Machapisho

TUMUOMBEE RAIS, TULIOMBEE TAIFA-MASHILI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Nzega.  WATANZANIA wamehamasishwa kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kupata utulivu wa kuliongoza Taifa la Tanzania kwa amani, upendo na mshikamano. Rai hiyo imetolewa leo Aprili 19, 2026 na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MASHILI COMPANY LIMITED ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Uchenjuaji Dhahabu wa (Matinje Mining, Msilale Mining na Igurubi Mining) Ndg Peter Andrea Mashili aliposhiriki tamasha la Inland Festival lililoandaliwa na kanisa la Africa Inland Church Tanzania - AIC Wilayani Nzega mkoani Tabora. Mashili amesema kuwa Mhe Rais Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuifungua nchi na kuleta maendeleo hivyo ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanamuombea ili aweze kuongoza kwa busara na mshikamano wa kitaifa. Pia Mashili amewataka viongozi wa dini na wananchi wote wa wilaya ya Nzega kumuombea Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini Mhe Hussein Bashe ili aweze kuitumikia nafasi yake kwa ...

HAMISI KIM KOMANDO AWAPA COMPUTER MAKIBA SEKONDARI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Arumeru.  MDAU wa madini ya Tanzanite, Hamisi Kim Komando ametoa zawadi ya kompyuta shule ya sekondari Makiba ya Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwa ajili ya matumizi ya masomo ya Tehama. Kim ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Makiba ameeleza hayo kwenye maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa shule hiyo mwaka 1996 na mahafali ya 15 ya kidato cha sita. Amesema anaiunga mkono shule hiyo kwa kununua kompyuta moja kwa ajili ya wanafunzi hao waboreshewe suala zima la Tehama. "Nawapongeza wanafunzi wote kwa kuhitimu kidato cha sita na ninawatakia kila la heri katika mtihani wenu mtakaofanya hivi karibuni," amesema Kim. Mkuu wa shule ya sekondari Makiba, Paul Kimaro amesema wameweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto ili wanafunzi wasome kidijitali kwa kutumia kompyuta. Kimaro amesema wanaendelea kutafuta wadau wa maendeleo, kuboresha usimamizi wa rasilimali zilizopo na kuhamasisha matumizi sahihi ya Tehama katika el...

MOKIA OLE MREFU AWATAKIA KILA LA HERI MAKIBA SEKONDARI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Arumeru.  MWENYEKITI wa chama cha wafanyabishara wa madini Mkoa wa Manyara na kurugenzi ya Habari na Mawasiliano wa chama cha wafanyabishara wa madini Taifa (CHAMMATA) Mokia Ole Mrefu, amewajengea uwezo na kuwapa moyo wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari Makiba Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, wanaotarajia kufanya mtihani wao wa kuhitimu hivi karibuni. Ole Mrefu amezungumza na wanafunzi hao kwenye maadhimisho ya miaka 30 tangu shule hiyo ianzishwe na mahafali ya 15 ya kidato cha sita kwa kuwatakia kila la heri katika mtihani wao wa kuhitimu. 'Hongereni sana vijana wetu jasiri wa kidato cha sita mnaojiandaa kuhitimu, leo nasimama kuwapa moyo na kuwakumbusha jambo moja muhimu: mmefika hapa si kwa bahati, bali kwa juhudi, nidhamu, na uvumilivu wenu," amesema Ole Mrefu . Ameeleza kwamba safari waliyoipitia imekuwa na changamoto nyingi, masomo magumu, mitihani ya majaribio, na nyakati za kuchoka, lakini bado mmesimama imara, hiyo peke yake ni ushin...

WITO WATOLEWA KUIMARISHA UDHIBITI WA MAGONJWA YA MAZINGIRA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Morogoro.  SERIKALI imetoa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya sekta mbalimbali ili kudhibiti magonjwa yanayotokana na mazingira, hatua inayolenga kulinda afya ya jamii na kuzuia milipuko ya magonjwa. Rai hiyo imetolewa Aprili 18, 2026, mkoani Morogoro katika kikao cha kuandaa mwongozo wa ufuatiliaji wa viashiria vya mazingira na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dkt. Otilia Gowelle,  Dkt. Gowelle amesema sekta zinazopaswa kushirikiana kuwa ni pamoja na afya ya mazingira, maji, mamlaka za serikali za mitaa, taasisi za utafiti, wadau wa maendeleo na mashirika yasiyo ya kiserikali. “Ubunifu, maelewano na ushirikiano ni nguzo muhimu katika kuilinda nchi dhidi ya magonjwa yatokanayo na mazingira hivyo wajibu wetu kuhakikisha mwongozo huu unatumika kuleta mabadiliko chanya ya afya ya jamii” amesema Dkt. Gowelle. Gowelle, amepongeza timu ya wataalamu kwa juhudi za kukusanya na kuandaa maarifa yao katika mwongozo unaozingatia sera zilizopo, akibainisha kuwa ...

