Machapisho

DAKTARI HATIANI KUUZA SARUJI NA MATOFALI ZAHANATI SUKURO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro.  MGANGA mfawidhi wa zahanati ya kijiji cha Sukuro kata ya Komolo wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Dk Daud Ndagala ametiwa hatiani kwa ubadhirifu wa mifuko ya saruji na matofali ya kukarabati zahanati hiyo. Mahakama ya wilaya ya Simanjiro imemtia hatiani Dk Ndagala kupitia shauri la jinai namba 4344/2026 kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi. Hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro Charles Uisso amesoma hukumu hiyo Machi 26,2026 na mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kituo maalum cha Mirerani Gervas Sarakikiya. Hakimu Uisso ameieleza mahakama hiyo kuwa Dk Ndagala ametiwa hatiani kwa kufuja Sh1 milioni za mauzo ya mifuko 57 ya saruji ya kukarabati zahanati hiyo. Amesema pia, Dk Ndagala alichepusha tofali 220 zilizoandaliwa kwa ajili ya ukarabati huo kisha akaziuza Sh605,000 kwa mtu binafsi. Amesema mshtakiwa huyo amefanya makosa hayo akitumia nafasi yake ya mganga mfawidhi wa zahanati ya ...

MAMBO YALIYOJIFICHA KUHUSU HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA UDZUNGWA

Picha
  1. Hifadhi ina njia mbalimbali za matembezi ya miguu na jumla ya Maporomoko ya maji 6 (Sanje, Sonjo, Njokamoni, Prince Benhard, Ichonde na Mwaya). 2. Vilele vikubwa vya  Milima (Luhomero mita 2,576  na Mwanihana mita 2,500 kutoka usawa wa bahari). 3. Kitovu cha Viumbe Adimu. Udzungwa ina viumbe wengi adimu ambao huwezi kuwapata mahala popote duniani. Spishi hizo ni pamoja na jamii mbili za primata (Ngolaga wa Sanje na Mbega wekundu wa Iringa), Spishi 2 za ndege (Kware wa Milima ya Udzungwa na “Rufous-winged Sunbird), Spishi 4 adimu za mimea ambapo moja wapo ni “Vernonia luhomeroensis”, Spishi 3 za vipepeo ambazo ni pamoja na “Charaxes lucyae mwanihanae”, Spishi ya Nyoka aitwaye “Red Snouted Wolf Snake na viumbe wengine wengi. 4. Baadhi ya Spishi nyingine adimu zinapatikana katika Milima ya Tao la Mashariki (Eastern Arc Mountains) baadhi ya spishi hizo  ni pamoja na Kinyonga Mfupi (Pygmy Chameleon).  #UdzungwaNountainsNationalPark #HikingParadise #tanzaniaparks...

UFAWAZA WAIPONGEZA DOREFA KWA USIMAMIZI NA UENDESHAJI SOKA DODOMA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  UMOJA wa Wanamichezo wa zamani wa Mkoa wa  Dodoma (UFAWAZA) umekipongeza Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) chini ya Mwenyekiti Aden Mohammed kwa jinsi ambavyo kimekuwa  kikiendesha na kusimamia kwa weledi soka la mkoa wa Dodoma. Pongezi hizo zimetolewa leo Machi 28,2026 Jijini Dodoma na Mjumbe wa Ufawaza,Samson Mkotya wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa DOREFA. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu kutoka Wilaya za Mkoa wa Dodoma pamoja na Vyama shiriki. Mkotya ambaye kitaaluma ni Mwalimu na Mwanasheria amesema DOREFA  imefanya mambo makubwa katika soka la Mkoa huo ikiwemo kuhakikisha soka linachezwa kuanzia katika ngazi za madaraja ya chini. "Kipekee naomba nikupongeze Mwenyekiti wetu (Aden Mohammed) tunajivunia wewe.Mkutano huu ni uthibitisho tosha mnatembea na Matukio  kwa kuhakikisha Mikutano ya kikatiba inafanyika hakika mnalitendea haki soka la Dodoma,"amesema Mkotya.

