Machapisho

MPINA AREJESHA FOMU YA URAIS ACT - WAZALENDO

Picha
Mpina akirejesha Fomu za Urais ACT-Wazalendo baada ya Uamuzi wa Mahakama

TAARIFA KWA UMMA.

Picha
LEO Septemba 13. 2025 Saa 6:00 Mchana Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo Ndugu  Luhaga Joelson Mpina, ataongea na waandishi wa Habari baada ya kurejesha fomu zake katika ofisi ya Tume jijini Dar esSalaam Mkutano utafanyika Makao Makuu ya ACT Wazalendo Magomeni Waandishi wa Habari Mnakaribishwa Kuhudhuria @ACT @Tumehuruyataifayauchaguzi @Tujitokezekupigakuraoctoba29  @Luhangampina @Zitokabwe

TAMASHA LA WIKI YA MWANCHI

Picha
HALI ILIVYO KWA SASA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA.  Fungua link hapo chini utazame live.  https://www.youtube.com/live/nUnhtCZTt1c?si=XWxxkzxjAPkhGWkI

MWELEKEO WA MVUA ZA VULI (OKTOBA-DESEMBA, 2025

Picha
 

RAIS MWINYI AZINDUA SERA YA NISHATI NA MPANGO MKUU WA UMEME ZANZIBAR 2025–2040

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati thabiti ya kisera ili kuhakikisha Zanzibar inapata nishati ya umeme wa uhakika wakati wote. Akizindua Sera ya Nishati ya Zanzibar ya 2025 pamoja na Mpango Mkuu wa Umeme wa Zanzibar wa 2025–2040, katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Golden Tulip, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dkt. Mwinyi alisema sekta ya nishati ndiyo uti wa mgongo wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Serikali ya Awamu ya Nane imelenga kujenga Zanzibar yenye uchumi shindani, kijani na jumuishi kwa kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi, nafuu na salama. Rais Dkt. Mwinyi amesema sera hiyo inalenga kupunguza gharama, kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuboresha ufanisi na kupunguza utegemezi wa kuni na makaa, hususan kwa wanawake katika shughuli za kiuchumi. Aidha, Serikali inaendeleza mikakati ya kuwekeza katika vyanzo mbadala vya nishati ikiwemo jua, upepo, ...

WAZIRI MAVUNDE: USUSI SI KAZI YA AIBU KWA VIJANA WA KIUME

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WAZIRI wa Madini, na mgombea ubunge Jimbo la Mtumba Anthony Mavunde amesema hakuna sababu ya vijana wa kiume kubezwa au kutazamwa kwa jicho la ajabu wanapoamua kujihusisha na kazi ya ususi, kwani ni kazi halali kama nyingine yoyote. Amesema hayo jijini Dodoma katika uzinduzi wa Siku ya Wasusi, uliowakutanisha wasusi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, ambapo alisisitiza kuwa jamii haina budi kuachana na mitazamo ya kudhalilisha kazi zinazofanywa na watu kwa bidii na maarifa yao. Mavunde amesema kuwa kazi ya ususi imekuwa mkombozi kwa vijana wengi, hususan wanawake, lakini sasa pia imekuwa ikiwavutia baadhi ya vijana wa kiume, jambo linalopaswa kuungwa mkono badala ya kubezwa. Ameongeza kuwa moja ya malengo yake ni kuhakikisha ususi unaboreshwa ili kuifanya kuwa kazi ya heshima na inayotambulika rasmi, huku serikali ikijiandaa kutoa mafunzo rasmi kwa vijana kupitia vyuo vya ufundi kama VETA.  "Tayari serikali imeanza kushirikiana na VETA...

