Machapisho

CCM YASHITUKA KUHUSU MIKUTANO YA KUCHOCHEA MAAANDAMANO.

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinazo taarifa zinazoashiria kuwepo kwa mikutano inayofanywa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambayo inadaiwa kuhusisha mipango ya kuhamasisha maandamano yenye uwezekano wa kuvuruga hali ya amani nchini. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa CCM anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, alisema chama hicho kimeendelea kuwataka Watanzania kuzingatia umuhimu wa utulivu na mshikamano wa kitaifa. Kihongosi ameeleza kuwa CCM inaamini maendeleo endelevu hayawezi kupatikana iwapo kutakuwa na misukosuko ya kisiasa, akisisitiza kuwa tofauti za vyama zinapaswa kuishia kwenye majadiliano ya sera. Alisema chama hicho kinatoa tahadhari kwa wananchi kutoshawishika kushiriki katika matukio yanayoweza kusababisha machafuko, akibainisha kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa. “Taarifa tulizonazo zinaonyesha k...

WACHIMBAJI WATAKIWA KUJIUNGA WCF

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani.  WACHIMBAJI wa madini nchini wametakiwa kuwalipia wafanyakazi wao asilimia 0.5 ya mishahara yao ili kuwachangia kwenye mfuko wa fidia kwa wafanyakazi utakaowanufaisha pindi wakipata madhila kupitia mafao saba. Mwakilishi wa Meneja mkuu wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) Naanjela Msangi ameeleza hayo akizungumza na viongozi wa wachimbaji madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. Msangi ameeleza kuwa endapo wamiliki wa migodi wakiwalipia wafanyakazi wao asilimia 0.5 ya mishahara yao kila mwezi watanufaika na mambo mengi ikiwemo kujikinga na kuzuia vihatarishi vya ajali. Amesema endapo wafanyakazi wakichangiwa watanufaika kwa kulipwa fidia katika sekta rasmi wanaopata ajali, ugonjwa ama kufariki dunia. "Katika kuteketeza jukumu hili WCF inatoa jumla ya mafao saba ambayo ni huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa muda na wa kudumu na malipo kwa anayemhudumia mgonjwa," amesema Msangi. Ametaja mafao mengine ni ...

ZFCT YARIDHISHWA NA MAFUNZO YA FCC KUHUSU USIMAMIZI WA MASHAURI YA USHINDANI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  BARAZA la Ushindani Halali Zanzibar (ZFCT) limefanya ziara ya mafunzo katika Tume ya Ushindani ya Haki (FCC) kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala ya ushindani wa biashara, udhibiti wa bidhaa bandia pamoja na usimamizi wa mashauri yanayohusiana na ushindani. Ziara hiyo iliyofanyika katika ofisi za FCC Juni 10, 2026 Jijini Dar es Salaam, imeelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha mazingira ya biashara yanakuwa ya haki kwa wadau wote. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa alisema kuwa kubadilishana uzoefu na taasisi za ndani ya nchi ni muhimu katika kuimarisha mifumo ya usimamizi wa ushindani na kulinda maslahi ya watumiaji dhidi ya vitendo vinavyokiuka sheria za ushindani na biashara. Alisema ujumbe wa ZFCT unapata fursa ya kujifunza namna FCC inavyotekelez...

TCDC YATOA ELIMU YA MALIPO KWA NJIA YA BENKI NA SIMU WILAYA YA MEATU

Picha
Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imetoa mafunzo ya elimu kuhusu mfumo wa malipo ya zao la pamba kwa njia ya benki na simu katika Wilaya ya Meatu, mafunzo hayo yamehusisha Makatibu Mameneja, Wenyeviti na Makarani wa AMCOS 71 kutoka wilaya hiyo.

