HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU YAPOKEA TUZO.

 



Na Mwandishi Wetu, Manyara. 

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbulu imepokea tuzo za pongezi kwenye kikao cha tathmini ya lishe ya Mkoa kilichofanyika 12/09/2025 katika ukumbi wa vikao kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Tuzo hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imeshika nafasi ya kwanza(1) kati ya Halmashauri saba Kimkoa kwenye usimamizi mzuri na upatikanaji wa bidhaa za afya.Pia Halmashauri imeingia kwenye kumi bora ya waliofanya vizuri Kitaifa kati ya Halmashauri 184 nchini.

Pia Halmashauri imepokea tuzo ya mshindi wa pili(2) kimkoa kwa sababu ya utekelezaji wa mkataba wa lishe,ikiwa na asilimia 99.4.

Halmashauri imepongezwa kwa kuongeza mapato katika kituo cha Afya Dongobesh kutoka Milioni 3 hadi kufikia Milioni 18 kwa Mwezi.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.