Machapisho

SINGIDA 0-AZAM 1 MPIRA NI MAPUMZIKO

Picha
NBCPL Ni mapumziko na mbili kibindoni…!!! HT: Dodoma Jiji 0-2 Azam FC  #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #DodomaJijiFC #AzamFC #DodomaJijiAzamFC

AFRIKA KUSINI YAONGEZA WANAJESHI KUKABILIANA NA MAGENGE YA DAWA ZA KULEVYA NA MAUAJI YA RAIA.

Picha
WANAJESHI wamepelekwa katika mitaa ya mji mkubwa zaidi nchini Afrika Kusini, Johannesburg, ili kukabiliana na uhalifu unaosababisha idadi kubwa ya watu kuuawa na mapigano kati ya magenge ya dawa za kulevya   Kwa habari zaidi tufuatilie kupitia you tube @habarikamilitv, Facebook habari kamili tv na kwenye blog @habarikamilitv

SERIKALI YAPENDEKEZA KUKUSANYA NA KUTUMIA SH. TRILIONI 62.334 KWA MWAKA WA FEDHA 2026/27

Picha
  Na Mwandishi Wetu.  WAZIRI wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27, ambapo katika kipindi hicho, inatarajia kukusanya nakutumia shilingi trilioni 62.334 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, maendeleo na kulipia deni la Taifa. Mhe. Balozi Omar amesema hayo wakati akiwasilisha Mpango huo ambapo amesema kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 10.3 ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2025/26. Tukio hilo limeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa pia na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu, na viongozi waandamizi wa Serikali.

RAIS DKT. SAMIA AMUASILI MTOTO ALIYETELEKEZWA GESTI WILAYANI NZEGA

Picha
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuasili Grace Samia Suluhu, mtoto mchanga aliyetelekezwa mjini Nzega, mkoa wa Tabora.  Dkt. Samia amesema kuwa, "Kila mtoto anayezaliwa ni baraka na hazina kwa jamii, tunao wajibu ndani ya Serikali na kila mwananchi kuhakikisha tunashiriki katika malezi, ulinzi, upendo na kesho ya watoto, kwani ndiyo kesho yetu na Taifa letu."   

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA AMALI MKOANI RUKWA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Rukwa.  WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumatatu, Machi 9, 2026 ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali ya Mkoa wa Rukwa iliyopo katika Kata ya Majengo, Namanyere, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa. Mradi huo unatekelezwa kupitia Programu ya Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 na unalenga kuboresha elimu ya ufundi stadi kwa kuwaandaa wanafunzi kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya Taifa. Mradi huo ulianza kutekelezwa Desemba 20, 2024 na ulitarajiwa kukamilika Machi 30 2025, ambapo hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo. Kwa mujibu wa taarifa ya mradi, hadi sasa ujenzi wa madarasa nane pamoja na jengo la utawala umekamilika na miundombinu hiyo tayari inatumika. Pia ujenzi wa jengo la TEHAMA na maktaba, nyumba ya mtumishi pamoja na vyoo vya wavulana na w...

DKT. MWIGULU: WANAFUNZI WATAKAOFAULU VIZURI KUSOMESHWA NJE YA NCHI KUPITIA SAMIA SCHOLARSHIP

Picha
  Awafikishia wanafunzi salamu za Rais Dkt. Samia; asema Serikali inaendelea kuwekeza katika elimu Na Mwandishi Wetu, Rukwa.  WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema wanafunzi watakaofaulu kwa viwango vya juu watanufaika na ufadhili wa masomo kupitia mpango wa Samia Scholarship unaotolewa na Serikali. Dkt. Mwigulu amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi katika ziara yake mkoani Rukwa, ambapo pia aliwasilisha salamu maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Daktari Samia Suluhu Hassan anasema kwa wale watakaofaulu kwa kiwango cha juu wanapata ufadhili asilimia 100. Na sio ufadhili tu wa asilimia 100 peke yake, asilimia 100 na unaenda kusoma nchi yoyote duniani… hiyo inaitwa Samia Scholarship,” alisema Waziri Mkuu. Aidha, alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu ambapo zaidi ya shule za sekondari 1,300, shule za msingi zaidi ya 2,700 pamoja na maelfu ya madarasa yamejengwa ka...

