Na Mwandishi wetu, Mirerani MAMLAKA ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imewapatia zawadi ya vyakula, mbuzi na fedha taslimu, watoto yatima na waliokuwa wanaishi katika mazingira hatarishi wa kituo cha Light In Africa kwenye kusherehekea sikukuu ya Christmas na mwaka mpya wa 2026 kwa tabasamu. Afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani, (TEO) Isack Mgaya akizungumza wakati akikabidhi vyakula hivyo ameeleza kwamba gharama walizotumia kuwapatia tabasamu watoto hao ni shilingi 1,847,000. Mgaya amesema lengo lao ni kuwapa tabasamu kwenye sikukuu ya Christmas na mwaka mpya wa 2026 watoto hao wa kituo cha Light In Africa ambao ni yatima na waliokuwa wanaoishi katika mazingira hatarishi washerehekee kwa furaha. Amesema pamoja na kuwapa fedha taslimu shilingi 220,000 wametumia shilingi 1,627,000 katika kununua mahitaji mbalimbali ikiwemo mbuzi mmoja, nyama kilo 10 na vyakula kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hizo za mwisho wa mwaka. Ameele...