Machapisho

WAZIRI KIKWETE AAHIDI USHIRIKIANO KWA WATUMISHI WA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI

Picha
  Na. Mwandishi Wetu-Dar es Salaam WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameipongeza Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa kuongoza na kusimamia Ndege za Serikali kwa weledi na  ufanisi mkubwa. Waziri Kikwete amesema hayo Desemba 12, 2025 jijini Dar es salaam wakati alipotembelea ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa lengo la kujitambulisha. “Ninaipongeza Bodi kwa kuendelea kuwa washauri wazuri na kufanya uendelevu wa Wakala, binafsi ninaridhika na utendaji kazi wake. Pia Nitumie fursa hii kuwapongeza watumishi wote kwa ustadi wenu mkubwa wa kusimamia Ndege za Serikali, mimi na Naibu Waziri wa ofisi yangu Mhe. Regina Qwaray tunawahakikishia ushirikiano wa dhati wakati wote wa uongozi wetu” alisema Mhe. Kikwete. Aidha, Mhe. Kikwete amewapongeza kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ambao unaonekana kuridhisha viongozi wanawahudumia. Hivyo, ametoa rai pia kwa watu...

HALMASHAURI YA MONDULI YATUA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR KUJIFUNZA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. TIMU ya wataalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoani Arusha ikiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Happiness Laizer imefika katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa lengo kujifunza jinsi ya ukusanyaji wa mapato. Timu hiyo imepokelewa na mwenyeji wao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji hilo ndugu Elihuruma Mabelya ambapo katika mazungumzo yake aliwaeleza wataalamu hao kuwa ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam unachangiwa na ushirikiano wa watumishi katika kanda maalum za ukusanyaji mapato. Amesema uanzishwaji wa kanda hizo, umewezesha kuwasogezea wananchi huduma mbalimbali katika maeneo yao hali iliyochangia kuwapunguzia umbali wa kufuata huduma zikiwemo vibali mbalimbali, leseni n.k makao makuu ya Halmashauri.

SOMO LA LEO KUTOKA RSA TANZANIA

Picha
KWAmujibu wa kifungu cha 5(1)(e) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na Kanuni za LATRA za Usajili na Uthibitishaji Madereva na Wahudumu wa Mabasi (THE LAND TRANSPORT REGULATORY AUTHORITY (CERTIFICATION OF COMMERCIAL VEHICLE DRIVERS AND REGISTRATION OF CREW) REGULATIONS)) 2020, Dereva aliyesajiliwa na Kuthibitishwa na LATRA ana wajibu ufuatao kama sehemu ya masharti ya Kuthibitishwa kwake:  1. Kuzingatia mwendo kikomo (speed limits) uliowekwa barabarani kwa mujibu wa sheria; 2. Kutoendesha gari huku akiwa amelewa pombe au madawa ya kulevya; 3. Kuheshimu amri halali ya askari polisi au maafisa wa LATRA; 4. Kuendesha gari akiwa na leseni hai na cheti cha uthibitishwaji Kwa dereva anayeendesha gari la abiria, anatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo ya ziada, kwa mujibu wa kanuni ya 10(2) ya kanuni tajwa hapo juu:  1. Kutopakia abiria Zaidi ya uwezo wa gari kama ulivyoandikwa kwenye cheti cha usajili wa/au leseni ya, gari; 2. Kuhakikisha milango imefungwa kab...

WAZIRI MKUU AKAGUA UKARABATI WA SOKO LA MAJENGO NA KUELEKEZA UKAMILIKE

Picha
Na Lubango Mleka, Dodoma WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ametembelea Soko la Majengo jijini Dodoma na kukagua maendeleo ya ukarabati wa soko hilo, ambapo amemuelekeza mkandarasi Kampuni ya Azhar Construction kukamilisha ukarabati huo ifikapo Mwezi Februari 2026 ili wafanyabiashara waanze kulitumia. Katika kuhakikisha maelekezo yake yanatekelezwa, Dkt. Mwigulu amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Frederick Sagamiko kufanya makubaliano ya kimaandishi na mkandarasi huyo kuwa, hakutakuwa na nyongeza ya muda wa ukarabati wa soko hilo ifikapo Mwezi Februari, 2026. “Serikali inataka ukarabati wa Soko ukamilike kwa wakati ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa Jiji la Dodoma, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya kuendelea kukuza uchumi wa wafanyabiashara,” Dkt. Nchemba amesisitiza. Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akimkaribisha Mhe. Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa ukarabati wa ...

