Machapisho

WANAFUNZI ZAIDI YA 3000 WANYWA MAZIWA KUBORESHA AFYA GEITA

Picha
  Ma Mwandishi Wetu, Geita. WANAFUNZI wapatao 3,385 wa Shule za Msingi na Sekondari mkoa wa Geita wamekunywa maziwa kwa ajili ya ustawi wa Afya Bora na Lishe. Akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni yaliyofanyika Septemba 24, 2025 katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani hapo, Mwakilishi wa Msajili Bodi ya Maziwa Tanzania, Bi. Deorinidei Mng’ong’o alisema maziwa yaliyotolewa ni Pakti 3964 ambayo ni sawa na lita 1004.6. Mng’ong’o alisema kabla ya Siku ya kilele kumekuwepo na Matukio kadhaa yaliyokuwa yanaendelea kama vile kutembelea wanafunzi wenye uhitaji maalumu ambapo zaidi ya wanafunzi 3,385 walinufaika kwakupata Maziwa ili kuendelea kuboresha Afya zao. Alisema idadi ya lita za maziwa zilizotolewa kuanzia Septemba 22 hadi Septemba 24 mwaka huu ni lita 1004.6. “Maziwa ni mlo kamili hivyo natoa rai kwa Wazazi, Walezi na Walimu kuhakikisha watoto wetu wanapata maziwa kwa lishe bora, Afya nzuri na ukakamavu wa akili”alisema. A...

TAARIFA KWA UMMA

Picha
Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF @taifastars_ @caf_online @ligikuu @bonwambura70 @ligikuu

KATIBU MKUU WA MADINI ATEMBELEA BANDA LA GST KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Geita. KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, ametembelea Banda la GST katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita. Katika ziara hiyo, Mhandisi Samamba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo. Aidha Viongozi wengine waliotembelea banda la GST ni pamoja na Dkt. Mussa Budeba Mtendaji Mkuu wa GST,  Mwenyekiti wa Tume ya Madini Dkt. Janet Lekashingo, pamoja na Makamishna wa Tume ya Madini Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi.  Kupitia maonesho hayo GST Imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Madini kuhusu teknolojia  na mashine mbalimbali zinazotumika kwenye utafutaji na uchenjuaji wa madini.

MELI KUBWA MPYA YA KISASA YAWASILI BANDARI YA DAR ES SALAAM

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.  MELI ya Grande Shanghai kutoka nchini China imetia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam usiku wa tarehe 20 Septemba, 2025. Meli hiyo maalum kwa ajili ya kubeba magari, ni mpya kabisa ambayo imetengenezwa mwaka 2025 inatumia nguvu ya umeme jua (solar power) ambayo ni teknolojia rafiki kwa mazingira badala ya kutumia mafuta katika uendeshaji wake. Meli hiyo ya ghorofa 14 na urefu wa mita 220 ina uwezo wa kubeba magari 9,000 kwa  wakati mmoja. Kwa sasa meli hiyo inaendelea na ushushaji wa magari 1624 katika Bandari ya Dar es Salaam. Wakizungumza wakati wa hafla fupi ya upokeaji wa meli hiyo, kwa niaba ya menejimenti ya meli hiyo, Bw. Girolamo Carignani amesema: “huu ni mwanzo kwa meli zetu kufika katika Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania." Amesema kuwa wataendelea kufanya safari za kuja nchini Tanzania ili kuboresha biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine, na kuongeza kuwa hivi karibuni itaanza safari za kwenda Japan kutokea Ch...

TAARIFA KWA UMMA

Picha
 

FAHAMU KUHUSU GAZETI LA SERIKALI

Picha
 

WAASI WA M23 WAANZA KUTOZA ADA KWA SHULE MJI WA GOMA.