MKUTANO MKUU DOREFA WAPITISHA MPANGO KAZI KWA MWAKA 2026 - 2027

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) wamepitisha  Mpango kazi wa mwaka 2025-2026 wa Chama cha Soka Mkoani Dodoma. Awali kabla ya kuupitisha Mpango kazi huo,wajumbe hao walisomewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma CPA,Edwin Michael na kisha kwa kauli moja kuupitisha katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama hicho uliofanyika leo Machi 28,2026 Jijini Dodoma. Moja ya malengo ni kuhakikisha kunakuwa na ligi imara na yenye ushindani kwa vijana,kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake pamoja na kuendeleza ushirikiano na wadau wa Soka. "Mpango kazi huu,wa mwaka 2026-2027 unaweka msingi imara wa Maendeleo ya mpira wa miguu Mkoa wa Dodoma Kwa kushirikiana na wadau wote wa michezo na kuhakikisha Mkoa unakuwa na ushindani wa Kitaifa na Kimataifa,"amesema CPA Michael.

ADEN AAHIDI MAKUBWA DODOMA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) Aden Mohammed ameahidi makubwa zaidi kwa soka la Mkoa wa Dodoma ikiwemo kuweka mazingira rafiki kwa klabu zinazoutumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wa nyumbani. Aden ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mjumbe wa Kanda namba 4 inayojumisha Mikoa ya Singida,Dodoma,Shinyanga na Simiyu amesema  wanafurahi  kwa jinsi ambayo Mkoa wa Dodoma umekuwa na timu nyingi za Ligi Kuu,Dodoma Jiji,Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons. Amesema Dorefa itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili klabu hizo ziendelee kuutumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wa nyumbani kwa kuhakikisha zinafanya vizuri. "Niwaahidi wana Dodoma, Dorefa itaendelea kuhakikisha soka linachezwa kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu lengo vipaji vizidi kuonekana,"amesema Aden.

BABA AMICHINJA MTOTO WAKE MCHANGA

Picha
  Na Allan Kitwe, Igunga MWANAUME mmoja mkazi wa Kijiji cha Imalanguzu, Kata ya Mwamakona, Tarafa ya Igurubi, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora amemchinja mtoto wake mchanga aliyekuwa na umri wa miezi miwili na kumjeruhi vibaya mke wake. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa , Richard Abwao ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 25 mwaka huu majira ya saa 3 usiku huko katika Kitongoji cha Ibindo, kijiji cha Imalanguzu. Amebainisha kuwa mwanaume aitwaye Bunzali Jidola (30) Msukuma, mkulima, mkazi wa Imalanguzu alimchinja kwa kutumia kitu chenye ncha kali mtoto wake aitwaye Dorcas Bunzali aliyekuwa na umri wa miezi miwili. Ameongeza kuwa baada ya mauaji hayo alimjeruhi pia mke wake aitwaye Jeni Ndaki (24) Msukuma, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Ibutamisuzi kwa kutumia kifaa hicho chenye ncha kali na kisha kutokomea kusiko julikana. Amesema majeruhi huyo aliokolewa na wasamaria wema na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga iliyoko Wilayani humo ...

WAKULIMA TABORA WANUFAIKA NA MNADA WA KWANZA WA KOROSHO

Picha
  Na Lubango Mleka, Tabora.  WAKULIMA wa zao la korosho mkoani Tabora wameanza kunufaika na fursa ya soko baada ya kuanza kwa mnada wa kwanza wa zao hilo, ambapo zaidi ya kilo elfu kumi na tatu zimeuzwa katika siku ya ufunguzi. Mafanikio hayo yameelezwa kuwa ni ishara ya kukua kwa zao la korosho mkoani humo, huku matarajio ya awali yakiwa ni kuuza kilo elfu kumi pekee. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Shabani Katalambula, amesema mwitikio wa wakulima ni mkubwa na unaonyesha wazi kuwa zao hilo linaweza kuwa tegemeo jipya la kiuchumi kwa wakazi wa Tabora. Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa kampuni ya Mateak Holdings Ltd, Violet Mordichai, amesema wamejikita katika kuwajengea uwezo wakulima kupitia elimu ya kilimo bora cha korosho, akisisitiza matumizi ya pembejeo ili kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao. Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora , Bi Upendo Wella, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, amewataka wakulima kujiunga na vyama vya ushirika ili kuwa na nguvu ya pamo...