HONGERA FRANONE MINING UJENZI ZAHANATI MIGODINI

Picha
  Na mwandishi wetu, Mirerani  MACHIMBO ya madini ya Tanzanite, Mji mdogo wa Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, ina migodi 2,000 yenye leseni hai 145 na watu 12,000 wenye kuingia na kutoka kila siku wakiwemo 5,000 wanaolala eneo hilo, haina hospitali wala kituo cha afya, hata zahanati. Wataalamu watetezi wa haki za binadamu wanaeleza kuwa haki kubwa kuliko zote ni haki ya kuishi kwani ukiwa hai utaweza kupata haki nyingine zilizobaki hivyo ili uishi inapaswa miundombinu ya afya nayo iwepo. Wataalamu hao wanaeleza kwamba uhai ni muhimu katika maisha ya binadamu ndiyo sababu mtu akiugua au akipata ajali anapelekwa hospitalini, kituo cha afya au zahanati, kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Fakii Lulandana hivi karibuni alifanya ziara kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite na kukagua zahanati inayojengwa na kampuni ya Franone Mining waliojitolea kwa ajili ya kutoa matibabu kwa wachimbaji madini. Kwa ujenzi wa zahanati hiyo katika migodi ya madin...

ASKARI WA TFS WAPONGEZWA KULINDA SHAMBA LA MITI SILAYO.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Chato WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),amewapongeza askari wa uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanaofanya kazi katika Shamba la Miti Silayo, wilayani Chato, kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda na kuhifadhi shamba hilo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Dkt. Kijaji ametoa pongezi hizo leo, Aprili 16, 2026, alipokuwa katika ziara ya kukagua shamba hilo, akibainisha kuwa mafanikio yaliyopatikana yametokana na ari ya kujituma, mshikamano na umoja wa askari hao katika kuhakikisha shamba linabaki katika hali bora na ya kuridhisha. “Niwapongeze sana askari wetu mnaofanya kazi nzuri sana huku uwandani. Kazi yenu ni njema mno, tunawapongeza sana. Na pongezi hizi hazitoki kwangu tu, bali zinatoka moja kwa moja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amenituma kuwafikishia pongezi hizi,” amesema Dkt. Kijaji. Aidha, ameongeza kuwa kazi wanayoifanya askari hao ni muhimu sana ...

CCM YATAKA WATENDAJI, WATAALAMU KUWAJIBIKA IPASAVYO

Picha
  Na Gilbert Dioniz na Allan Kitwe, Ngara CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Ngara Mkoani  Kagera kimewataka Watendaji na Wataalamu waliopewa dhamana kusimamia miradi ya maendeleo kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao ili kuharakisha maendeleo ya wananchi. Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngara Vitalice Ndairagije kwenye ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya kukagua miradi ya maendeleo. Amesema kuwa kiu ya wananchi ni kuona miradi inayotekelezwa na serikali yao inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, na hili haliwezi kufanikiwa kama Watendaji na Wataalamu waliopewa dhamana hawatafanya kazi kwa weledi. ‘Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuleta mamilioni ya fedha hapa Ngara kwa ajili ya miradi ya maendeleo, fedha hizi tunataka zifanye kazi iliyokusudiwa na zisimamiwe ipasavyo’, amesema. Mwenyekiti alidokeza kuwa miradi ikisimamiwa ipasavyo itakamilika kwa wakati na thamani ya fedha zilizotumika ...

