WAZIRI MAVUNDE: USUSI SI KAZI YA AIBU KWA VIJANA WA KIUME
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WAZIRI wa Madini, na mgombea ubunge Jimbo la Mtumba Anthony Mavunde amesema hakuna sababu ya vijana wa kiume kubezwa au kutazamwa kwa jicho la ajabu wanapoamua kujihusisha na kazi ya ususi, kwani ni kazi halali kama nyingine yoyote. Amesema hayo jijini Dodoma katika uzinduzi wa Siku ya Wasusi, uliowakutanisha wasusi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, ambapo alisisitiza kuwa jamii haina budi kuachana na mitazamo ya kudhalilisha kazi zinazofanywa na watu kwa bidii na maarifa yao. Mavunde amesema kuwa kazi ya ususi imekuwa mkombozi kwa vijana wengi, hususan wanawake, lakini sasa pia imekuwa ikiwavutia baadhi ya vijana wa kiume, jambo linalopaswa kuungwa mkono badala ya kubezwa. Ameongeza kuwa moja ya malengo yake ni kuhakikisha ususi unaboreshwa ili kuifanya kuwa kazi ya heshima na inayotambulika rasmi, huku serikali ikijiandaa kutoa mafunzo rasmi kwa vijana kupitia vyuo vya ufundi kama VETA. "Tayari serikali imeanza kushirikiana na VETA...