MATAPELI WATANO WANASWA KWA TUHUMA ZA KUIBA MILIONI 40 TABORA
Na mwandishi wetu, Tabora. Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa shilingi milioni 40 kutoka kwa mfanyabiashara Fatuma Nasoro, mkazi wa Wilaya ya Kaliua, katika tukio lililotikisa wakazi wa eneo hilo. Kwa mujibu wa taarifa za awali, watuhumiwa hao walinaswa kufuatia msako maalum ulioendeshwa kwa nyakati tofauti ndani ya mkoa huo, baada ya kubainika kuwa walikuwa wakijihusisha na vitendo vya utapeli huku wakiendelea na maisha yao ya kawaida bila wasiwasi wowote. Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha, amesema miongoni mwa waliokamatwa, wawili wanaotambulika kwa majina ya Marseli Gwasima na Fred Ricardo walitumia mbinu za udanganyifu kwa kujifanya wahudumu wa kampuni ya mawasiliano ya YAS (zamani Tigo). Ameeleza kuwa kwa kutumia ujanja huo, watuhumiwa walimshawishi mfanyabiashara huyo, anayejihusisha na biashara ya khanga na vitenge wilayani Kaliua, kuwasajili laini yake, hatua iliyowapa mwanya wa kuhamisha ...