Machapisho

MJIKO BANIFU KWA BEI YA RUZUKU YAWAFIKIA WANANCHI CHUNYA.

Picha
Majiko 1,555 kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Serikali kutoa ruzuku ya asilimia 85 kwa kila jiko. Na Mwandishi Wetu, Chunya - Mbeya*  KAIMU Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa halmashauri hiyo, Wakili Athumani Bamba leo Aprili 24, 2026 amezindua rasmi mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika mji mdogo wa Makongolosi, wilayani Chunya mkoani Mbeya. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mradi huo unalenga kuwapatia wananchi nishati mbadala iliyo nafuu, salama na rafiki kwa mazingira, huku ukichochea kupunguza matumizi makubwa ya kuni na mkaa ambao umeendelea kuwa chanzo cha uharibifu wa misitu. Ameeleza kuwa kupitia mpango huo wa ruzuku, wananchi wataweza kumudu kununua majiko banifu kwa gharama nafuu zaidi, jambo litakalosaidia kupunguza matumizi ya nishati zisizo rafiki pamoja na kuboresha afya za watumiaji kwa kupunguza athari za moshi majumbani. “Ni muhimu wananchi wakautumia vyem...

WATAALAMU WA AFYA, SANYANSI ONGEZENI JUHUDI MATUMIZI YA TEKNOLOJIA

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  SELIKALI  imewataka wataalamu wa afya na sayansi nchini kuongeza juhudi katika kuimarisha matumizi ya teknolojia ya vinasaba, ili kuboresha huduma za afya na kusaidia utoaji wa haki jinai kwa ufanisi zaidi. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, wakati akifungua mkutano wa kisayansi wa teknolojia ya vinasaba uliofanyika jijini Dodoma, uliowakutanisha wataalamu wapatao 400 kutoka sekta mbalimbali. Amesema teknolojia ya vinasaba imekuwa mhimili muhimu katika huduma za kisasa za afya, ikisaidia katika upandikizaji wa viungo kama figo na uroto wa mifupa, pamoja na kuboresha utambuzi wa magonjwa na utoaji wa tiba za kisasa zikiwemo tiba jeni na chanjo. Mbali na sekta ya afya, amesema teknolojia hiyo imeleta mapinduzi katika mfumo wa haki jinai kwa kuwezesha upatikanaji wa ushahidi wa kisayansi unaosaidia uchunguzi na utoaji wa haki kwa usahihi zaidi. Dkt. Samizi ameeleza kuwa serikali imeendelea kuwekeza katika kuimari...

MKENDA:URASIMISHAJI UJUZI KUINUA HADHI YA VIJANA

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema programu ya utambuzi na urasimishaji ujuzi inalenga kumpa kijana hadhi, sauti na fursa pana za ajira ndani na nje ya nchi. Amesema hayo Aprili 22, 2026 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mama Samia ya Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi, inayolenga kuwasaidia vijana wenye ujuzi walioupata nje ya mfumo rasmi kutambuliwa kitaaluma. “Ujuzi ni mali, mtaji na nguvu ya taifa, hivyo vijana wanapaswa kujitokeza ili kutathminiwa na kurasimishwa,” amesema. Ameeleza kuwa utoaji wa vyeti kupitia programu hiyo siyo tu utoaji wa nyaraka, bali ni njia ya kumpa kijana nafasi ya kushindana katika soko la ajira kwa kuaminika zaidi. Aidha, amesema serikali imepanga kusogeza huduma karibu na wananchi ili mafundi wasilazimike kusafiri umbali mrefu, huku akisisitiza kuwa mchakato huo unatekelezwa bila gharama kwa wanufaika.  Ameongeza kuwa si kila mwenye ujuzi atapewa cheti moja kwa moja, bali ...

SERIKALI YAKIRI UHABA WA WATAALAMU, MALIPO YALALAMIKIWA

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  NAIBU Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, amesema serikali inatambua changamoto ya uhaba wa wataalamu wa usingizi na ganzi nchini, akibainisha kuwa kwa sasa kuna takribani wataalamu 2,950 wanaohudumia hospitali zaidi ya 800. Amesema serikali imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na upungufu huo kwa kuongeza nafasi za mafunzo, hususan katika ngazi ya stashahada, ili kuongeza idadi ya wataalamu na kuboresha utoaji wa huduma za afya. “Lengo la serikali ni kuhakikisha tunakuwa na wataalamu wa kutosha watakaoweza kutoa huduma salama na kupunguza vifo vinavyotokana na upasuaji, hasa kwa mama na mtoto,” amesema. Hata hivyo, wataalamu wa huduma ya usingizi na ganzi wameiomba serikali kuhakikisha wanalipwa kwa wakati malipo ya saa za ziada wanazofanya, wakisema kucheleweshewa stahiki hizo kunapunguza ari ya kazi na kuhatarisha ubora wa huduma kwa wagonjwa. Akizungumza katika kongamano la nne la Chama cha Wataalamu wa Dawa za Usingizi, Ganzi na Upasuaji...