BAROZI MATINYI AKABIDHI HATI KWA RAIS WA ALGERIA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Algeria.  BAROZI wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare  Matinyi, amekabidhi hati za utambulisho wa kibalozi kwa Mhe. Rais Abdelmadjid Tebboune wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya jijini Algiers, tarehe 10 Juni, 2026, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu ya kibalozi. Katika mazungumzo yao mafupi yaliyofuatia baada ya hafla hiyo, Mhe. Balozi Matinyi alimshukuru Mhe. Rais Tebboune, serikali na watu wa Algeria kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kudumisha ushirikiano wa kindugu wa nchi hizi mbili ambao umedumu kwa zaidi ya miongo sita. Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mazungumzo yake na Mhe. Rais Tebboune, Balozi Matinyi alisema kwamba walijadiliana namna ya kusonga mbele baada ya kufikia mafanikio mazuri katika sekta za ulinzi na elimu ya juu ili kuhakikisha watu wa nchi hizi wananufaika pia katika sekta zingine muhimu. Mh...

UNYONYAJI WA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI BADO WATAJWA KUWA CHANGAMOTO

Picha
Na Jasmine Shamwepu, Habari Kamili Blog-Dodoma.  MATUKIO ya unyonyaji, mishahara duni na ukosefu wa mikataba ya ajira yameendelea kutajwa kuwa miongoni mwa changamoto zinazoathiri ustawi wa wafanyakazi wa majumbani nchini, hali inayochochea wito wa kuwepo kwa hatua zaidi za kuwalinda. Hayo yameelezwa na wadau wa sekta ya ajira wakati wa mkutano wa kujadili utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Kazi za Majumbani wa mwaka 2025/26 hadi 2029/30 uliofanyika jijini Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Majumbani nchini, Zanini Athumani, amesema pamoja na umuhimu wa kazi za majumbani katika jamii, bado baadhi ya wafanyakazi wanakabiliwa na mazingira yasiyozingatia haki zao za msingi. Amesema changamoto hizo zinajumuisha kucheleweshwa kwa mishahara, kutokuwepo kwa mikataba ya kazi na kukosekana kwa mifumo madhubuti ya kushughulikia malalamiko wanayokumbana nayo. “Wafanyakazi wengi wa majumbani bado wanahitaji ulinzi zaidi ili waweze kufanya kazi zao kwa usalama na kupata stahiki zao ...

WAKAZI USUNGA WAFURAHIA MRADI WA MAJI

Picha
  Na Allan Kitwe, Sikonge.  WAKAZI wa Kijiji Cha Usunga, Kata ya Usunga Wilayani Sikonge Mkoani Tabora wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea mradi wa maji safi na salama ya kunywa. Wametoa shukrani hizo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 58 tangu kuanzishwa kwa Kijiji hicho zilizofanyika jana kwenye uwanja wa CCM (Centre) na kueleza bayana kuwa serikali imemaliza kilio chao cha muda mrefu. Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho James Mgulu ameeleza kuwa mradi wa maji katika Kijiji hicho umeleta neema, furaha na shangwe kwa wananchi kwa sababu familia zao zilikuwa zinapata shida sana kwa kukosa maji safi na salama. ‘Tuna kila sababu ya kuishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea mradi huu wa maji na miradi mingine ya maendeleo, wananchi sasa wana amani tele, na maisha yao yamekuwa bora zaidi’, ameeleza.  Ameongeza kuwa wanapoadhimisha sherehe hiyo kila mwaka wanalenga kudumisha mila, utamad...

MIUNDOMBINU CHUO CHA NYUKI TABORA YABORESHWA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  CHUO Cha Ufugaji Nyuki (BTI) Tabora kimeendelea kuboresha miundombinu yake kwa kujenga jengo jipya la kisasa la mihadhara linalogharimu zaidi ya shilingi milioni 500, utekelezaji mradi huu umefikia zaidi ya asilimia 48. Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Chuo hicho Semu Daud alipokuwa akiongea na mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake, ambapo ameeleza kuwa jengo hilo litaboresha ufundishaji wa wakufunzi na kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa chuoni hapo. Amefafanua kuwa ujenzi wa jengo hilo unafadhiliwa na Mfuko wa Misitu Tanzania (TAFF) ambao wametoa kiasi cha shilingi milioni 500 sawa na asilimia 82 huku shilingi milioni 92 sawa na asilimia 20 zikitoka kwenye mfuko wa chuo. Ukumbi huo utakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 kwa wakati mmoja hivyo kukamilika kwake kutatoa fursa kwa wanafunzi wengi zaidi kujiunga na fani ya ufugaji nyuki. Mkuu amedokeza kuwa kupitia mradi huo mbali na wanafunzi kuongezeka chuoni hapo pia utasaidia kufa...

