Machapisho

JAFO AANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KISARAWE

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Kisarawe. MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, ameanza utekelezaji wa ahadi alizozitoa wakati wa uchaguzi mkuu 2025 kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akitaja barabara, maji, afya na elimu kuwa miongoni mwa vipaumbele vyake vikuu katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe, Dkt. Jafo amesema tayari amewasiliana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuhusu barabara ya Kisarawe, hatua inayolenga kuhakikisha mkandarasi anaanza utekelezaji wa mradi huo kwa wakati. Katika sekta ya maji, amesema amefanya kikao na ujumbe kutoka Korea kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji utakaohusisha ujenzi wa vituo 105 vya kuchotea maji katika vijiji 17. Ameongeza kuwa ameomba kuzingatiwa kwa uwekaji wa matenki makubwa na kuangalia uwezekano wa kuvifikia vijiji vya Gwata na Dololo. “Eneo hili linahitaji matenki makubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu kufuatia uwepo wa ...

PBPA YAFUNGUA ZABUNI ZA UAGIZAJI MAFUTA KWA MWEZI FEBRUARI 2026 JIJINI DAR ES SALAAM

Picha
  Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam WAKALA ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) leo, Desemba 16, 2025, imetekeleza zoezi la ufunguzi wa zabuni za uagizaji mafuta kwa ajili ya mahitaji ya mwezi Februari, 2026 ambapo kampuni 8 kati ya 11 zimeshinda zabuni hizo katika vipengele tofauti. Zoezi hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa PBPA jijini Dar es Salaam, likihusisha wazabuni wa kimataifa na wa ndani, pamoja na wadau wa sekta ya nishati. Ufunguzi huo ni sehemu ya utaratibu wa kisheria na kikanuni wa kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya Mafuta ya kutosha na ya uhakika, huku ikizingatia misingi ya uwazi, ushindani wa haki, na gharama nafuu kwa mlaji wa mwisho. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa PBPA, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Petroli, Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Mhandisi Bruno Tarimo amewapongeza washindi wa zabuni hizo. "Nawapongeza wazabuni wote mlioshinda. Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, ninasisitiza kwa wasambazaji...

WANAFUNZI 40 WATEULIWA MABALOZI WA UTALII

Picha
  Mwandishi wetu, Babati. WANAFUNZI 40 wa sekondari katika.shule zilizopo katika eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge,wilayani Babati wameteuliwa kuwa mabalozi wa kuhamisha utalii na uhifadhi. Akizungumza katika hafla ya     kuwaaga wanafunzi hao kwenda kujifunza shughuli za Utalii katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na hifadhi ya Ngorongoro     Mkuu wa wilaya ya Babati mkoa wa Manyara,Emmanuela Kaganda    alisema wanafunzi hao baada ya ziara hiyo watakuwa mabalozi wa utalii na uhifadhi eneo la Burunge WMA ambalo ni muhimu sana kwa sekta ya utalii nchini. Ziara ya wanafunzi hao pamoja na.baadhi ya wazazi wao, walimu,maafisa elimu,viongozi wa serikali za vijiji na WMA imeanza leo Desemba 15 na itakamilika Desemba 18 imefadhiliwa na taasisi ya Chemchem Association   iliyowekeza shughuli za Utalii wa picha na hoteli za kitalii katika eneo hilo. Akizungumza wakati wa kuwaaga wanafunzi hao,Mkuu huyo wa wilaya amesema wanaf...