Picha
  SHULE ambazo hapo awali zilikuwa zinatoa elimu bila malipo katika mji wa Goma ,nchini DRC sasa zimeanza kutoza ada chini ya udhibiti wa waasi wa M23, huku walimu wakikosa mishahara kutoka serikali kuu , jambo linalozua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wazazi na walimu kuhusu upatikanaji wa elimu, wakati huu juhudi za upatanishi zinazoongozwa na Qatar zikilenga kushughulikia mzozo mpana wa eneo hilo. #M23 #drceducation #goma #drcgoma #Elimu

TBS YAONDOA TANI 42 ZA BIDHAA ZA CHAKULA ZA WATOTO ZENYE MIDOLI NDANI YAKE MAARUFU KWA JINA LA CHAMA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.  SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeondoa sokoni tani 42 za bidhaa za chakula za watoto maarufu chama zenye ‘mido li’ ndani yake.  Pia, limesema baada ya kufanya uchunguzi na kubaini uwepo wa viwanda vinavyozalisha bidhaa hizo, ilipiga marufuku na kusitisha uzalishaji na uingizwaji wa bidhaa hizo sokoni.  Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria wa TBS, Kandida Shirima alitoa ufafanuzi huo wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari uliofanyika jana kuelezea mafanikio ya TBS katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.  Aidha, shirika lilibaini uwepo wa baadhi ya wazalishaji wanaofunga vyakula na vitu vingine kama midoli hasa kwenye bidhaa za chakula za watoto kwa lengo la kuvutia watumiaji.  Amesema kuwa, baadaye walichukua hatua ya kutoa taarifa kwa umma na kuvifikia vi wanda vinavyozalisha bidhaa hizo na kusitisha uzalishaji wake.  “Tumefanya ukaguzi kupitia ofisi zetu za kanda nchi nzima na tum...

TANZANIA YAANDAA WATAALUMU WA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Austria  TANZANIA imeanza kuandaa wataalamu wa Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kupitia vyuo vya ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujenga uwezo wa kitaifa na kupunguza utegemezi wa wataalamu kutoka nje. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema hayo hivi karibuni jijini Vienna, Austria wakati wa kikao maalum na Mkurugenzi wa Divisheni ya Afrika wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), Dkt. Gashaw Gebeyehu Wolde, kando ya Mkutano Mkuu wa 69 wa IAEA. Katika mazungumzo yake na Theresa Wutz, Afisa Mkuu Muidhinishaji wa Miradi wa kampuni ya eee Austria, Prof. Nombo alipongeza hatua ya Austria kupitia UniCredit – Bank of Austria kuendelea kufadhili Mradi wa Elimu Kidigitali Zanzibari, akieleza kuwa msaada huo utafungua fursa za kupanua matumizi ya TEHAMA hadi shule na vyuo vya Tanzania Bara. Kukamilika kwa awamu za mradi huo kutaiwezesha Tanzania kuwa na mifumo madhubuti ya kidigitali, miundombinu imara na rasilima...

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA AALCO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Kampala - Uganda.  TANZANIA ni mwanachama wa AALCO, imeshiriki katika Mkutano wa 63 uliofanyika Kampala, Uganda, ambapo ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Bi. Bibiana Kileo, na TAKUKURU ikiwakilishwa na Mchunguzi Kiongozi Msaidizi Debora Elisha Mlowe kutoka Kurugenzi ya Huduma za Sheria.  Ushiriki huu unaonesha nafasi muhimu ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa na urejeshaji wa mali zinazopatikana kutokana na vitendo vya rushwa. Katika mkutano huo wa siku tano, Tanzania imesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na makosa ya kimataifa yanayovuka mipaka, pia imeunga mkono juhudi za kuimarisha nyanja za urejeshaji wa mali na utaifishaji mali, hatua inayodhihirisha dhamira ya taifa katika kulinda rasilimali na kuimarisha uwajibikaji barani Afrika na Asia.

BAROZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA AKUTANA NA WAANDISHI ZANZIBAR.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  MHE. Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tone Tinnes, na ujumbe wake wamekutana na waandishi wa habari na content creators ili kusikia simulizi za mafanikio yao kupitia program ya SWIL. Kupitia mafunzo ya wanawake na uongozi, waandishi wamekuwa daraja muhimu la kusambaza habari, kuibua mijadala na kuhamasisha jamii kuhusu usawa wa kijinsia.

MTANDAOO WA MSHIKAMANO WA KIMATAIFA UMEANDAA SALUNI YA KITAMADUNI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA MSHIKAMANO WA KUSINI MWA DUNIA.