HATUA MPYA PANGANI! USAMBAZAJI WA MITUNGI YA GESI YA RUZUKU WAANZA RASMI

Picha
  Na Mwandishi Wetu Pangani.  WILAYA ya Pangani mkoani Tanga imepiga hatua muhimu katika kuboresha maisha ya wananchi wake kupitia utambulisho wa mradi wa uuzaji na usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku. Mradi huo unalenga kuongeza upatikanaji wa nishati safi na salama ya kupikia, hususan kwa kaya zenye kipato cha chini. Akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha mradi huo mbele ya katibu tawala wa Wilaya ya Pangani, Bi. Ester Gama, msimamizi wa mradi  kutoka REA, Ndugu Abdulrazack Mkomi ameeleza kuwa lengo kuu la mradi huo ni kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, ambayo yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira pamoja na athari za kiafya kwa wananchi, hasa wanawake na watoto. Alifafanua kuwa kupitia mradi huo, mitungi ya gesi ya kilo sita itapatikana kwa bei nafuu ya shilingi 17,500 tu kutokana na ruzuku iliyotolewa, hali itakayowezesha wananchi wengi zaidi kuimudu na kuanza kutumia nishati mbadala iliyo rafiki kwa mazingira.  Aidha, mfumo mz...

SALALI: AIPONGEZA SERIKALI KUANDA SERA INAYOZINGATIA MAKUNDI MAALUM

Picha
  Na Carlos Claudio, Dodoma. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation Disability Hope (FDH), Maiko Salali, ameipongeza serikali kwa kuandaa sera jumuishi inayozingatia makundi maalum, ikiwemo watu wenye ulemavu, hatua aliyoieleza kuwa ni muhimu katika kukuza usawa wa kijamii na kiuchumi nchini. Akizungumza leo Jumatano, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ya Mwaka 2025, Salali alisema sera hiyo imezingatia kwa kiasi kikubwa dhana ya ujumuishwaji. Alieleza kuwa utekelezaji wa sheria ya ununuzi wa umma inayotenga asilimia 30 kwa makundi maalum umeendelea kufungua milango ya fursa kwa watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. “Tumeridhishwa na namna sera hii ilivyozingatia ujumuishwaji. Hata watu wenye ulemavu wa kuona wamewezeshwa kuipata sera hii kupitia maandishi ya nukta nundu,” alisema Salali. Aidha, alibainisha kuwa uongozi wa Rais S...

WADAU WA KILIMO WAOMBA SERIKALI KUONDOA KODI YA ONGEZEKO (VAT)

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WADAU wa Kilimo wameiomba serikali kuondoka kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya asilimia 18 kwenye mifuko ya tabaka ya kuhifadhia mazao ya nafaka na mbegu ili kuwesha wakulima kuongeza kipato na usalama wa chakula. Hayo yalielezwa Jijini Dodoma  na Afisa Mradi Jukwaa la Wadau wa Kilimo wasiokuwa wa Kiserikali (ANSAF)  Werner Hillary wakati akifungua warsha ya kujadili maboresho ya kisera ili kudhibiti changamoto za upotevu kwa wakulima wadogo kwa kushirikiana na Shirika la Helvetas. " Warsha hii ilitohusisha wadau mbalimbali wa Kilimo ikiwemo Serikali, wazalishaji wadogo na Asasi za Kiraia ni sehemu ya mradi unaotekelezwa kwa ushirikiani wa Helvetas Tanzania, SAT, Chuo cha Kilimo SUA na Chuo Kikuu cha Zurich. Afisa huyo amesema lengo la wadau kuiomba Serikali kuondoa kodi ya VAT ni kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kununua na kutumia mifuko hiyo inayozuia wadudu waharibifu na upotevu wa nafaka. "Matumizi ya mifuko ya tabaka hus...

ENABEL YAWEZESHA MABINTI 200 KASULU KUPATA ELIMU

Picha
  Na Allan Kitwe, Kasulu.  SHIRIKA la Maendeleo la Ubelegiji (ENABEL) limeunga mkono juhudi za serikali kwa kuwezesha watoto wa kike zaidi ya 200 Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma kupata mafunzo ya ujuzi katika Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Kasulu (FDC). Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Chuo hicho Fridegarda Mukyanuzi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake ambapo ameeleza kufurahishwa na ujio wa mradi huo ili kuwezesha wasichana wasio na uwezo. Amebainisha kuwa kupitia mradi huo Shirika limegharamia mahitaji yote ya Chuo kwa watoto hao na kuwawezesha kusoma fani mbalimbali za ufundi ikiwemo ushonaji nguo, ususi na urembo, umeme wa majumbani na ufundi bomba. Fani nyingine ni ufundi magari, uchomeleaji na uungaji vyuma, umeme wa magari na wa majumbani na kila wanapohitimu Shirika huwawezesha vifaa vya kuanzia shughuli zao. Amefafanua kuwa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 600 umekuwa mkombozi kwa Chuo na kwa watoto hao kwani umesaidia kuboresha...

