WANAWAKE TANTRADE WASHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI SAMBAMBA NA MIAKA 50 YA DHAHABU YA SABASABA
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania (TanTrade) imeungana na Wanawake wote Duniani katika kusheherekea Siku ya Wanawake. Akiongea katika maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkuu TanTrade Dkt.Latifa Mohamed Khamis amesema "Leo, tunatambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Tunawapongeza wanawake wote kwa uongozi wao, uvumilivu, na kujitolea katika kuendeleza jamii zetu."
TanTrade pia imetumia maadhimisho haya kuwakaribisha Wadau wote wa biashara kushiriki kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam - Sabasaba ya Jubilei ya Dhahabu ya 50. Ambapo watapata fursa za masoko mapya, teknolojia ya kisasa, na mtandao mpana wa kibiashara.
Maadhimisho hayo yamefanyika Mburahati, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.






Maoni