Machapisho

VIWANDA NA BIASHARA WAPANDA MITI KUMUUNGA MKONO RAIS, DKT. SAMIA KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA.

Picha
Na Mwandishi Wetu,  Dodoma. MITI imekuwa muhimili muhimu katika ukuaji wa Sekta ya Viwanda na Biashara kwani kupitia miti, viwanda hupata malighafi, biashara hukua, na uchumi huimarika. Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb.), Januari 27, 2026, akiwa ameambatana na Naibu Waziri,Mhe. Dennis Londo pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Needpeace Wambuya kushiriki zoezi la kupanda miti katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma.  Zoezi hilo ni sehemu ya kusherehekea kumbukizi ya  siku ya kuzaliwa ya  Mwanamazingira namba moja hapa nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye aliazimisha siku yake 27 Januari, 1960 kwa kupanda mti wa Muembe (Mangifera indica) katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 27 Januari, 2026. Aidha, Waziri Kapinga wakati akiongea na Watumishi wa Wizara hiyo baada ya kupanda mti, Altria rai kwa watumishi wa wizara ...

HALMASHAURI YA IGUNGA YAUNGANA NA WATANZANIA KUPANDA MITI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Igunga. MKURUGENZI  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid ameiongoza Menejimenti ya Halmashauri hiyo kupanda miti kwa lengo la kuitekeleza 27 ya kijani iliyoasisiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Selwa ameungana na viongozi hao leo,  ikiwa ni ishara ya kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia katika kumbukizi ya kazaliwa kwake. "Kipekee ninaishukuru na kuipongeza Menejimenti kujindaa na kushiriki zoezi hili baada ya masaa ya kazi kuungana na 27 ya kijani ikiwemo kumpongeza na kumtakia kila la kheri Mheshimiwa. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan," ameshukuru.  Ameeleza kuwa wamepanda miche 70 ambapo miche 50  yakivuli huku 20 ikiwa ni ya  matunda ambayo yatawafaidisha vizazi na vizazi.

IGUWASA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS, DKT. SAMIA KWA KUPANDA MITI.

Picha
  Tabora, Januari 27, 2026. Na Lubango Mleka, Igunga. KAATIKA kuunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu upandaji wa miti kama sehemu ya utunzaji wa mazingira, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Igunga (IGUWASA) imefanya zoezi la upandaji wa miti mbalimbali katika eneo la ofisi zake. Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mheshimiwa Rais, ambapo taasisi hiyo imeeleza kuwa inalenga kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kulinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho. Viongozi na watumishi wa IGUWASA wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Bi. Selwa  Abdallah Hamid wameshiriki katika zoezi hilo, wakisisitiza kuwa upandaji miti ni hatua muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa rasilimali za maji. IGUWASA imewahimiza wananchi kuiga mfano huo kwa kupanda ...

MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA GARI SHINYANGA 12 WAJERUHIWA

Picha
DEREVA wa Lori lenye namba za usajili RAE 848  Mali ya Kampuni ya Jaja ya nchini Rwanda amepoteza maisha baada ya kugongana uso kwa uso na basi la abiria namba T 229 EEL mali ya kampuni ya Kisire lililokuwa likitokea Kahama kwenda Mwanza na kusababisha Majeruhi 12. Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Januari 27 katika eneo la Tinde Mnadani na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Basi la Kisire aliyetaka kupita mkokoteni uliokuwa umebeba matunda na kuhama upande mwingine na kugongana uso kwa uso na lori hilo.

SERIKALI YAZINDUA MFUMO "ONGEA NA WAZIRI, MWANACHI KUPEWA SAUTI YA MOJA KWA MOJA SEKTA YA AFYA

Picha
  Na WAF, Arusha. SERIKAL imetangaza mwanzo wa enzi mpya ya uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi katika sekta ya afya baada ya kuzindua rasmi kwa mfumo wa kidijitali wa “Ongea na Waziri wa Afya” unaomuwezesha mwananchi kuwasiliana moja kwa moja na Wizara ya Afya saa 24 kwa siku. Hayo yamesemwa na Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa  hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Januari 26,2026 jijini Arusha. Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, amesema mfumo huo ni utekelezaji wa vitendo wa dhamira ya Serikali ya kuisogeza huduma ya afya karibu na mwananchi na kuhakikisha sauti ya wananchi inatumika kama dira ya maboresho ya huduma. “Mfumo wa "Ongea na Waziri wa Afya" unatuma ujumbe ulio wazi kuwa sauti ya mwananchi si ya pembeni, bali ndiyo msingi wa maamuzi ya Serikali katika kuboresha huduma za afya,” amesema Waziri Mchengerwa. Amefafanua kuwa uzinduzi wa mfumo huo ni mapinduzi makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa unajenga utamaduni mpya wa uongozi unaosiki...

