MABORESHO SEKTA YA AFYA YAGUSA WANANCHI TABORA
Na Allan Kitwe, TABORA.
VIONGOZI na Wadau mbalimbali Mkoani Tabora wamepongeza juhudi kubwa zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuboresha huduma za afya.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa maboresho makubwa ya miundombinu ya huduma za afya yaliyofanywa na serikali ya Awamu ya Sita yameleta na mageuzi makubwa katika sekta hiyo.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoani hapa, Idd Moshi ameeleza kuwa ndoto ya Watanzania kupata huduma bora na za uhakika za afya imeanza kutimia baada ya maboresho makubwa ya miundombinu na ujenzi wa hospitali mpya za Wilaya, Vituo vya afya na zahanati katika Wilaya, Kata na Vijiji vyote..
Ameongeza kuwa hata kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu Rais Samia aliahidi kutekeleza mpango wa Huduma ya Bima ya Afya kwa wote ndani ya siku 100 tuu akiingia madarakani...
'Hii ni habari njema kwa Watanzania wote na inaonesha jinsi Rais wetu alivyo na dhamira ya dhati ya kumaliza kero ya upatikanaji huduma za afya za uhakika kwa wananchi wake', amesema.
Amefafanua kuwa Bima hii ni mkombozi kwa wananchi wote waishio vijijini na mijini kwa kuwa itawawezesha kupata matibabu mahali popote pale hakuna mwananchi yeyote atakaye achwa ateseke punde tu itakapoanza.
Mwenezi ameomba Wizara ya Afya na Halmashauri zote kusimamia kwa dhati upatikanaji huduma za afya na kutatua kwa dhati kero zote zinazokwaza wananchi..
Naye mdau wa Maendeleo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi wa Jadi katika halmashauri ya manispaa Tabora Elisha Daud Mponeja ameeleza kufurahishwa na mazuri yote yaliyofanwa na serikali ya Awamu ya Sita..
Ameomba Maafisa wa serikali waliopewa dhamana ya kumsaidia Mheshimiwa Rais kuhakikisha wanawatendea haki wananchi ikiwemo kutozuia miili ya ndugu zao wanaopoteza maisha kwa kushindwa kulipia gharama zao za matibabu.




Maoni