GRUMETI FUND YAWEZESHA SAFARI KWA VIJANA WAWILI KUJIFUNZA NAMNA BORA YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NCHINI TAIWAN

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Serengeti. SHIRIKA la Grumeti Fund kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii, kituo cha Mazingira, limefadhili safari ya vijana wawili kutoka katika Shule za Sekondari Issenye na Natta za Wilayani Serengeti kwenda nchini Taiwan kwa ajili ya programu maalum ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora za utunzaji na uhifadhi wa mazingira.  Msimamizi wa Kituo cha Mazingira Bw. Laurian Kahatano amebainisha kuwa, Flora Nyaboko Gesimba, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Natta na Mkazi wa Kijiji cha Maburi pamoja na Cosmas Godfrey Kitena, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Issenye na Mkazi wa Kijiji cha Singisi wamepata ufadhili wa safari hiyo baada ya kuibuka washindi katika shindano la uandishi wa i insha (Essay) lililohusisha wanafunzi 32 kutoka katika shule 16 zilizopo kwenye program ya Elimu ya Mazingira inayoendeshwa kwenye kituo chetu cha Mazingira (EEC). "Hivi karibu tuliendesha mdahalo wa utunzi wa insha, katika shule zote 16 ambapo wanafunzi walipewa ...

WANAWAKE NKINGA HOSPITALI WAZINDUA KIKUNDI CHA KUSAIDIANA

Picha
Na Lubango Mleka, Nkinga - Igunga. WANAWAKE watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga jana Disemba 11, 2025 wamezindua rasmi kikundi chenye lengo la kusaidiana katika changamoto mbalimbali za kimaisha. Kikundi hicho kilichopewa jina la Nkinga Super Women Group kimezinduliwa katika Kikao cha kwanza cha Kufunga Mwaka, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ndg.Victor Ntundwe alikuwa ndiye mgeni rasmi. "Ninawapongeza kwa kuunganisha nguvu ya pamoja katika kukabiliana na changamoto zenu, Siku zote Umoja ni nguvu, Uongozi wa hospitali unawathamini sana kwa jinsi mnavyoongoza wafanyakazi wengine kwa nidhamu, weledi na kuwa vinara wa huduma kwa mteja" amesema Mkurugenzi Ntundwe katika hotuba yake Bi.Epifania Nyaki ni mwenyekiti wa Umoja huo amesema, kuanzishwa kwa Umoja huo ni matokeo ya mawazo katika sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani Machi, 2024 baada ya kushikwa mkono na Mkurugenzi wa Hospitali, na ndipo January 2025 kikundi hicho kikaanza rasmi. Ameongeza, kwasasa kikundi hich...

TANZIA

Picha
  SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. MUSSA AZZAN ZUNGU (MB) ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MBUNGE WA PERAMIHO MHE. JENISTA JOAKIM MHAGAMA KILICHOTOKEA LEO 11,DESEMBA,2025 JIJINI DODOMA.

AMNESTY INTERNATIONAL YALISHUTUMU KUNDI LA HAMAS

Picha
SHIRIKA la Amnesty International limeishtumu Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina kwa mara ya kwanza kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwemo mauwaji, wakati na baada ya shambulio la Oktoba 7, 2023 lililochochea vita vya Gaza. #HamasIsISIS ##palestine #AmnestyInternational

UJUMBE WA LEO KUTOKA RSA TANZANIA

Picha
   NDANI ya Jiji la Dar es Salaam au kwengineko ukiendesha kwa mwendo wa wastani wa kati ya 50-60Kph kwenye Zebra yoyote utaweza kusimama na kuwapisha wavukaji wavuke, ila spidi ikizidi hapo sio rahisi kusimama hasa mwenda kwa miguu anapotokea ghafla.  Hata hivyo, Jizoeshe Kusimama kwenye kila zebra kupisha watu wavuke, maana hata wewe ni mwenda kwa miguu ukitoka kwenye usukani.  Usiposimama kuwapisha, hawatakuwa na mahala pengine salama pa kuvuka zaidi ya kuhatarisha maisha yao.  Hivyo jambo la kwanza ondoa ile kasumba au mtazamo kuwa *Aagh wasumbufu hawa*, kwakuwa hata wao hao unaowaona kero wana haki ya kutumia barabara. Ni tofauti ya kipato tu au mazingira ya wakati huo ndio yamewafanya kwenda kwa miguu.  Na jinsi miji inavyozidi kukua ndivyo idadi ya watu inavyoongezeka huku kukiwa na miundo mbinu michache sana ya waenda kwa miguu, tegemea idadi kubwa ya waenda kwa miguu kila kwenye zebra. Hivyo kuwa mwenda kwa miguu sio dhambi.  Hii ndio sababu k...

