Na Mwandishi Wetu. MKUU wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James kwa kutambua kazi iliyofanywa na serikali amewahimiza Wananchi mkoani humo kuhakikisha wanalinda na kuitunza miundombinu iliyojengwa katika sekta ya elimu mkoani humo ili iweze kutumika kwa muda mrefu na kuufikisha mkoa katika lengo la kuinufaisha jamii kielimu na taifa kwa ujumla. Ametoa rai hiyo wakati akizungumzia hatua zilizofikiwa na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu kupitia Mradi wa kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP). Mhe Kheri amesema kuwa Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 umepokea kiasi cha shilingi 21,017,700,420. Amesema fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Shule za Sekondari. Aidha, miundombinu iliyojengwa katika kipindi hicho ni pamoja na Shule mpya za kata, Shule ya wasichana ya Mkoa (Lugalo), Shule ya amali Mafinga, Mabweni, Madarasa, nyumba za walimu pamoja na ma...