Machapisho

WATAALAM WA MAABARA WATAKIWA KUSIMAMIA WELEDI NA MATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. Wataalam wa maabara wametakiwa kusimamia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kuhakikisha matumizi sahihi ya rasilimali ili kuboresha utoaji wa huduma bora za afya kwa jamii. Wito huo umetolewa leo, Desemba 19, 2025, na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Afya Bw. Issa Ng’imba wakati wa mahafali ya mafunzo ya Global Laboratory Leadership Program (GLLP) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Bw. Ng’imba amesema mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo viongozi chipukizi wa maabara katika masuala ya uongozi na kuwapa mbinu za kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi.  Ameongeza kuwa mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka, hasa katika kipindi ambacho kuna hitaji la kuimarisha mifumo ya maabara, hususan katika masuala ya utawala, utatuzi wa kero za wagonjwa, upimaji pamoja na ushiriki katika ufuatiliaji wa magonjwa. “Niishukuru Serikali pamoja na mdau wetu, Global Fund, kwa kutambua umuhimu wa ku...

MABORESHO SEKTA YA AFYA YAGUSA WANANCHI TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, TABORA. VIONGOZI na Wadau mbalimbali Mkoani Tabora wamepongeza juhudi kubwa zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuboresha huduma za afya. Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa maboresho makubwa ya miundombinu ya huduma za afya yaliyofanywa na serikali ya Awamu ya Sita yameleta na mageuzi makubwa katika sekta  hiyo. Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoani hapa, Idd Moshi ameeleza kuwa ndoto ya Watanzania kupata huduma bora na za uhakika za afya imeanza kutimia baada ya maboresho makubwa ya miundombinu na ujenzi wa hospitali mpya za Wilaya, Vituo vya afya na zahanati katika Wilaya, Kata na Vijiji vyote.. Ameongeza kuwa hata kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu Rais Samia aliahidi kutekeleza mpango wa Huduma ya Bima ya Afya kwa wote ndani ya siku 100 tuu akiingia madarakani... 'Hii ni habari njema kwa Watanzania wote na inaonesha jinsi Rais ...

MWENYEKITI SIKONGE AHIMIZA KASI YA MAENDELEO

Picha
  Na Allan Kitwe, Sikonge. MWENYEKITI wa Halmasahauri ya Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora Andrea Gasto amewataka Madiwani na Watendaji wa halmashauri hiyo kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya sita katika kukusanya mapato ili kuharakisha maendeleo. Ametoa rai hiyo jana alipokuwa akiongea na watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo baada ya kuchaguliwa kwa kishindo kuongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, yaani 2025-2030. Amesema kuwa wakazi wa Halmashauri hiyo wana imani na matumaini makubwa na madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo na wako tayari kuwapa ushirikiano ili kuchocheo kasi ya maendeleo yao. Mwenyekiti amedokeza kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alishatoa mwelekeo wa yale atakayowafanyia wana Sikonge ndani ya siku 100 na mengineyo mengi kama yalivyobainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030. ‘Wakazi wa Sikonge wana imani kubwa na serikali yao ya Chama Cha Mapinduzi, naomba kila mmoja aliyepewa dhamana ya kusimamia maendeleo yao ...

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro MWENYEKITI wa kijiji cha Namalulu Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Marumai Kirikai amepumzishwa kazi kwa muda wa siku 28 ili kupisha uchunguzi wa matumizi mabaya ya madaraka katika kijiji hicho. Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Raphael Lulandala ameunda kamati ya watu saba itakayofanya uchunguzi kwa muda wa siku 24 na baada ya siku 28 endapo  Mwenyekiti huyo atabainika hausiki na tuhuma hizo atarejea kwenye nafasi yake. Lulandala ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Namalulu, baada ya kusikiliza kero, malalamiko na changamoto zao. Ameeleza kwamba hamsimamishi kazi Mwenyekiti huyo ila anapisha uchunguzi kwa muda wa siku 28 na endapo hatakuwa na makosa atarejea tena kwenye nafasi hiyo. "Hausimamishwi kaz ila unakaa pembeni kwa muda wa siku 28 ili kupisha uchunguzi na ofisa mtendaji wa kijiji cha Namalulu Sarafina Olotu ataongoza kijiji kwa kipindi hiki," amesema DC Lulandala. DC Lulandala amewataja wajumbe saba wa kamati ...

