporomoko ya maji 6 (Sanje, Sonjo, Njokamoni, Prince Benhard, Ichonde na Mwaya). 2. Vilele vikubwa vya  Milima (Luhomero mita 2,576  na Mwanihana mita 2,500 kutoka usawa wa bahari). 3. Kitovu cha Viumbe Adimu. Udzungwa ina viumbe wengi adimu ambao huwezi kuwapata mahala popote duniani. Spishi hizo ni pamoja na jamii mbili za primata (Ngolaga wa Sanje na Mbega wekundu wa Iringa), Spishi 2 za ndege (Kware wa Milima ya Udzungwa na “Rufous-winged Sunbird), Spishi 4 adimu za mimea ambapo moja wapo ni “Vernonia luhomeroensis”, Spishi 3 za vipepeo ambazo ni pamoja na “Charaxes lucyae mwanihanae”, Spishi ya Nyoka aitwaye “Red Snouted Wolf Snake na viumbe wengine wengi. 4. Baadhi ya Spishi nyingine adimu zinapatikana katika Milima ya Tao la Mashariki (Eastern Arc Mountains) baadhi ya spishi hizo  ni pamoja na Kinyonga Mfupi (Pygmy Chameleon).  #UdzungwaNountainsNationalPark #HikingParadise #tanzaniaparks...

UFAWAZA WAIPONGEZA DOREFA KWA USIMAMIZI NA UENDESHAJI SOKA DODOMA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  UMOJA wa Wanamichezo wa zamani wa Mkoa wa  Dodoma (UFAWAZA) umekipongeza Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) chini ya Mwenyekiti Aden Mohammed kwa jinsi ambavyo kimekuwa  kikiendesha na kusimamia kwa weledi soka la mkoa wa Dodoma. Pongezi hizo zimetolewa leo Machi 28,2026 Jijini Dodoma na Mjumbe wa Ufawaza,Samson Mkotya wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa DOREFA. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu kutoka Wilaya za Mkoa wa Dodoma pamoja na Vyama shiriki. Mkotya ambaye kitaaluma ni Mwalimu na Mwanasheria amesema DOREFA  imefanya mambo makubwa katika soka la Mkoa huo ikiwemo kuhakikisha soka linachezwa kuanzia katika ngazi za madaraja ya chini. "Kipekee naomba nikupongeze Mwenyekiti wetu (Aden Mohammed) tunajivunia wewe.Mkutano huu ni uthibitisho tosha mnatembea na Matukio  kwa kuhakikisha Mikutano ya kikatiba inafanyika hakika mnalitendea haki soka la Dodoma,"amesema Mkotya.

MKUTANO MKUU DOREFA WAPITISHA MPANGO KAZI KWA MWAKA 2026 - 2027

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) wamepitisha  Mpango kazi wa mwaka 2025-2026 wa Chama cha Soka Mkoani Dodoma. Awali kabla ya kuupitisha Mpango kazi huo,wajumbe hao walisomewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma CPA,Edwin Michael na kisha kwa kauli moja kuupitisha katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama hicho uliofanyika leo Machi 28,2026 Jijini Dodoma. Moja ya malengo ni kuhakikisha kunakuwa na ligi imara na yenye ushindani kwa vijana,kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake pamoja na kuendeleza ushirikiano na wadau wa Soka. "Mpango kazi huu,wa mwaka 2026-2027 unaweka msingi imara wa Maendeleo ya mpira wa miguu Mkoa wa Dodoma Kwa kushirikiana na wadau wote wa michezo na kuhakikisha Mkoa unakuwa na ushindani wa Kitaifa na Kimataifa,"amesema CPA Michael.