AMUUA MWANAYE KWA KIPIGO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mbeya. MWANAMKE Mmoja  aitwaye ,Marry Timotheo mkazi wa kijiji cha Garijembe kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga na kitu kizito kichwani mtoto wake, Scola Mwaba(10)kwa madai ya kuzidi utukutu kisha mwili wake kutupa shamba lilo karibu na nyumbani anakoishi . Akizungumzia tukio hilo Desemba 10,2025 Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema marehemu Scola alikuwa Mwanafunzi wa Darasa la Nne shule ya Msingi Ngonde wilaya ya Mbeya.  Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Desemba 9,2025 ,majira ya saa 6.30 mchana katika Kijiji cha Garijembe ,Kata na Tarafa ya Tembela  Wilaya ya Mbeya. "Mama wa marehemu alimshambulia kwa kitu kizito kichwani  mtoto wake kwa madai ya kuzidi utukutu kisha mwili wake kutupa jirani na shamba la nyumba anakoishi "amesema Kamanda Kuzaga.  Aidha Kuzaga ameeleza kuwa pia licha ya  kumshikilia mama wa marehemu ,pia  jirani yake ,Sharifa Nz...

NAIBU WAZIRI MAKAMBA AIPONGEZA PBPA KWA UTENDAJI KAZI MZURI

Picha
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb) ameipongeza Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa utendaji kazi mzuri katika kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha. Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya PBPA leo jijini Dar es Salaam. "Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya lakini hakikisheni mnatoa elimu kwa Watanzania kuhusu majukumu yenu na kazi zenu" amesema Mhe. Salome. Aidha, ametumia nafasi hiyo kuitaka PBPA kuwawezesha Watanzania wazawa kuingia kwenye biashara ya mafuta na kufanya kazi kwa ushirikiano. "Lazima tupate wawekezaji wa Tanzania, tuwawezeshe waingie kwenye hii biashara " amesisitiza Mhe. Salome. Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Bw. Erasto Simon amesema wakala hiyo imefanikiwa kuhakikisha kunakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha, uwepo wa takwimu sahihi za kiasi cha mafuta pamoja na kuiwezesha Serikali kupanga ukusanyaji wa mapato. ...

KALEYA MOLLEL ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA SIMANJIRO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro DIWANI wa Kata ya Msitu wa Tembo, Kaleya Melita Mollel amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, kwa kura zote 24 za Madiwani waliohudhuria kikao. Mwakilishi wa Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro, Edosi Evaristi Ndikwiki amesema Mollel ambaye ni Diwani wa Kata ya Msitu wa Tembo, amepata kura zote 24 zilizopigwa  Ndikwiki pia amesema, madiwani hao wamemchagua Diwani viti maalum wa Tarafa ya Terrat, Mwanjaa Jacob kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kura zote 24 za ndiyo. Amesema katika uchaguzi huo uliofanyika  mji mdogo wa Orkesumet ulihusisha madiwani wote wanaotokana na CCM wa kata zote 18 na viti maalumu sita. Ndikwiki amewaasa madiwani hao kutoa ushirikiano kwa wataalam wa halmashauri hiyo kwani wameshaapa kutumikia nafasi zao. "Tuzingatie mahusiano mazuri na watumishi, tuwape ushirikiano na tuwe watatuzi wa migogoro tusiibue migogoro ambayo itaturudisha nyu...

WANANCHI BABATI WAIPA KONGOLE REA

Picha
Mitungi ya gesi 3,255 kusambazwa  na kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Mitungi mmoja kuuzwa kwa bei ya ruzuku TZS 17,500. Na Mwandishi Wetu, Babati. Kongole hizo zimetolewa leo, tarehe 04 Disemba, 2025 na wananchi wa kata ya Ayalagaya Wilaya ya Babati mkoani manyara wakati wa usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku katani hapo. Uuzaji wa majiko hayo umeongozwa na  diwani wa kata ya Ayalagaya Mheshimiwa Sabil John , mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Babati, mtendaji kata ya Ayalagaya , Afisa kutoka REA na mwakilishi wa kampuni Manjis Logistics Limited.  "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia  katika kutunza mazingira na afya za wananchi" amesema Mhe. Sabil. Mhe. Sabil amesema, Lengo la mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni kuendeleza juhudi za utunzaji wa mazingira na Afya za wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu  na hamasa ya ...