MASHAMBULIZI YA NDEGE ZISIZO NA RUBANI YARIPOTIWA SUDANI
MASHAMBULIZI ya ndege zisizo na rubani yameripotiwa mapema Jumanne karibu na mji mkuu wa Sudan, Khartoum, yakilenga miundombinu muhimu na maeneo ya kijeshi.
Kwa mujibu wa mashuhuda na maafisa wa jeshi waliozungumza na shirika la habari la AFP, mashambulizi hayo yalilenga kituo cha kusafisha mafuta cha Al-Jaili, kituo cha umeme cha Al-Markhiyat kilichoko Omdurman, na kiwanda cha silaha cha Yarmuk.
Hili linakuja miezi kadhaa baada ya jeshi kuwatimua wanamgambo wa RSF kutoka eneo hilo, na wakati serikali inayoungwa mkono na jeshi ikiendeleza juhudi za ujenzi upya katika mji wa Khartoum, ambako mapigano makali yalizua wimbi la wakimbizi tangu Aprili 2023.
#sudan #sudanese #khartoumattack #Khartoum #umdurman #Yarmuk #RSF

Maoni