MAJIKO BANIFU KUPUNGUZA MATUMIZI YA MKAA NA KUNI MBEYA
*Majiko banifu 9,330 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Mbeya. Wilaya Sita kunufaika na mradi. Kila Wilaya kupata majiko 1,555* Na Mwandishi Wetu, Mbeya. SERIKALI ya Mkoa wa Mbeya kupitia Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu, Rodrick Mpogolo leo Jumanne Septemba 2, 2025 imepokea mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu 9,330 yenye ufanisi mkubwa katika utumiaji wake. Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya mradi Mhandisi wa miradi kutoka wakala wa nishaji vijijini (REA), Raya Majallah amesema, Kupitia utafiti uliofanyika 2016 unakadiria kuwa takribani watu 33,024 hufariki kabla ya wakati kila mwaka hii ni sawa na asilimia 8.49 ya vifo vyote nchini Tanzania, kutokana na magonjwa ambayo yanachangiwa na uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba wakati wa upikaji kwa kutumia nishati isiyo safi na salama. Hivyo kwa kutambua hilo, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imeaanda mpango wa uuzaji na usambazaji majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku ili kupu...