WILAYA YA LUSHOTO YAPOKEA MRADI WQ USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MITUNGI YA GESI KWA BEI YA RUZUKU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Lushoto - Tanga.  WANANCHI wa Wilaya ya Lushoto wamepata fursa mpya ya kunufaika na nishati safi ya kupikia baada ya wilaya hiyo kupokea rasmi mradi wa usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).  Mradi huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mheshimiwa Zephania Sumaye, kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha nishati safi ya kupikia inawafikia Watanzania wengi zaidi. Hafla ya mapokezi ya mradi huo imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, maafisa kutoka REA pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Manjis Logistics Limited, ambayo imepewa jukumu la kutekeleza mradi huo kwa kushirikiana na REA. Mradi huo ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na REA nchini kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa nishati safi na salama kwa wananchi, kupunguza utegemezi wa kuni ...

ZAIDI YA WAKULIMA 200 WA ZAO LA PAMBA WAFUNGUA AKAUNTI IGUNGA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Igunga.  ZAIDI ya wakulima 200 wa zao la pamba kutoka vijiji vya Mwahalanga, Bukama, Mwabakima, Jogoya na Jilelabalimi vilivyopo katika Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora, wamefungua akaunti za benki na kusajili laini za simu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kupokea malipo ya mazao yao kwa njia ya kidijitali, hatua inayolenga kuongeza uwazi, usalama na uharaka wa malipo. Wakulima hao wamefungua akaunti kupitia Benki ya NMB pamoja na kusajili laini kupitia Mtandao wa simu wa Mixx by Yas, hatua ambayo itawawezesha kupokea fedha zao kwa urahisi kupitia mifumo ya benki na simu za mkononi. Ufunguzi wa akaunti hizo na usajili wa laini za simu unatekelezwa kufuatia maelekezo ya waraka wa Mrajis wa Vyama vya Ushirika unaozitaka AMCOS za wakulima wa pamba kuhakikisha malipo ya wakulima yanafanyika kupitia akaunti za benki na huduma za fedha kwa njia ya simu, badala ya kutumia mfumo wa malipo ya fedha taslimu (cash).  Lengo la hatua hiyo ni kuongeza uwazi, usalam...

TANZANIA NA UTURUKI KUIMARISHA BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA

Picha
  Na Lubango Mleka.  WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga, akiwa katika ziara ya kikazi nchini Uturuki Juni 06, 2026, Jijini Istanbul amefanya mazungumzo na Waziri wa Viwanda na Teknolojia wa Uturuki, Mehmet Fatih Kacır pamoja na Waziri wa Biashara wa Uturuki, Ömer Bolat, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na viwanda kati ya nchi hizi mbili. Mazungumzo na Waziri Kacır yamejikita katika kukuza maendeleo ya viwanda vya kimkakati, kuimarisha matumizi ya teknolojia, pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika viwanda rafiki kwa mazingira. Mhe. Kapinga ameeleza dhamira ya serikali ya kutumia ushirikiano huo kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya mwaka 2050 ya kuwa nchi ya kipato cha kati cha juu kupitia mageuzi ya sekta ya viwanda, huku Uturuki ikiahidi kuendeleza ushirikiano wa kiufundi, kiteknolojia na ubunifu kwenye sekta hiyo. Kwa upande wa biashara, mazungumzo na Waziri Bolat yamejikita katika kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekezaji na kuongeza kiwango cha ...