ADEN AAHIDI MAKUBWA DODOMA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) Aden Mohammed ameahidi makubwa zaidi kwa soka la Mkoa wa Dodoma ikiwemo kuweka mazingira rafiki kwa klabu zinazoutumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wa nyumbani. Aden ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mjumbe wa Kanda namba 4 inayojumisha Mikoa ya Singida,Dodoma,Shinyanga na Simiyu amesema  wanafurahi  kwa jinsi ambayo Mkoa wa Dodoma umekuwa na timu nyingi za Ligi Kuu,Dodoma Jiji,Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons. Amesema Dorefa itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili klabu hizo ziendelee kuutumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wa nyumbani kwa kuhakikisha zinafanya vizuri. "Niwaahidi wana Dodoma, Dorefa itaendelea kuhakikisha soka linachezwa kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu lengo vipaji vizidi kuonekana,"amesema Aden.

BABA AMICHINJA MTOTO WAKE MCHANGA

Picha
  Na Allan Kitwe, Igunga MWANAUME mmoja mkazi wa Kijiji cha Imalanguzu, Kata ya Mwamakona, Tarafa ya Igurubi, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora amemchinja mtoto wake mchanga aliyekuwa na umri wa miezi miwili na kumjeruhi vibaya mke wake. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa , Richard Abwao ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 25 mwaka huu majira ya saa 3 usiku huko katika Kitongoji cha Ibindo, kijiji cha Imalanguzu. Amebainisha kuwa mwanaume aitwaye Bunzali Jidola (30) Msukuma, mkulima, mkazi wa Imalanguzu alimchinja kwa kutumia kitu chenye ncha kali mtoto wake aitwaye Dorcas Bunzali aliyekuwa na umri wa miezi miwili. Ameongeza kuwa baada ya mauaji hayo alimjeruhi pia mke wake aitwaye Jeni Ndaki (24) Msukuma, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Ibutamisuzi kwa kutumia kifaa hicho chenye ncha kali na kisha kutokomea kusiko julikana. Amesema majeruhi huyo aliokolewa na wasamaria wema na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga iliyoko Wilayani humo ...

WAKULIMA TABORA WANUFAIKA NA MNADA WA KWANZA WA KOROSHO

Picha
  Na Lubango Mleka, Tabora.  WAKULIMA wa zao la korosho mkoani Tabora wameanza kunufaika na fursa ya soko baada ya kuanza kwa mnada wa kwanza wa zao hilo, ambapo zaidi ya kilo elfu kumi na tatu zimeuzwa katika siku ya ufunguzi. Mafanikio hayo yameelezwa kuwa ni ishara ya kukua kwa zao la korosho mkoani humo, huku matarajio ya awali yakiwa ni kuuza kilo elfu kumi pekee. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Shabani Katalambula, amesema mwitikio wa wakulima ni mkubwa na unaonyesha wazi kuwa zao hilo linaweza kuwa tegemeo jipya la kiuchumi kwa wakazi wa Tabora. Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa kampuni ya Mateak Holdings Ltd, Violet Mordichai, amesema wamejikita katika kuwajengea uwezo wakulima kupitia elimu ya kilimo bora cha korosho, akisisitiza matumizi ya pembejeo ili kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao. Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora , Bi Upendo Wella, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, amewataka wakulima kujiunga na vyama vya ushirika ili kuwa na nguvu ya pamo...

VIJANA ZAIDI YA 60 WALIOHITIMU FDC NZEGA WAPATA AJIRA

Picha
  Na Allan Kitwe, Nzega.  TAASISI, Mashirika ya Umma na makampuni binafsi yamepongezwa kwa kutoa fursa za ajira kwa vijana wa kike na kiume wanaohitimu mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali kwenye Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) . Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Nzega (Nzega FDC) Nichodemus Shirima alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliomtembelea Ofisini kwake jana ili kujionea maendeleo ya chuo hicho. Ameshukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuvifanyia maboresho makubwa vyuo vyote vya maendeleo ya wananchi nchini na kuvipatia vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia hali ambayo imechochea vyuo hivyo kutoa elimu bora. ‘Zaidi ya vijana sitini (60) waliohitimu fani mbalimbali katika chuo chetu hapa Nzega wamepata ajira rasmi katika taasisi mbalimbali za umma na makampuni ya watu binafsi na wengine wamejiajiri na wanapata kipato cha uhakika’, ameeleza. Shirima amefafanua vijana walioajiriwa kuwa ni wa fani za ufundi bomba (zaidi...