BAROZI MATINYI AKABIDHI HATI KWA RAIS WA ALGERIA.
Na Mwandishi Wetu, Algeria. BAROZI wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, amekabidhi hati za utambulisho wa kibalozi kwa Mhe. Rais Abdelmadjid Tebboune wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya jijini Algiers, tarehe 10 Juni, 2026, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu ya kibalozi. Katika mazungumzo yao mafupi yaliyofuatia baada ya hafla hiyo, Mhe. Balozi Matinyi alimshukuru Mhe. Rais Tebboune, serikali na watu wa Algeria kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kudumisha ushirikiano wa kindugu wa nchi hizi mbili ambao umedumu kwa zaidi ya miongo sita. Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mazungumzo yake na Mhe. Rais Tebboune, Balozi Matinyi alisema kwamba walijadiliana namna ya kusonga mbele baada ya kufikia mafanikio mazuri katika sekta za ulinzi na elimu ya juu ili kuhakikisha watu wa nchi hizi wananufaika pia katika sekta zingine muhimu. Mh...