SIMANJIRO CHANGAMKIENI BILIONI 200 ZA RAIS SAMIA -OLE MILLYA

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro. NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Ole Millya, amewataka vijana wa wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, kuchangamkia fursa ya mikopo ya shilingi bilioni 200 zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan. Ole Millya ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Simanjiro amewataka vijana kuhakikisha wanaomba mikopo katika fedha hizo ambazo zinatolewa katika siku 100 za mwanzo wa utawala wa awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye kata ya Komolo wilayani Simanjiro, akiwahamasisha vijana kuchangamkia fursa hizo ili wajinufaishe kiuchumi. "Kuna shilingi bilioni 200 zinatolewa katika siku 100 za mwanzo wa utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan hivyo vijana wenzangu wa Simanjiro tuchangamkie fursa hiyo," amesema Ole Millya. Amewataka vijana wa Simanjiro kuandika miradi na kuomba mkopo kupitia fedha hizo kwani Tanzania nzima wanapaswa kupatiwa. "Vijana wa Simanjiro changamkien...

UPENDO WELLA AONYA UBADHIRIFU KWENYE MIRADI

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora MKUU wa Wilaya ya Tabora Upendo Wella amewataka Wataalamu, Watendaji na Madiwani wa Halmashauri ya manispaa Tabora kuongeza umakini kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na kujiepusha na vitendo vya ubadhirifu. DC ametoa onyo hilo juzi alipokuwa akiongea na Wakuu wa Idara, Watendaji na madiwani wa halmashauri ya manispaa hiyo ambapo aliwataka kuhakikisha miradi yote inasimamiwa ipasavyo ili ilete tija. Amedokea kuwa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi sana kwa ajili ya utekelezaji miradi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi. Ametaja baadhi ya miradi inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya Sita katika manispaa hiyo kuwa ni ujenzi wa stendi mpya ya kisasa, soko kuu, barabara za lami za mitaa zenye urefu wa km 10 na mingineyo. ‘Simamieni ipasavyo miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yenu ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, kinyume na hapo tutakuwa na mashaka na weledi wenu’, am...

WASIMAMIZI WA USAILI WAPEWA MAFUNZO MAALUM

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. KATIBU wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Mick Kiliba ameongoza kikao kazi cha Mafunzo kwa wasimamizi wa usaili Mkoa wa Dar es Salaam jana tarehe 14 Desemba, 2025 katika Ukumbi wa Karimjee. Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika kila mkoa Nchini yakiwa na lengo la kuwakumbusha wasimamizi wa usaili kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu za uendeshaji wa mchakato wa ajira ili kuhakikisha haki inatendeka na wasailiwa wanapata kazi kulingana na uwezo na umahiri waliouonyesha katika saili hizo. “Mwanzoni mwa mwezi wa kumi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa ahadi ya kuajiri nafasi 12,000 za kazi ndani ya siku 100 za kwanza baada ya kuapishwa, ambapo nafasi 5000 ni kwa kada za Afya na nafasi 7000 kwa kada za Elimu.  Sekretarieti ya Ajira ilishaanza kazi ya kutekeleza Maagizo hayo na leo hii nyinyi mmeteuliwa kuhakikisha adhma ya Mhe. Rais inatekelezwa kwa wakati ili kabla ya siku 100 kufika tuwe tumekamilisha kupata wat...

WAZIRI MKUU: WATANZANIA TUNZENI AKIBA YA CHAKULA

Picha
  ..Ahimiza matumizi ya mbolea na mbegu za mazao ya muda mfupi. Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania watunze akiba ya chakula walichonacho na waepuke matumizi yasiyofaa kutokana na hali ya kuchelewa kwa msimu wa mvua. Waziri Mkuu ametoa wito huo leo jioni (Jumapili, Desemba 14, 2025) wakati akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma. Amewaeleza viongozi hao kutoka mikoa ya Dodoma na Singida kwamba Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa utabiri wa mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli na mvua za msimu kwa kipindi cha Oktoba 2025 hadi Desemba 2025 na kipindi cha mwezi Novemba, 2025 hadi Aprili 2026 mtawalia.  “Kutokana na utabiri huo, baadhi ya mikoa nchini inatarajiwa kuwa na mvua za chini ya wastani hadi wastani na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usioridhisha,” amesema.  Amesema tathmini hiyo ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaonesha hali ya...