HABARI PICHA

Picha
WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo Januari 26, 2026 amefanya kikao kazi na Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) chenye lengo la kujadili mikakati ya kuimarisha na kuendeleza utendaji wa wakala huo. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesm Mramba, Mwenyekiti wa Bodi ya PBPA, Dkt. Lutengano Mwakahesya, Mtendaji Mkuu wa PBPA, Bw. Erasto Simon, pamoja na Wajumbe wa Bodi na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati.

WIZARA YA MADINI YAJENGA MAABARA KUBWA YA KISASA DODOMA

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. WIZARA  ya Madini imetangaza ujenzi wa Maabara kubwa ya kisasa katika eneo la Nala, mkoani Dodoma, kwa lengo la kusaidia upimaji na utoaji wa taarifa sahihi za sampuli za madini. Maabara hiyo inatarajiwa kuwa kitovu cha utoaji wa huduma za madini kusini mwa Jangwa la Sahara. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema hayo leo Januari 26,2026 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha pili cha Awamu ya Sita ya Serikali. Amesema kuwa ujenzi wa maabara hiyo utaleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa Tanzania na nchi jirani, sambamba na kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani.  Aidha, Wizara imeingia makubaliano na GST ili taasisi hiyo iwe kitovu cha utoaji huduma za maabara kusini mwa Jangwa la Sahara. Katika kuongeza thamani ya madini, Waziri Mavunde amebainisha kuwa Wizara inaendelea kwa kasi na ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani, ambapo hadi sa...

SERIKALI YASAJILI ZAIDI YA WAFABIASHARA NDOGONDOGO 119,000 NCHINI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. SERIKALI kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imesajili jumla ya wafanyabiashara ndogondogo 119,595 katika Mfumo wa Usimamizi na Usajili wa Wafanyabiashara Ndogondogo (WBNMIS), hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kunufaika na fursa mbalimbali za maendeleo. Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa wizara hiyo, Mheshimiwa Dorothy Gwajima, amesema mafanikio hayo yamepatikana katika kipindi cha siku 100 za utekelezaji wa ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo Serikali imejikita katika urasimishaji wa wafanyabiashara, utoaji wa mikopo nafuu na uwezeshaji wa makundi maalum. "Kati ya waliosajiliwa wanawake ni 73,341 na wanaume 46,254, huku makundi yaliyosajiliwa yakijumuisha machinga 103,102, mama na baba lishe 12,384 pamoja na waendesha bodaboda na bajaji 4,109," Amesema Waziri Gwajima. Ameeleza kuwa katika ...

VIKUNDI 222 UYUI VYAWEZESHWA MIKOPO NAFUU YA BILIONI 1

Picha
   Na Allan Kitwe, Tabora. HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora imetoa mikopo nafuu isiyo na riba ya shilingi bilioni 1 kwa vikundi 222 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kuwainua kiuchumi. Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi za mikopo hiyo jana, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo Amoniche Mtweve amesema kuwa mikopo hiyo imetokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri. Ameongeza kuwa jumla ya wanachama 1,121 wanaounda vikundi hivyo wamenufaika na mikopo hiyo na kuwapa nguvu ya kuendeleza miradi yao ya biashara na uzalishaji mali katika maeneo yao. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Shabani Katalambula, amewataka wanufaika kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwezesha wananchi wengine kunufaika na mikopo hiyo katika awamu zijazo. Amefafanua lengo la mikopo hiyo kuwa ni kusaidia vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi kupitia miradi midogo midogo ya ujasiriam...

MADIWANI TABORA WAPEWA MAFUNZO YA UWAJIBIKAJI

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora MADIWANI wa halmashauri ya manispaa Tabora na Uyui Mkoani Tabora wamepewa mafunzo maalumu yatakayowawezesha kutekeleza wajibu wao kwa weledi mkubwa kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni. Akifungua mafunzo hayo leo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tabora Mohamed Katete amesema kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati mwafaka baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ili kuwajengea uwezo. Amebainisha kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa kuwa yatawaongezea weledi katika kusimamia utendaji wa halmashauri zao na kuongeza kasi ya kutumikia wananchi waliowachagua katika kata zao. ‘Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mafunzo haya yatolewe kwa madiwani wote nchini ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa weledi mkubwa na kukamilika kwa wakati’, ameeleza. Aidha amewataka kujenga mahusiano mazuri na wataalamu na watendaji wa halmashauri zao na kuhakikisha fedha zinazoletwa na serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo na z...