Picha
  *"Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa" huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Kusini mwa Dunia* Na Mwandishi Wetu, Egypt  KATIKA  kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Kusini, Mpango wa Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa unaosimamiwa na Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa umeanda saluni ya kitamaduni.  Saluni hiyo yenye mada: "Vyama vya Ushirika katika Kusini ya Duniani", sambamba na tamko la Umoja wa Mataifa la kutangaza mwaka 2025 kuwa mwaka wa vyama vya ushirika chini ya kauli mbiu: "Vyama vya Ushirika: Sauti ya Pamoja ya Kusini Duniani kuelekea Mustakabali Endelevu." Saluni hiyo imemkaribisha Dkt. Mohamed Abdel Hakim Ibrahim, Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Uchumi wa Kijamii na Ushirika katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na mwandishi wa kitabu cha “Vyama vya Ushirika na Maswali ya Maendeleo”, kama mzungumzaji mkuu katika Saluni hiyo.  Pia Saluni hiyo ilihudhuriwa na Mtafiti Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Mtandao wa Ms...

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU YAPOKEA TUZO.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Manyara.  HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbulu imepokea tuzo za pongezi kwenye kikao cha tathmini ya lishe ya Mkoa kilichofanyika 12/09/2025 katika ukumbi wa vikao kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Tuzo hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imeshika nafasi ya kwanza(1) kati ya Halmashauri saba Kimkoa kwenye usimamizi mzuri na upatikanaji wa bidhaa za afya.Pia Halmashauri imeingia kwenye kumi bora ya waliofanya vizuri Kitaifa kati ya Halmashauri 184 nchini. Pia Halmashauri imepokea tuzo ya mshindi wa pili(2) kimkoa kwa sababu ya utekelezaji wa mkataba wa lishe,ikiwa na asilimia 99.4. Halmashauri imepongezwa kwa kuongeza mapato katika kituo cha Afya Dongobesh kutoka Milioni 3 hadi kufikia Milioni 18 kwa Mwezi.

HIVI HAPA VIINGILIO NGAO YA JAMII 16,09,2025

Picha
  Viingilio vya mchezo wa Ngao ya Jamii 2025  Msimu 2025/2026🔥🔥🔥 @ligikuu @tratanzania @azamtvsports Kwa taarifa zaidi tembelea link 👇👇👇 https://habarikamilitv.blogspot.com/2025/09/hivi-hapa-viingilio-ngao-ya-jamii.html

MPINA AREJESHA FOMU YA URAIS ACT - WAZALENDO

Picha
Mpina akirejesha Fomu za Urais ACT-Wazalendo baada ya Uamuzi wa Mahakama

TAARIFA KWA UMMA.

Picha
LEO Septemba 13. 2025 Saa 6:00 Mchana Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo Ndugu  Luhaga Joelson Mpina, ataongea na waandishi wa Habari baada ya kurejesha fomu zake katika ofisi ya Tume jijini Dar esSalaam Mkutano utafanyika Makao Makuu ya ACT Wazalendo Magomeni Waandishi wa Habari Mnakaribishwa Kuhudhuria @ACT @Tumehuruyataifayauchaguzi @Tujitokezekupigakuraoctoba29  @Luhangampina @Zitokabwe

TAMASHA LA WIKI YA MWANCHI

Picha
HALI ILIVYO KWA SASA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA.  Fungua link hapo chini utazame live.  https://www.youtube.com/live/nUnhtCZTt1c?si=XWxxkzxjAPkhGWkI

MWELEKEO WA MVUA ZA VULI (OKTOBA-DESEMBA, 2025

Picha
 

RAIS MWINYI AZINDUA SERA YA NISHATI NA MPANGO MKUU WA UMEME ZANZIBAR 2025–2040

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati thabiti ya kisera ili kuhakikisha Zanzibar inapata nishati ya umeme wa uhakika wakati wote. Akizindua Sera ya Nishati ya Zanzibar ya 2025 pamoja na Mpango Mkuu wa Umeme wa Zanzibar wa 2025–2040, katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Golden Tulip, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dkt. Mwinyi alisema sekta ya nishati ndiyo uti wa mgongo wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Serikali ya Awamu ya Nane imelenga kujenga Zanzibar yenye uchumi shindani, kijani na jumuishi kwa kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi, nafuu na salama. Rais Dkt. Mwinyi amesema sera hiyo inalenga kupunguza gharama, kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuboresha ufanisi na kupunguza utegemezi wa kuni na makaa, hususan kwa wanawake katika shughuli za kiuchumi. Aidha, Serikali inaendeleza mikakati ya kuwekeza katika vyanzo mbadala vya nishati ikiwemo jua, upepo, ...