DKT. MWAMBA: TUMIENI JUKWAA LA WANAWAKE NA KODI KUTOA ELIMU

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amewataka Wanawake wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutumia Jukwaa la Wanawake na Kodi lililozinduliwa  hivi karibuni kuelimisha wajasiriamali wanawake kuhusu umuhimu wa kujisajili, kuwasilisha taarifa sahihi na kulipa kodi kwa wakati. Dkt. Mwamba ametoa wito huo wakati akizungumza na wanawake wa TRA,  katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo zilihudhuriwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Mcha Hassan Mcha, Kaimu Mkurugenzi Usimamizi Rasilimali watu na Utalawa Bw. Nahoda Pandu Nahoda.

PROF. KABUDI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 26 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JUMUIYA YA MADOLA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, London.  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Palamagamba J. Kabudi, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 26 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola (CFAMM) uliofanyika Machi 8, 2026 jijini London, Uingereza akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb). Akichangia mjadala, Prof. Kabudi amesema Jumuiya ya Madola inapaswa kubaki kuwa jukwaa muhimu la kushughulikia changamoto za maendeleo na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa (multilateralism) katika kipindi cha sasa chenye changamoto za kisiasa, kiuchumi na kimazingira. Katika masuala ya uchumi, Prof. Kabudi amesisitiza umuhimu wa kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya nchi wanachama kwa kujifunza kutoka mifano ya ushirikiano wa kikanda kama Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA). Amesema jukwaa la biashara na uwekezaji la Jumuiya ya Madola litasaidia kupunguza vikwazo vya biashara na kuongeza biashara kati ya ...

e-GA YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE UHUTAJI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Pwani.  KATIKA kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8, wanawake wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wametoa msaada wa mifuko 50 ya saruji, matofali 1,000 pamoja na mahitaji mbalimbali ya watoto katika Kituo cha kulea watoto yatima na waliofanyiwa ukatili cha Shalom kilichopo Kidenge B, Kata ya Msangani, Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani Machi 6, 2026. Akizungumza jana wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja wa Udhibiti na Viwango wa Mamlaka hiyo Bi. Sultana Seiff, alisema kuwa wanawake wa e-GA wameamua kusherehekea siku hiyo kwa kuwafikia watoto wanaohitaji msaada katika jamii na kukichagua kituo hicho ikiwa kama sehemu ya kurudisha kwa jamii. Meneja huyo alisema kuwa baada ya kuwasiliana na kituo hicho na kupata changamoto mbalimbali zinazohitaji kutatuliwa katika kituo hicho ikiwemo ujenzi wa uzio ili kuhakikisha Watoto hao wanakua salama waliamua kuchangia vifaa vya ujenzi pamoja na mahitaji mengine muhimu...

WANAWAKE TANTRADE WASHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI SAMBAMBA NA MIAKA 50 YA DHAHABU YA SABASABA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania (TanTrade) imeungana na Wanawake wote Duniani katika kusheherekea Siku ya Wanawake. Akiongea katika maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkuu TanTrade Dkt.Latifa Mohamed Khamis amesema "Leo, tunatambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Tunawapongeza wanawake wote kwa uongozi wao, uvumilivu, na kujitolea katika kuendeleza jamii zetu." TanTrade pia imetumia maadhimisho haya kuwakaribisha Wadau wote wa biashara kushiriki kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam - Sabasaba ya Jubilei ya Dhahabu ya 50. Ambapo watapata fursa za masoko mapya, teknolojia ya kisasa, na mtandao mpana wa kibiashara. Maadhimisho hayo yamefanyika Mburahati, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.