AKAMATWA NA POLISI KWA KUTOA MIMBA YA MIEZI 6

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora JESHI la Polisi Mkoani Tabora linamshikilia mwanamke mmoja (21) mkazi wa Mtaa wa Singo, Kata ya Gongoni katika halmashauri ya manispaa Tabora kwa tuhuma za kutoa ujauzito wake unaokadiriwa kuwa na umri wa miezi 6. Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Richard Abwao amethibitisha kutokea tukio hilo Aprili 6 mwaka huu majira ya saa 12.45 za jioni katika Kata hiyo ambapo mwanamke huyo mpare, mkristo na mkulima aligundulika kufanya kitendo hicho. Amesema kuwa mtuhumiwa baada ya kumeza dawa ya kutoa ujauzito huo, uchafu aliuweka kwenye kopo na kuufunga kwenye mfuko ili akautupe kwenye shimo la takataka lililo jirani na eneo hilo. Kamanda ameongeza kuwa mbali na mtuhumiwa huyo pia wamemkamata mwanaume mmoja (25) msukuma, mkazi wa Kata ya Chemchem katika manispaa hiyo ambaye ni Mtaalaumu wa Maabara aliyempatia dawa za kutolea mimba hiyo. Ameeleza sababu ya kutoa ujauzito huo kuwa ni mwanaume aliyempa mimba hiyo kuikataa hivyo akaamua kwenda kwa Mtaalaumu binafsi wa Maabara ili ...

MRADI WA ESP KUNUFAISHA WASICHANA ZAIDI YA 60 NZEGA.

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora.  WASICHANA zaidi ya 60 wanaotoka katika familia zisizo na uwezo Wilayani Nzega Mkoani Tabora wanatarajiwa kunufaika na mradi wa uwezeshaji mtoto wa kike kupata ujuzi (Empowerment Through Skills Program in Tanzania-ESP). Mradi huo unaofadhiliwa na nchi ya Canada (Canada Fund) kwa lengo la kuwezesha watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kupata fursa za ujuzi, unatekelezwa katika Vyuo 12 viivyopo katika Mikoa zaidi ya 8 hapa nchini. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Mwanhala, Nzega ni miongoni mwa vyuo 12 vilivyoingizwa katika program ya ufadhili ili kutoa mafunzo hayo ya muda mfupi (short course) kwa watoto wa kike.   Akizungumza juzi na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho Enock Lalida, Afisa Utumishi Hekima Amri Lupembe ameeleza kuwa mradi huo ni muhimu sana kwa kuwa unawapa fursa watoto wa kike kupata ujuzi. ‘Wasichana 30 wanaotoka katika kaya zinazoishi katika mazingira magumu Wilayani hapa tayari wamesajiliwa na kuan...

RUWASA KIGOMA WAMWAGA PONGEZI KWA RAIS SAMIA

Picha
  Na Allan Kitwe, Kigoma.  WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoani Kigoma wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 79 za miradi ya maji. Pongezi hizo zimetolewa na Meneja wa Wakala huo Mkoani hapa Mhandisi Mathius Mwenda alipokuwa akiongea kwenye mahojiano maalumu na waandishi wa habari Ofisini kwake. Amesema kuwa RUWASA Kigoma ina kila sababu ya kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kufanikisha utekelezaji miradi mbalimbali ya maji katika Wilaya zote 7 za Mkoa huo hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa kero ya maji. Mhandisi Mwenda amebainisha kuwa kuanzia Machi 2021 hadi Februari 2026, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alitenga zaidi ya shilingi bilioni 79 kwa ajili ya kutekeleza miradi 113 ya maji katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo. Amedokeza kuwa kati ya kiasi hicho cha fedha, serikali ilitoa jumla ya shilingi bilioni 55.9 na wadau wakaiunga mkono kwa kutoa kiasi cha shiling...