DC MYINGA ATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI SIKONGE JUU YA UPUNGUFU WA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI.
Na Mwandishi Wetu, Sikonge-Tabora. UPUNGUFU wa madawati katika shule za msingi Wilayani Sikonge umechukua sura mpya baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mheshimiwa Thomas Myinga, kutoa agizo kali kwa viongozi wa vijiji na kata kuhakikisha wanatumia rasilimali zilizopo kumaliza changamoto hiyo kwa haraka. Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha viongozi wa serikali za vijiji, kata pamoja na walimu, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Mheshimiwa Myinga alisisitiza kuwa hakuna sababu ya wanafunzi kuendelea kukaa chini ilhali maeneo yao yana rasilimali za kutosha, ikiwemo misitu inayoweza kutumika kutengeneza madawati. Alielekeza viongozi hao kupanga na kutekeleza bajeti zao kwa kuzingatia kipaumbele cha elimu, akibainisha kuwa ushirikiano kati ya serikali, wananchi na wadau wa maendeleo ni muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Seif Salum...