WAZIRI MKUU WA NORWAY KUSALIA MADARAKANI
WAZIRI Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store atasalia madarakani kwa muhula mwingine wa miaka minne, baada ya chama chake cha Labour kuibuka mshindi katika uchaguzi wa Bunge uliofanyika siku ya Jumatatu.
Chama cha Labour kimeongoza kwa kupata asilimia 28 ya kura, na kwa kushirikiana na vyama vingine vinne vya mrengo wa kushoto, kimefanikiwa kupata wingi wa kutosha wa viti bungeni kuunda serikali ya muungano.
Katika hotuba yake baada ya kutangazwa kwa matokeo, Store amesema ushindi huo ni uthibitisho wa imani ya wananchi kwa sera za kijamii na kiuchumi ambazo serikali yake imekuwa ikitekeleza.
#norway #LabourParty #gahrstore #winner

Maoni