AMUUA MWANAYE KWA KIPIGO
Na Mwandishi Wetu, Mbeya. MWANAMKE Mmoja aitwaye ,Marry Timotheo mkazi wa kijiji cha Garijembe kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga na kitu kizito kichwani mtoto wake, Scola Mwaba(10)kwa madai ya kuzidi utukutu kisha mwili wake kutupa shamba lilo karibu na nyumbani anakoishi . Akizungumzia tukio hilo Desemba 10,2025 Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema marehemu Scola alikuwa Mwanafunzi wa Darasa la Nne shule ya Msingi Ngonde wilaya ya Mbeya. Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Desemba 9,2025 ,majira ya saa 6.30 mchana katika Kijiji cha Garijembe ,Kata na Tarafa ya Tembela Wilaya ya Mbeya. "Mama wa marehemu alimshambulia kwa kitu kizito kichwani mtoto wake kwa madai ya kuzidi utukutu kisha mwili wake kutupa jirani na shamba la nyumba anakoishi "amesema Kamanda Kuzaga. Aidha Kuzaga ameeleza kuwa pia licha ya kumshikilia mama wa marehemu ,pia jirani yake ,Sharifa Nz...