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA ALAT TAIFA

Picha
  Na Mwandishi Wetu.  MSTAHIKI Meya wa Jiji la Mwanza amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Association of Local Authorities of Tanzania (ALAT) Taifa, baada ya kujizolea jumla ya kura 273 kati ya kura 339 zilizopigwa. Katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali, jumla ya wagombea wanne walijitokeza kuwania nafasi hiyo muhimu ya uongozi wa mamlaka za serikali za mitaa nchini.  Hata hivyo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza aliibuka mshindi kwa kupata kura nyingi zaidi, akionesha imani kubwa waliyonayo wajumbe wa ALAT Taifa kwake. Ushindi huo unaashiria heshima na imani kwa uongozi wa Jiji la Mwanza katika kusimamia na kuendeleza masuala ya maendeleo ya serikali za mitaa nchini.  Aidha, ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya halmashauri mbalimbali na kuendeleza ajenda za maendeleo kwa wananchi. Kupitia nafasi hiyo mpya, Mstahiki Meya anatarajiwa kusimamia na kuratibu shughuli za ALAT Taifa, ikiwa ni pamoja na kutetea maslahi ya mamlaka...

HAWA MWAIFUNGA AAHIDI TABASAMU KWA WAKAZI MANISPAA TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  MBUNGE wa Jimbo la Tabora Mjini Hawa Subira Mwaifunga amefanya mkutano mkubwa wa hadhara Jimboni humo na kupokea kero za wananchi huku akiahidi kuwapa tabasamu kwa mazuri yatakayofanyika. Ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika uwanja wa TBC ulio karibu na Ofisi za CCM Tabora Mjini ambapo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi na wana CCM wote kwa kumchagua kuwa mbunge wao. Mwaifunga amesema kuwa kuanzia sasa ataanza utaratibu wa kupita mtaa kwa mtaa, kata kwa kata ili kupokea mawazo ya nini wananchi wanataka, kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka na wa kudumu. Amefafanua kuwa mbunge ni mtumishi wa wananchi, hivyo ana wajibu wa kutembelea, kusikiliza na kutatua kero na shida za wananchi wake kwa kuwa ndio waliompeleka bungeni. ‘Mbunge na diwani wanawajibika moja kwa moja kwa waliowachagua, kwa kuhakikisha wanajua kero zao na kuzitafutia ufumbuzi, kazi yetu ni kuwapa tabasamu wananchi na si vinginevyo,’ a...

MALIASILI NA UTALII WATATHMINI UTENDAJI WA ROBO TATU MWAKA DODOMA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WATAALAMU wa Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake wamekutana katika Kikao kazi cha Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kwa ajili ya Maandalizi ya Taarifa ya Ufuatiliaji na Utendaji Kazi wa Wizara kwa Kipindi cha Robo Tatu Mwaka (Julai, 2025 hadi Machi, 2026) katika Ukumbi wa TANAPA jijini Dodoma. Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Bure Nassibu amesema kuwa lengo la kikao hicho ni Kujadili na Kuandaa Taarifa ya Ufuatiliaji wa Utendaji Kazi wa Wizara kwa kipindi cha Robo Tatu (Julai, 2025 – Machi, 2026) kwa kuzingatia viwango vya ubora na ushahidi wa utekelezaji. Bi Bure aliongeza kuwa kikao hicho kinaongozwa na Kaulimbiu ya Kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini kwa Matokeo Endelevu ya Utekelezaji wa Sera, Mipango na Miradi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026. Aidha, Wataalamu hao watafanya mapitio ya utekelezaji wa shughuli za Wizara ikiwemo kupima hatua iliyofik...

NYANSAHO FOUNDATION YAZIDI KUHAMASISHA MAENDELEO BILLION 1.4 ZAKUSANYWA KWENYE HARAMBEE KIJIJI CHA MUSATI WILAYANI SERENGETI.

Picha
Na Jovina Massano, Serengeti.  KATIKA kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu karibu na maeneo yao Nyansaho Foundation na wadau mbalimbali  wachangia Shillingi Billioni 1.4 zitakazowezesha upatikanaji wa huduma za afya na elimu Kijiji cha Musati. Harambee hiyo imefanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Musati wilayani Serengeti mkoani Mara ambapo ilitanguliwa na uzinduzi wa kanisa la Waadventista wa Sabato- Musati Central na nyumba ya mchungaji ambavyo vyote kwa pamoja vimejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya Nyansaho  kwa kiasi cha millioni 500. Akiongoza harambee hiyo Waziri wa Ujenzi ,Mh.Abdalah Ulega(MB) ameweza kukusanya jumla ya Shillingi Billioni 1.4 zitakazowezesha kujenga Shule pamoja na Zahanati katika Kijiji hicho. Katika harambee hiyo Waziri Ulega na rafiki zake wamechangia shillingi millioni 100 na kuongoza uchangiaji kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo (wafanyabiashara) zikiwemo taasisi za fedha, wageni waalikwa na wananchi na kuweza kufikisha kiasi hicho ...