WAFANYAKAZI WA KOREA KUSINI WAZUIWA NA WAVAMIZI NCHINI MAREKANI

Picha
MAMIA ya wafanyikazi wa Korea Kusini wamezuiliwa kufuatia uvamizi wa wahamiaji wiki iliyopita nchini Marekani, na kuzua wasiwasi miongoni mwa makampuni ya Korea Kusini kuhusu uwekezaji nchini Marekani. Wafanyakazi waliozuiliwa walitarajiwa kurejea nyumbani kwa ndege ya kukodi baadaye wiki hii, shirika la habari la Yonhap lilisema Jumatatu, likimnukuu mwanadiplomasia wa Korea Kusini. Kwa ushirikiano na mashirika ya kutekeleza sheria ya serikali, serikali na mitaa, maajenti wa Idara ya Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha ya Marekani (ICE) walitekeleza hati ya utafutaji ya serikali mnamo Septemba 4 katika kampuni kwa sababu ya madai mazito ya utendakazi kinyume cha sheria na uhalifu mwingine wa shirikisho, ICE ilisema kwenye tovuti yake. Uvamizi huo wa wahamiaji ulitokea katika eneo la ujenzi wa kiwanda cha betri za magari ya umeme linaloendeshwa na ubia kati ya Hyundai Motor Group na LG Energy Solution. Waliokamatwa ni watu 475, wakiripotiwa kujumuisha takriban raia 300 wa Korea Kusini a...

MASHAMBULIZI YA NDEGE ZISIZO NA RUBANI YARIPOTIWA SUDANI

Picha
 MASHAMBULIZI ya ndege zisizo na rubani yameripotiwa mapema Jumanne karibu na mji mkuu wa Sudan, Khartoum, yakilenga miundombinu muhimu na maeneo ya kijeshi.  Kwa mujibu wa mashuhuda na maafisa wa jeshi waliozungumza na shirika la habari la AFP, mashambulizi hayo yalilenga kituo cha kusafisha mafuta cha Al-Jaili, kituo cha umeme cha Al-Markhiyat kilichoko Omdurman, na kiwanda cha silaha cha Yarmuk.  Hili linakuja miezi kadhaa baada ya jeshi kuwatimua wanamgambo wa RSF kutoka eneo hilo, na wakati serikali inayoungwa mkono na jeshi ikiendeleza juhudi za ujenzi upya katika mji wa Khartoum, ambako mapigano makali yalizua wimbi la wakimbizi tangu Aprili 2023. #sudan #sudanese #khartoumattack #Khartoum #umdurman #Yarmuk #RSF

ETHIOPIA KUZINDUA MRADI MKUBWA WA UMEME.

Picha
ETHIOPIA imejiandaa kuzindua mradi mkubwa zaidi wa umeme wa maji barani Afrika leo Jumanne, mradi ambao umeahidi kuleta mapinduzi katika sekta ya nishati ya nchi hiyo. Nchi hiyo inatarajia kuanza kuuza umeme kwa mataifa mengine lakini pia kuongeza magari ya umeme hadi zaidi ya 500,000 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.  Kwa Ethiopia, Bwawa la Grand Renaissance (GERD) ni mradi wa kitaifa wa kiwango cha kihistoria na ishara adimu ya umoja katika nchi inayokumbwa na migogoro ya ndani inayoendelea. Hata hivyo mradi huo umeibua mvutano wa kidiplomasia na majirani wa mto Nile walioko chini ya mkondo hasa Misri na Sudan.

PUTIN AMTUNUKU TUZO YA UJASIRI JENERALI GERASIMOV

Picha
  RAIS wa Urusi Vladimir Putin Jumatatu ametunukiwa Tuzo ya ujasiri kwa Jenerali wa Jeshi Valery Gerasimov, mkuu wa wafanyakazi wakuu wa vikosi vya jeshi la Urusi na kamanda mkuu wa vita vya Urusi nchini Ukraine. Gerasimov, mmoja wa watu wenye nguvu zaidi katika jeshi la Urusi na ambaye Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ilitoa waranti dhidi yake ya kukamatwa kwa madai ya uhalifu nchini Ukraine, anatajwa kuwa msanifu mkuu wa mkakati wa kisasa wa vita vya Urusi. Alitimiza umri wa miaka 70 Jumatatu. Gerasimov alipewa Tuzo ya ujasiri na mapambo ya kifahari ya serikali, "kwa ujasiri, ushujaa, na jitolea katika kutimiza wajibu wa kijeshi," kulingana na amri iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya sheria ya Urusi mwishoni mwa Jumatatu. Gerasimov anadhaniwa kushikilia mojawapo ya mikoba mitatu ya nyuklia inayoweza kutuma maagizo ya shambulio la nyuklia. Alitekeleza jukumu muhimu katika wakati Urusi ilipoitwaa Crimea kutoka kwa Ukraine mnamo 2014 na katika uungaji mkono wa kijeshi wa Uru...

