Machapisho

TAARIFA KWA UMMA

Picha
Gaza  ABU Obeida, anayejulikana kwa kuonekana akiwa amejifunika uso kwenye ujumbe wa video, alikuwa msemaji wa kikosi cha kijeshi cha Qassam na sauti kuu ya propaganda ya Hamas. Tangu kuanza kwa vita vya Gaza, Israel imewaua viongozi kadhaa wa Hamas, akiwemo Yahya Sinwar, anaetajwa kuwa mpangaji mkuu wa mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 kusini mwa Israel.  #Gaza #Israel #Hamas #AbuObeida #MiddleEastConflict Credit DW. 

JESHI LA ISRAEL LAFANYA MASHAMBULIZI USIKU KUCHA GAZA

Picha
JESHI la Israel limefanya mashambulizi ya usiku kucha kwenye maeneo yaliyoko Mjini Gaza kutokea angani na ardhini na kuharibu majumba na kuzilazimu familia zaidi kuondoka eneo hilo. #Gaza #Israel #evacuation

NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUTUMIKA MAGEREZA YOTE NCHINI

Picha
Matukio mbalimbali katika picha yakimuonesha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia magerezani, iliyofanyika Agosti 30, 2025, Gereza Karanga, Kilimanjaro.

ABIRI AKAMATWA BAADA YA KUMPIGA NGUMI MUHUDUMU WA KWENYE NDEGE

Picha
POLISI wamemkamata abiria kutoka kwenye ndege iliyowasili kutoka Saudia kwenye uwanja wa ndege huko Heathrow mapema Alhamisi ya wiki iliyopita.  Polisi na Maofisa wa  Wazima Moto waliizingira ndege ya Saudia Airlines katika uwanja wa ndege wa Heathrow na kumkamata abiria wa kiume mwenye umri wa miaka 33 ambaye inadaiwa alimpiga ngumi mfanyakazi na kujaribu kufungua mlango wa ndege hiyo. Huduma za dharura zilikimbilia kwenye Boeing 787 muda mfupi baada ya kutua kutoka Jeddah majira ya saa 7 mchana ya Alhamisi. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, ndege hiyo ilifunga breki kali kwenye barabara ya teksi kuelekea Terminal 4 baada ya tukio hilo, na kuwafanya marubani kuita usaidizi wa haraka. Ngazi ziliwekwa na maafisa walipanda ndege hiyo, iliyokuwa imebeba abiria kwenye Flight namba SV119. Picha zilizopatikana na gazeti la The Sun zinaonyesha angalau malori manne ya zima moto, magari sita ya polisi na ambulensi kadhaa kwenye eneo la tukio.

INEC YAKUTANA NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA KUPITIA NA KUFANYA MABADIRIKO MADOGO KWENYE MIKUTANO YA HADHARA YA RAIS NA MAKAMU RAIS.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 30 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais. Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Zanzibar. Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.

DK.MWINYI:CCM ITAFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KWA SERA ZENYE TIJA KWA WANANCHI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na kuahidi kuwa CCM itafanya kampeni za kistaarabu zitakazozingatia Utamaduni, Silka na Desturi za Wazanzibari. Dkt. Mwinyi amechukua fomu hiyo katika Afisi za Tume ya Uchaguzi leo, tarehe 30 Agosti 2025, asubuhi, na hatimaye msafara wake ukaelekea Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui kupitia Barabara ya Miembeni, Kariakoo, Rahaleo na Michenzani, akisindikizwa na mamia ya wanachama wa chama hicho waliokuwa wamejipanga pembezoni mwa barabara. Aidha, Dkt. Mwinyi amezuru Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, na kisha kuzungumza na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi afisini hapo. Akizungumza na mamia ya wanachama wa CCM katika Uwanja wa Mao Tse Tung, Mgombea Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuwa...

NDEGE YA KIVITA YAANGUKA MAZOEZINI

Picha
NDEGE aina ya F-16 imeanguka wakati wa mazoezi ya maonyesho ya ndege mjini Radom, katikati ya Poland, August 28.2025 Rubani alifariki kwa mujibu ya msemaji wa serikali #Poland #mazoeziyakijeshi #ndegeyavita

RAIS MWINYI AISHUKURU SERIKALI YA QATAR

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kiuchumi katika sekta mbalimbali yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 10. Hafla hiyo imefanyika Ikulu leo tarehe 29 Agosti 2025, ambapo kwa upande wa Qatar mkataba huo ulisainiwa na mmoja wa Wanafamilia ya Kifalme wa Qatar, Mhe. Sheikh Mansour Bin Jabor Bin Jassim Al Thani, ambaye pia ni Mmiliki wa Kampuni ya Al Mansour Holding itakayotekeleza miradi hiyo.  Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, utiaji saini uliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Ndg. Khamis Mwalim Suleiman. Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Qatar kwa kuonesha dhamira ya dhati ya kushirikiana na Zanzibar katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayohitaji uwekezaji mkubwa. Rais ...

JKT YATOA THANK YOU KWA YAKOUB SULEIMAN

Picha
JKT Tanzania🇹🇿  yaachana rasm na Golikipa Yakoub Suleiman na kuumtakia maisha mema katika majukumu yake mapya. #yakoub_suleiman_ #WajengaNchi #KichapoChaKizalendo

REA KUTEKELEZA KWA VITENDO MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Picha
📌 *Majiko banifu 5,176 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoa wa Iringa*  📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 14,300 tu* . Na Mwandishi Wetu, Iringa.  WAKATI Taifa likiwa kwenye mkakati wa kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi na salama ya kupikia, Wakala wa Nishati Vijijini umekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa  majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku yanayotumia kuni na mkaa mchache sana na yenye ufanisi mkubwa katika matumizi yake. Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa, Mhandisi Kelvin Tarimo amesema, Mradi huu umekuja kwa lengo la kuimarisha utunzaji wa Afya za wananchi na Mazingira, kukuza upatikanaji wa Nishati Safi na Endelevu, kupanua usambazaji wa nishati mbadala katika maeneo ya Vijijini na zaidi kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi kupitia teknolojia za kisasa na bora za kupikia. Mhandisi Tarimo ameendelea kwa kusema, Serikali kupitia wakala wa Nishati Vijijini umeandaa mpango huu wa usambazaji na uuzaji wa m...

MAAFISA NA ASKARI WA MAGEREZA WAUNGANA NA VYOMBO VINGINE VYA ULINZI MARA KATIKA MAZOEZI YA PAMOJA

Picha
MAAFISA na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mara, leo tarehe 29 Agosti 2025 wameshiriki mazoezi ya pamoja ya vyombo vya ulinzi na usalama.