SIKU YA NYUKI DUNIANI’ YAADHIMISHWA KITAIFA TABORA
Na Allan Kitwe, Tabora. MAADHIMISHO ya Siku ya Nyuki Duniani yanayoyohusisha utundikaji mizinga, maonesho ya bidhaa na mazao ya nyuki yameanza leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Vita Mjini Tabora na kuvuta umati mkubwa wa wananchi. Wakizungumza kwenye maadhimisho hayo wakazi wa Tabora wameeleza kufurahishwa na tukio hilo kwa kuwa linawapa fursa wageni kutembelea Mkoa huo na kuonja utamu wa asali inayozalishwa katika misitu ya Mkoa huo. Daud Elisha, mjasiriamali mkazi wa Kata ya Kanyenye, Halmashauri ya manispaa ya Tabora ameeleza kuwa zao la asali ni miongoni mwa mazao ya kujivunia yanayozalishwa katika Mkoa huo na kuuzwa kwa bei kubwa ndani na nje ya nchi. ‘Haya maadhimisho ni fursa muhimu sana kwa wana Tabora kuuza asali yao na kupanua wigo wa uzalishaji zao hilo katika Wilaya zote za Mkoa huu, hivyo kuwaneemesha zaidi kiuchumi’, amesema. Amina Madereka, mjasiriamali anayejishughulisha na utundikaji mizinga na uuzaji asali katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ame...