MAREMA WANUNUA UWANJA WA MILIONI 30

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani  CHAMA cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) kimenunua kiwanja cha thamani ya Sh30 milioni kwa ajili ya ujenzi wa matumizi ya ofisi na ukumbi wa mikutano. Chama hicho cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara hakina ofisi ambayo ni mali yao hivyo kupitia kiwanja hicho watajenga ofisi zao na ukumbi wa mikutano. Mwenyekiti wa Marema, Elisha Nelson Mnyawi ameyasema hayo kwenye mkutano mkuu wa mwaka 2025 wa wanachama wa MAREMA, Tawi la Mirerani ambao wanachimba madini ya Tanzanite na kinywe. Mnyawi amesema kwa sababu makao makuu ya MAREMA yapo Mirerani, wamenunua kiwanja hicho kwa ajili ya kujenga ofisi zao na ukumbi. "Ninawashukuru Makamu Mwenyekiti Money Yusuf, kampuni ya California, Joseph Manga na mimi mwenyewe kwa kutoa Sh5 milioni kila mmoja kwa ajili ya kununua kiwanja hicho," amesema Mnyawi. Amesema lengo ni kuhakikisha MAREMA inakuwa na ofisi yake na kila tawi linakuwa na ofisi zake kwa lengo la kuwatumikia wachimbaji madini wa Manyara....

JAFO: MAONO YA RAIS SAMIA NI NGUZO YA MAENDELEO YA TAIFA

Picha
  Na Alex Sona, Kisarawe. MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, amewaomba wananchi wa Kisarawe na watanzania kwa ujumla kumuombea Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ana maono makubwa ya kuwatumikia Watanzania na kulisukuma Taifa mbele kimaendeleo. Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza katika kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe, kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo. “Niwaombe wajumbe wa Halmashauri Kuu kuhakikisha tunamuombea Rais Dkt. Samia kwa kuwa ana kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo Watanzania na kuhakikisha Taifa letu linaendelea kusonga mbele,” amesema Dkt.Jafo. Ameongeza kuwa amani na usalama ni nguzo muhimu za maendeleo ya kiuchumi, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kumuombea Rais na Taifa kwa ujumla. “Bila amani na usalama, nchi yetu haiwezi kupata...

HABARI PICHA

Picha
Wajumbe wa Mkutano wakifuatilia mada juu ya Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora zinazotolewa wakati wa mafunzo ya Sekretarieti ya Kusimamia Maadili na Kushughulikia Mrejesho ya Makao Makuu ya Polisi yanayofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) Disemba 17, 2025.

DKT SEIF- TUREJESHE TABASAMU KWA WANANCHI KWA KUTOA HUDUMA BORA

Picha
Na Lubango Mleka, Mwanza. VIONGOZI katika ngazi zote wametakiwa kuhakikisha wanarejesha tabasamu kwa watanzania kwa kuwapeleka huduma bora ikiwa ni sambamba na kusimamia na kutunza miundombinu iliyopo ili iweze kuleta tija na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Jafar Seif (MB) tarehe 16 Desemba, 2025 na) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Manispaa ya Ilemela ambapo lengo kuu la ziara ni  kutembelea miradi ya afya pamoja na kukutana na watumishi kwa ajili ya kujadili na kubaini changamoto zinazoikablili sekta hiyo katika utoaji wa huduma kwa wananchi. “Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunamsaidia Mhe. Rais kurudisha tabasamu kwa watanzania, ahadi ambayo aliitoa wakati akilihutubia bunge la 13 ambapo aliahidi kwamba ndani ya awamu ya sita kipindi cha pili tuhakikishe tunarejesha tabasamu kwa watanzania kw...

TASAC YAKUSANYA MAONI YA MAREKEBISHO YA NAULI ZA MV. BIJLEE NA MV. NYEHUNGE

Picha
  Na Lubango Mleka, Mwanza. SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), leo tarehe 16 Desemba 2025 limefanya mkutano wa wadau jijini Mwanza kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu maombi ya marekebisho ya nauli za meli za MV. Bijlee na MV. Nyehunge, zinazofanya safari kati ya Mwanza na Nansio- Ukerewe katika Ziwa Victoria. Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Dominic ulifunguliwa rasmi na Bw. Nahson Sigalla, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, waendeshaji wa meli, pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri wa majini jijini Mwanza.  Akizungumza wakati wa ufunguzi, Bw. Sigalla amesema kuwa maombi ya marekebisho ya nauli yamewasilishwa na Kampuni ya Manoj V. Mehta Investments Ltd., waendeshaji wa MV. Bijlee, na Said Mohamed & Brothers Co. Ltd., waendeshaji wa MV. Nyehunge. Alieleza kuwa kikao hicho kimeandaliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura ya 415, kinachotaka ushirikishwaji wa wadau ...

TANTRADE YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA UBUNIFU SEKTA YA UMMA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki na kushinda tuzo ya Ubora katika Uhamasishaji Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Uchumi. Tuzo hizo za sekta ya Umma zinaangazia ubunifu unaofanywa na taasisi mbalimbali za umma kwa muktadha wa kutoa huduma bora zinazoakisi maendeleo endelevu ya uchumi wa Tanzania.  TanTrade imekua ikifanikisha hayo kupitia Maonesho ya Sabasaba, kuratibu Maonesho mbalimbali ya Kimataifa kama vile Expo's, Mifumo mbalimbali ya Kidigitali ya Biashara kama vile Trade Portal, Biashara App, nk. Hafla ya tuzo hizo zimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.