RUWASA KIGOMA WAMWAGA PONGEZI KWA RAIS SAMIA
Na Allan Kitwe, Kigoma. WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoani Kigoma wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 79 za miradi ya maji. Pongezi hizo zimetolewa na Meneja wa Wakala huo Mkoani hapa Mhandisi Mathius Mwenda alipokuwa akiongea kwenye mahojiano maalumu na waandishi wa habari Ofisini kwake. Amesema kuwa RUWASA Kigoma ina kila sababu ya kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kufanikisha utekelezaji miradi mbalimbali ya maji katika Wilaya zote 7 za Mkoa huo hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa kero ya maji. Mhandisi Mwenda amebainisha kuwa kuanzia Machi 2021 hadi Februari 2026, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alitenga zaidi ya shilingi bilioni 79 kwa ajili ya kutekeleza miradi 113 ya maji katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo. Amedokeza kuwa kati ya kiasi hicho cha fedha, serikali ilitoa jumla ya shilingi bilioni 55.9 na wadau wakaiunga mkono kwa kutoa kiasi cha shiling...