VIJANA ZAIDI YA 60 WALIOHITIMU FDC NZEGA WAPATA AJIRA

Picha
  Na Allan Kitwe, Nzega.  TAASISI, Mashirika ya Umma na makampuni binafsi yamepongezwa kwa kutoa fursa za ajira kwa vijana wa kike na kiume wanaohitimu mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali kwenye Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) . Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Nzega (Nzega FDC) Nichodemus Shirima alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliomtembelea Ofisini kwake jana ili kujionea maendeleo ya chuo hicho. Ameshukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuvifanyia maboresho makubwa vyuo vyote vya maendeleo ya wananchi nchini na kuvipatia vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia hali ambayo imechochea vyuo hivyo kutoa elimu bora. ‘Zaidi ya vijana sitini (60) waliohitimu fani mbalimbali katika chuo chetu hapa Nzega wamepata ajira rasmi katika taasisi mbalimbali za umma na makampuni ya watu binafsi na wengine wamejiajiri na wanapata kipato cha uhakika’, ameeleza. Shirima amefafanua vijana walioajiriwa kuwa ni wa fani za ufundi bomba (zaidi...

MMOJA AFARIKI, WAWILI WAJERUHIWA WAKIBISHANIA SIMBA NA YANGA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MTU mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kutokea ugomvi uliozuka kutokana na ushabiki wa mpira kati ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza. Kwa mujibu taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa amesema tayari wameanzisha msako wa kumtafuta kijana mmoja (jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za kumuua Abel Mganga Mazuri (25) mkazi wa Nyamahengo, na kuwajeruhi watu wawili kufuatia ugomvi uliotokana na ushabiki wa mpira. Taarifa hiyo imesema tukio hilo limetokea Machi 24, 2026 majira ya saa 5:30 usiku katika kitongoji cha Nyamahengo, kijiji na kata ya Sumve, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. "Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeanza msako wa kumtafuta kijana mmoja (jina limehifadhiwa kwa sasa) kwa tuhuma za mauaji ya Abel Mganga Mazuri, miaka25, mkazi wa Nyamahengo aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani kisha kuwajeruhi watu wawili kwa kutumia kitu c...

FDC URAMBO WAJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA

Picha
  Na Allan Kitwe, Urambo.  CHUO Cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Urambo kimeishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu na kukipatia vifaa vya mafunzo ambavyo vimekiongezea mapato. Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Chuo hicho Elias Niima alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake ambapo alieleza kufurahishwa na uamuzi wa serikali ya Awamu ya Sita kukifanyia maboresho makubwa chuo hicho.   Amesema kuwa kipindi cha miaka 4 ya Uongozi wa Rais Samia na siku 100 za awamu yake ya pili tangu aingie madarakani, chuo kimepata mafanikio makubwa ikiwemo kuzalisha samani za taasisi mbalimbali na kuingiza mapato. Ametaja baadhi ya samani zilizotengenezwa kuwa ni madawati, viti na meza zaidi ya 7,000 kwa shule za msingi na sekondari za halmashauri za Wilaya ya Urambo na 2,500 za halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. ‘Miradi hii imetekelezwa na Chuo kwa kutumia nguvu kazi ya wanafunzi na walimu wao, ikiwa ni sehe...

TAKUKURU, TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA YASAINI MIKATABA YA KUDHIBITI RUSHWA.

Picha
  Na Hamida Ramadhan,  Dodoma.  TAASISI  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika zimesaini makubaliano ya ushirikiano yatakayolenga kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa katika vyama vya ushirika nchini.  Hatua hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji, uwazi na kurejesha imani ya wanachama wa ushirika. Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Msajili na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, alisema sekta ya ushirika imekuwa ikikabiliwa na changamoto za usimamizi wa rasilimali, ambazo kwa kiasi kikubwa zimechangiwa na vitendo vya rushwa. Alieleza kuwa wanachama wengi wamekuwa wakiweka fedha, mazao na rasilimali zao katika vyama vya ushirika kwa matarajio ya kunufaika, lakini vitendo vya rushwa vimekuwa vikikwamisha malengo hayo na kupunguza imani yao. “Ushirikiano huu unalenga kukomesha vitendo vya rushwa na kurejesha matumaini ya wanachama tumejipanga kuhakik...