NYANSAHO FOUNDATION YAZIDI KUHAMASISHA MAENDELEO BILLION 1.4 ZAKUSANYWA KWENYE HARAMBEE KIJIJI CHA MUSATI WILAYANI SERENGETI.
Na Jovina Massano, Serengeti.
KATIKA kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu karibu na maeneo yao Nyansaho Foundation na wadau mbalimbali wachangia Shillingi Billioni 1.4 zitakazowezesha upatikanaji wa huduma za afya na elimu Kijiji cha Musati.
Harambee hiyo imefanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Musati wilayani Serengeti mkoani Mara ambapo ilitanguliwa na uzinduzi wa kanisa la Waadventista wa Sabato- Musati Central na nyumba ya mchungaji ambavyo vyote kwa pamoja vimejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya Nyansaho kwa kiasi cha millioni 500.
Akiongoza harambee hiyo Waziri wa Ujenzi ,Mh.Abdalah Ulega(MB) ameweza kukusanya jumla ya Shillingi Billioni 1.4 zitakazowezesha kujenga Shule pamoja na Zahanati katika Kijiji hicho.
Katika harambee hiyo Waziri Ulega na rafiki zake wamechangia shillingi millioni 100 na kuongoza uchangiaji kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo (wafanyabiashara) zikiwemo taasisi za fedha, wageni waalikwa na wananchi na kuweza kufikisha kiasi hicho Cha fedha.
Akizungumza katika harambee hiyo, Mhe. Ulega amempongeza Mhe. Dkt.Rhimo Nyansaho (MB), kwa juhudi zake za kuwaletea maendeleo watanzania wakiwemo wananchi wa Serengeti na mkoa.
“Wana Mara hongereni sana kwa kuwa na Dkt. Nyansaho, kazi anazofanya ni kubwa Watu wa Mara mnaye mtu wa kijivunia,” amesema Mhe. Ulega
Kwa Upande wake Mwenyekiti na muanzilishi wa Taasisi ya Nyansaho Dkt.Rhimo Nyansaho (MB) ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ameelezea uamuzi wa Taasisi hiyo kuwa imejikita katika kusaidia miradi ya kijamii kama vile elimu na afya pia imedhamiria kujenga shule na zahanati kwa lengo la kutoa huduma bora za afya na elimu kwa wananchi.
Ameongeza kuwa baada ya kujenga kanisa, sasa nguvu za Taasisi ya Nyansaho, inaelekezwa kujenga zahanati na shule ambavyo vyote kwa pamoja vitatoa huduma kwa watu wote bila kujali dini zao.
“Tunawashukuru sana kwa michango hii, lengo letu ni kujenga shule kuanzia nursery (chekechea) hadi kidato cha sita ili vijana wetu wote, bila kujali dini zao, wapate elimu na huduma za afya kutoka katika shule na zahanati hiyo,” amesema Dkt. Nyansaho.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria harambee hiyo ambao ni pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. George Masaju, Mkuu wa Majeshi,Jenerali Jacob Mkunda, Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi,Dkt. David Mpwani, Askofu Kanisa la Waadventista Wasabato, Mara Kaskazini,MNEC Christopher Gachuma,Chifu Peter Zakaria, Chacha Soya na wabunge wa mkoa wa Mara.
Uchangiaji huu unaonyesha umoja na mshikamano kwa wananchi na Viongozi wa Serikali, wanasiasa na viongozi wa dini katika ujenzi wa Taifa na kuleta Maendeleo nchini.

.jpg)
.jpg)




















Maoni