MHE. CHANDE AWAFUNDA WAHITIMU CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI MWEKA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro. NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amewataka wahitimu wa chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, kuzingatia uadilifu, uzalendo na unyenyekevu wakati wa kuhudumia wananchi na kulinda rasilimali za wanyamapori ili kuongeza thamani katika maendeleo ya ukuaji wa sekta ya utalii kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla. Mhe. Chande ametoa wito huo mkoani Kilimanjaro wakati wa mahafali ya 61 ya chuo hicho kilichopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo amewasisitiza wahitimu hao kutumia vyema maarifa na taaluma ya elimu  waliyopata kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa katika kuisaidia jamii kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kusaidia kutatua migogoro baina ya binadamu na Wanyamapori wakali na waharibifu. “Vyeti tu havitoshi, bali utekelezaji wa yale mliyojifunza na kufunzwa chuoni, hivyo  nendeni kuyaonesha kwa vitendo huko mnapokwenda, kwa sababu cheti ni karatasi lakini maarifa mliyoyapata katika...

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA LINDI MWAMBAO LTD CHAWEKA REKODI YA KUUZA TANI 41,000 ZA KOROSHO KATIKA MINADA MITANO

Picha
Na Lubango Mleka, Lindi. CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao kimeendelea kufanya vizuri katika msimu wa mauzo ya korosho baada ya kupeleka sokoni jumla ya tani 41,000 katika minada mitano iliyofanyika tangu kuanza kwa msimu huu. Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mnada wa tano uliofanyika katika Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi Mjumbe wa Bodi ya Lindi Mwambao Said Mwinyi amesema chama hicho kimeendelea kuhakikisha kuwa korosho za wanachama wake zinafika sokoni kwa wakati na kwa utaratibu unaotakiwa. Mwinyi amesema  katika minada yote mitano bei ya juu ya korosho imefikia shilingi 2,650 kwa kilo huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,170 hatua ambayo amesema inaonesha utulivu wa soko na mwitikio mzuri kutoka kwa wanunuzi. “Hadi sasa tumeshapeleka sokoni zaidi ya tani 41,000 za korosho, jambo ambalo linaonesha uimara wa chama na maandalizi mazuri tuliyofanya. Wanachama wetu wanaendelea kunufaika na mchakato huu wa mauzo,” amesma Mwinyi.

ECOWAS YATARAJIA KUKUTANA HII LEO JIJINI ABUJA NIGERIA

Picha
JUMUIYA  ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS inatarajiwa kukutana hii leo jijini Abuja nchini Nigeria, wakati huu ikitangaza hali ya hatari ya kikanda kufuatia kuongezeka kwa uongozi wa kijeshi na majaribio ya mapinduzi katika nchi za Mali, Burkina Faso, Niger, Guinea, na njama ya hivi punde zaidi nchini Benin ikitoa tahadhari mpya.

WAZIRI KIKWETE AAHIDI USHIRIKIANO KWA WATUMISHI WA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI

Picha
  Na. Mwandishi Wetu-Dar es Salaam WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameipongeza Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa kuongoza na kusimamia Ndege za Serikali kwa weledi na  ufanisi mkubwa. Waziri Kikwete amesema hayo Desemba 12, 2025 jijini Dar es salaam wakati alipotembelea ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa lengo la kujitambulisha. “Ninaipongeza Bodi kwa kuendelea kuwa washauri wazuri na kufanya uendelevu wa Wakala, binafsi ninaridhika na utendaji kazi wake. Pia Nitumie fursa hii kuwapongeza watumishi wote kwa ustadi wenu mkubwa wa kusimamia Ndege za Serikali, mimi na Naibu Waziri wa ofisi yangu Mhe. Regina Qwaray tunawahakikishia ushirikiano wa dhati wakati wote wa uongozi wetu” alisema Mhe. Kikwete. Aidha, Mhe. Kikwete amewapongeza kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ambao unaonekana kuridhisha viongozi wanawahudumia. Hivyo, ametoa rai pia kwa watu...