ETHIOPIA KUZINDUA MRADI MKUBWA WA UMEME.
ETHIOPIA imejiandaa kuzindua mradi mkubwa zaidi wa umeme wa maji barani Afrika leo Jumanne, mradi ambao umeahidi kuleta mapinduzi katika sekta ya nishati ya nchi hiyo. Nchi hiyo inatarajia kuanza kuuza umeme kwa mataifa mengine lakini pia kuongeza magari ya umeme hadi zaidi ya 500,000 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Kwa Ethiopia, Bwawa la Grand Renaissance (GERD) ni mradi wa kitaifa wa kiwango cha kihistoria na ishara adimu ya umoja katika nchi inayokumbwa na migogoro ya ndani inayoendelea.
Hata hivyo mradi huo umeibua mvutano wa kidiplomasia na majirani wa mto Nile walioko chini ya mkondo hasa Misri na Sudan.

Maoni