WAZIRI MKUU WA NORWAY KUSALIA MADARAKANI

Picha
WAZIRI Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store atasalia madarakani kwa muhula mwingine wa miaka minne, baada ya chama chake cha Labour kuibuka mshindi katika uchaguzi wa Bunge uliofanyika siku ya Jumatatu. Chama cha Labour kimeongoza kwa kupata asilimia 28 ya kura, na kwa kushirikiana na vyama vingine vinne vya mrengo wa kushoto, kimefanikiwa kupata wingi wa kutosha wa viti bungeni kuunda serikali ya muungano. Katika hotuba yake baada ya kutangazwa kwa matokeo, Store amesema ushindi huo ni uthibitisho wa imani ya wananchi kwa sera za kijamii na kiuchumi ambazo serikali yake imekuwa ikitekeleza. #norway #LabourParty #gahrstore #winner

WAZIRI MKUU WA UFARANSA KUJIUZULU LEO.

Picha
  RAIS wa Ufaransa Emmanuel Macron leo atakubali kujiuzulu kwa waziri mkuu Francois Bayrou baada ya serikali yake kukataliwa katika kura ya imani.  Macron yuko mbioni kutafuta waziri mkuu wa saba kujaza pengo lililojitokeza kuepusha mgogoro mpya wa kisiasa Ufaransa baada ya hapo jana Bayrou kupoteza kura ya imani aliyoiitisha yeye mwenyewe.  Matokeo ya kura iliyopigwa jana katika bunge la kitaifa, yanaonesha wabunge 364 walipiga kura kusema hawana imani na serikali huku 194 pekee wakisema wana imani nayo.  Macron atakutana na Bayrou leo Jumanne "kukubali kujiuzulu kwa serikali yake. Credit :DW. 

WANANCHI WA KATEMBE, MWALONI MULEBA WAONDOKANA NA ADHA YA BARABARA

Picha
*Ni kiunganishi cha wafanyabiashara wa Rwanda, Burundi na Uganda* Na Mwandishi Wetu, Muleba.  UJENZI wa barabara ya lami ya Katembe -Mwaloni inayounganisha Barabara kuu ya kutoka nchi za Uganda, Rwanda na Burundi katika wilaya ya Muleba  Mkoani Kagera  uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 400 umeleta ahueni kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na wafanyabiashara wa samaki kutoka katika visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria kwenda ndani na nje ya Nchi. Kiongozi wa mbio za Mwenge  wa uhuru Kitaifa Ndugu Ismail  Ussi ameridhisha na viwango vya mradi huo na kuwapongeza TARURA kwa utekelezaji wa mradi wenye viwango ambao unaendeleaa kuwasaidia wananchi . Alisema kuwa Ili wanachi wapate huduma bora na nguvu ya kuzalisha wanahitaji Barabara nzuri zenye viwango na kupitia umma wa wananchi ameshukuru usimamizi wa mradi huo na namna Halmashauri ya Muleba ulivyotoa mapato ya ndani kujenga Barabara imara inayoweza  kuchochea uchumi na kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara...

WAZIRI WA HABARI ZANZIBAR ANUNUA TIKETI 100 MCHEZO WA NIGER NA TANZANIA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh: Tabia Maulid Mwita, amenunua Tiketi 100, kwa ajili ya Mashabiki, Kushuhudia Mchezo Kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Niger. #tabiamwita #r.hmwinyi #wizara_ya_habari_zanzibarz #Tanzania #Niger

TRA YAKARIBISHWA MAKANISANI KUTOA ELIMU YA KODI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro.  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kilimanjaro imealikwa kutoa elimu ya kodi kwa Wanachama wa ELCT SACCOS katika kikao cha mwaka cha taasisi hiyo.  Mafunzo hayo yamefanyika jana tarehe 06.09.2025 katika Kanisa  la KKKT ushirika wa Majengo , katika manispaa ya Moshi, Mwika na Hai  mkoani Kilimanjaro ambapo mada  zilizowasilishwa ni pamoja na Usajili wa biashara mtandaoni, Dawati maalumu la uwezeshaji biashara na uwasilishaji wa ritani za kodi na ulipaji wa kodi kwa hiari. Akiwasilisha mada, Afisa Msimamizi wa Kodi Mwandamizi, Bw. Odupoi Papaa amewasisitiza wanachama kuwasilisha ritani za kodi na kufanya ya kodi kwa wakati pamoja na kutoa na kudai risiti za kielektroniki.